Umejibu hoja yangu kwa unyonge mwingi sana, tena naona unajaribu kubadilisha mada kwa porojo ambazo huwezi ukazidhibitisha. Inamaanisha kwamba unaelewa vizuri uhalisia wa mambo kama yalivyo. Tatizo lenu ni uongozi, sio majirani. Unakumbuka hizi kauli za ajabu ajabu kutoka kwa rais wenu? Mlianza kwa kupuuzilia mbali virusi vya Corona kisha mkaanza kujifukiza, wakati wataalamu tayari wamebainisha kwamba haisaidii chochote dhidi ya virusi na maambukizi ya COVID-19. Sasa hivi mmerukia kwenye dawa feki ya CVO kutoka Madagascar mmechanganyikiwa kweli kweli.