Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Bado nipo upande wa Tanzania

Upande uliopo wewe ni huu ambao kibongo bongo unayo nia ya kutaka kila upande usipime wageni wao ili kujiridhisha kwa sababu haka kaugonjwa ni kaupepo tu?

Haitakuwa una mpango wa siri wa kuwasambazia wenzio *ngwengwe* kisa tu wewe umeamua kuikumbatia?
 

Vyovyote utakavyochukulia au kuniita still itabaki vile vile.. Hakuna mwenye muda wa kubembelezana na vigeu geu.. I know where your strong hold is..Too bad. Njaa ikawakamata sawa sawa watakubali tu masharti.

Nchi yako ni super power ukanda huu, jivunie hilo na tembea kifua mbele kabisa bila wasi wasi. So we dictate terms and not otherwise.

Halafu mpende Raisi wako Mh. Magufuli, he has done so much for this country for a short period of time.
 
Hivi huoni aibu kwamba kwenye huu uzi wako ni wewe tu uko hapa kuwapigania Wakenya?

Mipaka imefungwa baada ya Wakenya kukiuka makubaliano, sasa kelele za nini? Wewe ndio Kenyata?

Mwenzako bia yenu bado anausoma uzi. Wewe Instagram panakufaa zaidi.

Kwani hata stamina ya kusoma tu unayo achilia mbali ya kujibu hoja?
 
Unachokieleza hapa na kile kinachoelezwa na madereva ni vitu viwili tofauti na ndiyo maana kuna member amekwambia hufuatilii taarifa za habari.
 

Mkuu utakuwa umenisoma ndivyo sivyo. Si kila mtu ni mwita watu wengine majina kijinga jinga.

Ila nilifurahi kupata uthibitisho wako kuwa mpaka ulikuwa umefungwa uthibitisho ambao kama ungetoka moja kwa moja tokea kwa waziri Profesa Kabudi (waziri wa mambo ya nje) ningelijua kuwa ulikuwa ni final and terminate.

Mkuu kwamba kuna migongano huko mipakani, mawazo yangu yako kwenye uzi yako wazi kabisa. Ni sababu ya kuwa Tanzania peke yake kama nchi, tuko nje ya protocols hizi za pamoja for whatever good or bad reasons of our own.

Miye kama binadamu mwenye haki ya kutafakari mizani inalalia wapi, ninayo haki ya kutambua kiini cha mzozo, mhusika mkuu, na hata mhanga ni nani.

Msema kweli ni mpenzi wa Mungu hivi sasa pana migogoro na wa kulaumiwa yupo. Nani wa kulaumiwa kwenye hili? Kwa sababu nilizoainisha wazi wazi kwa nionavyo miye wa kulaumiwa ni sisi.

Kama wewe unaona ni wao, sababu zako ziko wapi? Hawa wenzetu wewe ungetaka labda wafanye je ili kupisha hii migogoro?

Mkuu nitatembea vipi kifua mbele wakati dhamira yangu inanishitaki kuwa pana udhalimu wa nchi au washirika wangu mahali fulani?
 
Unachokieleza hapa na kile kinachoelezwa na madereva ni vitu viwili tofauti na ndiyo maana kuna member amekwambia hufuatilii taarifa za habari.

Nilichoandika kuhusiana na alivyosema aliye ongelea dereva kuhusiana na Rwanda kipo hapa chini. Kama nililichokieleza hapa ni kweli tatizo liko wapi?



Kama nilichoeleza hapo si kweli weka ukweli hapa tuuone. Tatizo liko wapi?

Kwa nini kuandikia mate wakati wino upo?

Kistaarabu hoja hupingwa kwa hoja si mipasho ya kwenye mirindimo ya pwani.
 
Kwa akili zako unahisi vipimo vinavyofanyika Ni vya corona tu...Kuna nchi zingine wanataka vipimo zaidi ya corona Kama yellow fever, Hepatisi A, HIV, TB, etc na still wanatrust hayo majibu as long as yametoka kwenye channel sahihi..vp kwa hao mbulula unaowatetea. Mmekaa mmekubaliana kwamba kifanyike Hiki Sasa vp uanze kuweuka...if ulikua na doubt Kuna channels sahihi ambazo walitakiwa kufanya..na si kukurupuka na kuanzisha uchochoro wako mwingine..tuache ujina jameni.
 
Nakuuliza swali unaangalia taarifa za habari kuhusu sakata hili? Nakuuliza hivyo kwa sababu madereva huwa wanaeleza kero pamoja na kufuata masharti ya hizo nchi.
 

Punguza mapovu bro. Mkataba na ACACIA tulipoona haufai tuliupiga chini. Jambo la heri sana kuwa tutafanya hivyo kwa makubaliano yoyote wakati wowote tukigundua kuwa hakuna tija wala maslahi. Kwetu. Hali hiyo haiwezi kuwa copyright yetu peke yetu. Kila mtu yu ana hali hiyo.

Wewe kwenye haya huna unaloona linatufaa sote?

1. Kila mtu apime wageni wake
2. Tuwe na maabara za pamoja.

3. Kama haya yote hayawezekani basi tufunge tu mipaka.

Katika hali yoyote rekodi huwekwa sawa yaani kuna mtu ambaye kayafikisha mambo hapo.

Kwa hali hii labda kukuuliza tu mburula wee, nini kifanyike hapa kutokufikia hii hatua ya 3 ambayo nayo ni option pia?

Au nani afanye vipi kuonyesha haki inatendeka?
 
Wewe Ni nani paka utoe hayo masharti nje ya Yale walivyokubaliana?
 
Nakuuliza swali unaangalia taarifa za habari kuhusu sakata hili? Nakuuliza hivyo kwa sababu madereva huwa wanaeleza kero pamoja na kufuata masharti ya hizo nchi.

Mbona miye nimekuwa naweja hoja zangu hapa? Weka hoja zako hapa tuzione.

Hoja hujibiwa kwa hoja mkuu.

Taarifa zote za habari naangalia na kufuatilia mambo kwa kina pia. Tuliambiwa akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu.
 
Umenunuliwa na mabeberu huna jipya
Kajipange upya
 
Mbona miye nimekuwa naweja hoja zangu hapa? Weka hoja zako hapa tuzione.

Hoja hujibiwa kwa hoja mkuu.

Taarifa zote za habari naangalia na kufuatilia mambo kwa kina pia. Tuliambiwa akili za kuambiwa tuchanganye na za kwetu.
Kama unafuatilia taarifa za habari sasa hayo unayoeleza wewe umeyapata wapi?
 
Wewe Ni nani paka utoe hayo masharti nje ya Yale walivyokubaliana?

Miye ni mtanzania Mzalendo tu nisiyependa kuona migogoro isiyokuwa na kichwa wala miguu ikiendelea.

Kwa hiyo umeshindwa kujibu siyo kuwa baina ya haya mawili:

1. Kila mtu apime wageni wake
2. Tuwe na maabara ya pamoja

Umeshindwa hata kupendekeza kwa mawazo yako tu nini kifanyike kama inawezekana ili mpaka usifungwe?

Uungwana mbona ni kitu cha bure ndugu. Ni wazi kuwa pana kauungwana tokea kwetu hakapo au hakakuwapo tokea mwanzo.

Wakitutuhumu kuwa kumbe tulikuwa na kampango ka siri ka kuendelea kuwaambukiza haka upepo utasema je?

Hebu kuwa mtu mzima kidogo.
 
Umenunuliwa na mabeberu huna jipya
Kajipange upya

Hoja hujibiwa kwa hoja siyo kwa mipasho.

Utakuwa unatumika na mabeberu wewe huna jipya wala huoni sababu ya kulinda maslahi yetu sisi kama watanzania.

Hujui hutaki nini wala unataka nini. Bure kabisa!
 
Unazijua kero za kupimia madereva mpakani? Umefuatilia ata kidogo kinachoendelea mpaka wa Kenya na Uganda Kule Malaba? Unapendekeza ujinga alaf unajiona genious. Vipimo vinachukua zaidi ya 24hrs huo msongamano hapo mpakani unauhandle vp?
 
Kama unafuatilia taarifa za habari sasa hayo unayoeleza wewe umeyapata wapi?

Soma uzi. Kama bado kapa - zipo Facebook na Instagram kwa ajili yako.

Pole lakini.
 
Unazijua kero za kupimia madereva mpakani? Umefuatilia ata kidogo kinachoendelea mpaka wa Kenya na Uganda Kule Malaba? Unapendekeza ujinga alaf unajiona genious. Vipimo vinachukua zaidi ya 24hrs huo msongamano hapo mpakani unauhandle vp?

Mapendekezo yako yako wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…