Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Mkorofi ni huyu aliyekuja kugundua kuwa jamaa wanakuja na vyeti kuwa hawana Corona kwa mujibu wa makubaliano lakini kiuhalisia wana Corona kinyume cha makubaliano.

Na sisi tunachotaka utaratibu huu huu uendelee tu kwa sababu ndiyo tuliokubaliana?

Ndiyo hivyo mkuu?

Sasa aligundua vipi waliovuka wana corona kama hakuvunja makubaliano kwanza kwa kuanza kupima upya? Na alifuata utaratibu gani wa kuvunja hayo makubaliano? Alumwambia nani madai yake? Au alikuruouka tu na kuanza kupima bila taratibu?

Ndivyo inavyokuwa hivyo? Kama sio ubabe na kiburi ni kitu gani kilifanya waanze kutoka nje ya makubaliano bila kushirikisha upande wa pili?
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada ili kumfunga paka huyu kengele.

Tunayoyashudia sasa hivi mipakani ni wazi kuwa yataendelea kwa muda mrefu tu na bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Ni wazi kuwa Tanzania kwa kukataa kuwemo katika protokali za pamoja kuhusiana na ugonjwa huu katika EAC au katika zile za dunia kupitia WHO, hakuna namna yoyote ambayo sisi tunaweza kuwa na mashirikiano au maingiliano na wengine pasipokuwa na migongano.

Tanzania imekuwa ikipotosha kauli na misimamo inayotolewa WHO ambayo kwa hakika imekuwa ikizingatiwa na mataifa takribani yote duniani. Mfano:

1. WHO inatambua ugonjwa huu kuwa ni janga la kimataifa. Kuwa ugonjwa huu ni hatari, unauwa, hauna dawa wala chanjo ya kujikinga nao.

Tanzania badala yake inatambua kuwa huu ugonjwa ni kaupepo tu ambako katapita. Tanzania pia inauona huu ugonjwa kuwa ni vita vya kiuchumi vya mabeberu dhidi yake. Tanzania inatambua kuwa tiba ya ugonjwa huu ipo. Ya kwamba nyungu ya kujifukiza, mitishamba na maombezi vinatambulika rasmi kama suluhu yake kamili.

2. WHO inatambua kuwa ugonjwa huu ungalipo na kuwa kama hatua stahiki za kuudhibiti hakuna, basi utaendelea kusambaa na hali kuwa hata mbaya zaidi.

Hata hivyo WHO inatambua ugonjwa huu utakuwapo kwa muda mrefu na kama jitihada sahihi za kuudhibiti zikiwapo, basi tunaweza kuendelea na maisha hata kama ugonjwa ungalipo hadi pale tiba au chanjo vitakapogunduliwa.

Tanzania kwa upande wake inaamini kuwa ugonjwa huu umeshakwisha hali hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazochukuliwa kuumaliza au kuuzuia kuendelea kusambaa. Msisitizo umekuwa zaidi kwenye kulinda uchumi, yaani kwenye kuwataka watu wake kuchapa kazi tu. Ya kuwa corona ni kaugonjwa kadogo tu kanakopita.

Katika EAC wanayatambua yote haya mawili tokea WHO vilivyo, isipokuwa kwa Tanzania tu.

Nchi nyingine zote katika EAC zinatambua umuhimu wa kuwaweka wananchi wao salama dhidi ya ugonjwa huu hata kama ni kwa kuuweka uchumi wa nchi zao hatarini.

Nchi nyingine zote katika EAC haziko tayari kusubiria wananchi wao kufa kwa Corona, bali wako tayari kufa wakati wakipambana nayo.

Nchi nyingine zote katika EAC ziko tayari kuishi na Corona iliyodhibitiwa. Katika hili, nchi hizo haziko tayari kuruhusu mgeni yeyote kuingia katika nchi zao bila ya wao kujiridhisha kwanza kuhusiana hali yake ya Corona ikoje.

Ukiangalia mfululizo wa protocols hizi ni wazi kuwa hapa pana "mwana mkaidi ambaye huyo yeye kufaidi ni mpaka siku ya Iddi!"

Tanzania tunapaswa tujitathmini. Hayupo mchawi bali ni sisi wenyewe. Tumekuwa kama watoto watukutu.

Wala tusimsubiri mno wa kuja kutufunga paka sisi kengele! Mbona sasa tunapitiliza mno?

***** ***** zote hizi huko mipakani, ni wazi kuwa washari ni sisi.

Kama sisi tumeamua kuishi na Corona tukiichukulia poa tusilazimishe hilo na kwa wengine pia.

Kama hatukubali raia wetu waendao kwa wenzetu kupata ruhusa za kuingia kwa kufuata masharti yaliyoko huko, basi na tuifunge tu hii mipaka. Vinginevyo migogoro hii isiyokuwa na tija itaendelea huku mkiwahimiza waathirika wa mitafaruku hii kuwalipa nyie kodi na vitisho vya mafaini juu.

Kwani hamzioni biashara za watu zinavyodorora huko mipakani? Kwani mnadhani wafanyabiashara hao watatoa wapi pesa za kuwalipa nyie kodi tena kwa wakati na kwa shuruti zenu?
Acha kuongea upuuzi brazaj.
Hao unaowaita jirani zetu unajua kwanini wanaendelea kushupalia lockdown???

Kabla hujaongea hoja fikiri kwa kina na kwa mapana.

Wanafunga mipaka na kusisitiza lockdown si kwa matakwa yao bali ni kwa matakwa ya mabeberu waliowapa misaada na mikopo ya pesa nyingi kupambana na corona hewa.

Wameomba pesa kwakili ya corona ....lazima waoneshe na waishi kama vile corona ipo kumbe si kwa kiasi hicho wanacho tuaminisha.

Yawezekana corona ipo nchini lakini si kwa kiwango kinachotishia na kusababisha shughuli za kimaendeleo kusimama.

Binafsi nasifia sana umahiri wa Raisi wangu JPM hasa ktk kipindi hiki cha corona. Kama Taifa ametuunganisha na kutujenga kiimani kwa kutuondolea hofu ya kipumbafu kabisa.

brazaj jaribu kufikiri kabla hujaongea
 
Umeonesha wasiwasi na vyeti vya Corona vya Tanzania eti kwa sababu tuna 'vitu hewa', au sio? Na kama tunatoa majibu feki kwa madereva wetu, kwa kutumia hiyo dhana yako ya 'Kila mtu apime wageni wake', ni kitu gani kitatuzuia kutoa majibu 'feki' kwa madereva toka Kenya na nchi zingine kama tukiwapimia huku kwetu?

Eti tuanzishe maabara ya pamoja, are you serious? Yaani maderva/wasafiri mamia kwa maelfu wapange foleni kwenye maabara moja kwa sababu ya kutokuiaminiana kwa nchi zetu? Itaanzishwa kwa gharama za nani? Itakuwa wapi? Itasimamiwaje? Haaaa! Kama imani ni ndogo kiasi hicho kwa nini mipaka isifungwe tu kabisa?

Bottom line: Kuruhusu madereva wa Kenya (au nchi nyingine) wapite kuja kwetu wakati wao hawaruhusu watu wetu kwenda kwao ni dharau kubwa na haipaswi kuungwa mkono na Mtanzania yoyote anayejielewa. Kama wao wanaamini sisi sio salama kwa nchi zao wafunge mipaka yao, na wafuate utaratibu wetu tukitaka baadhi ya watu wao wavuke mipaka yetu kwa manufaa ya nchi.

Mkuu hawa jirani zetu nao ni watu:

1. Wana wasiwasi na vyeti vyetu kwa kuwa wameona watu wetu wana vyeti kuwa hawana Corona wakati wana Corona. Hivyo vyeti vyetu hawavitambui tena. Bila shaka ndiyo maana wanaona bora kila mtu apime wageni wake kwa sababu zilizoorodheshwa kwenye uzi.

2. Kuna mapendekezo ya maabara ya pamoja. Haya unayakataa kuwa eti foleni. Utaratibu wa kuepuka foleni si utawekwa mkuu? Pia hili si litawahusu wageni wote wa pande zote mbili?

Kama haya hayawezekani option inavyotakiwa ni kuwa mpaka ufungwe.

Sasa hii bottom line yako inatokea wapi mkuu wakati mpaka utakuwa umefungwa?

"Bottom line: Kuruhusu madereva wa Kenya (au nchi nyingine) wapite kuja kwetu wakati wao hawaruhusu watu wetu kwenda kwao ni dharau kubwa na haipaswi kuungwa mkono na Mtanzania yoyote anayejielewa. Kama wao wanaamini sisi sio salama kwa nchi zao wafunge mipaka yao, na wafuate utaratibu wetu tukitaka baadhi ya watu wao wavuke mipaka yetu kwa manufaa ya nchi."
 
Sasa aligundua vipi waliovuka wana corona kama hakuvunja makubaliano kwanza kwa kuanza kupima upya? Na alifuata utaratibu gani wa kuvunja hayo makubaliano? Alumwambia nani madai yake? Au alikuruouka tu na kuanza kupima bila taratibu?

Ndivyo inavyokuwa hivyo? Kama sio ubabe na kiburi ni kitu gani kilifanya waanze kutoka nje ya makubaliano bila kushirikisha upande wa pili?

Sasa mkuu hapo si sawa na kupima mbuzi, oil, mapapai au kware ili kujiridhisha?

Si alikuwa anajiridhisha tu?

Nyie mlitaka ameze tu matango pori mnayomsokomezea mdomoni?

Kwa hiyo kustuka kwake sasa sisi ndiyo tumekasirika kuwa kavunja makubaliano na kuwa mkorofi ni yeye?

Mbona maajabu ya Mussa basi?
 
Acha kuongea upuuzi brazaj.
Hao unaowaita jirani zetu unajua kwanini wanaendelea kushupalia lockdown???

Kabla hujaongea hoja fikiri kwa kina na kwa mapana.

Wanafunga mipaka na kusisitiza lockdown si kwa matakwa yao bali ni kwa matakwa ya mabeberu waliowapa misaada na mikopo ya pesa nyingi kupambana na corona hewa.

Wameomba pesa kwakili ya corona ....lazima waoneshe na waishi kama vile corona ipo kumbe si kwa kiasi hicho wanacho tuaminisha.

Yawezekana corona ipo nchini lakini si kwa kiwango kinachotishia na kusababisha shughuli za kimaendeleo kusimama.

Binafsi nasifia sana umahiri wa Raisi wangu JPM hasa ktk kipindi hiki cha corona. Kama Taifa ametuunganisha na kutujenga kiimani kwa kutuondolea hofu ya kipumbafu kabisa.

brazaj jaribu kufikiri kabla hujaongea

Mkuu tukae kwenye kufunga mpaka. Kwa nini tusikubali moja katika haya:

1. Kila mmoja apime wa kwake
2. Maabara ya pamoja
3. Tufunge mpaka.

Tukajikita na yetu maana sisi msimamo wetu hata kama Corona siyo pandemic si wetu?

Hata kama sisi nyungu ni dawa kama wao si dawa si wao?

Kwa nini tunataka kuwapimia wageni wao?

Kama wao wameshupaa na lockdown si wao. Inakuuma nini wewe?

Wastarabu huwa hawatumii matusi. Upuuzi ni tusi na si ustaarabu. Pia si busara kudhani kuna anayeweza kuandika bila kufikiria.

Zaidi sana hoja hujibiwa kwa hoja.
 
Sasa mkuu hapo si sawa na kupima mbuzi, oil, mapapai au kware ili kujiridhisha?

Si alikuwa anajiridhisha tu?

Nyie mlitaka ameze tu matango pori mnayomsokomezea mdomoni?

Kwa hiyo kustuka kwake sasa sisi ndiyo tumekasirika kuwa kavunja makubaliano na kuwa mkorofi ni yeye?

Mbona maajabu ya Mussa basi?

Dawa ya moto ni moto. Katumia ubabe kupima bila kufuata makubaliano na sisi DC kafunga mpaka. End of story.
 
Mkuu nimekusoma. Kati ya wawili hawa yupo mmoja mkorofi.

Akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Ni vizuri unayajua mawazo yangu yapo kwenye title. Lengo likiwa wazi: "kumfunga paka kengele".
 
Vizuri kama umeelewa.
 
Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada ili kumfunga paka huyu kengele.

Tunayoyashudia sasa hivi mipakani ni wazi kuwa yataendelea kwa muda mrefu tu na bila ya kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.

Ni wazi kuwa Tanzania kwa kukataa kuwemo katika protokali za pamoja kuhusiana na ugonjwa huu katika EAC au katika zile za dunia kupitia WHO, hakuna namna yoyote ambayo sisi tunaweza kuwa na mashirikiano au maingiliano na wengine pasipokuwa na migongano.

Tanzania imekuwa ikipotosha kauli na misimamo inayotolewa WHO ambayo kwa hakika imekuwa ikizingatiwa na mataifa takribani yote duniani. Mfano:

1. WHO inatambua ugonjwa huu kuwa ni janga la kimataifa. Kuwa ugonjwa huu ni hatari, unauwa, hauna dawa wala chanjo ya kujikinga nao.

Tanzania badala yake inatambua kuwa huu ugonjwa ni kaupepo tu ambako katapita. Tanzania pia inauona huu ugonjwa kuwa ni vita vya kiuchumi vya mabeberu dhidi yake. Tanzania inatambua kuwa tiba ya ugonjwa huu ipo. Ya kwamba nyungu ya kujifukiza, mitishamba na maombezi vinatambulika rasmi kama suluhu yake kamili.

2. WHO inatambua kuwa ugonjwa huu ungalipo na kuwa kama hatua stahiki za kuudhibiti hakuna, basi utaendelea kusambaa na hali kuwa hata mbaya zaidi.

Hata hivyo WHO inatambua ugonjwa huu utakuwapo kwa muda mrefu na kama jitihada sahihi za kuudhibiti zikiwapo, basi tunaweza kuendelea na maisha hata kama ugonjwa ungalipo hadi pale tiba au chanjo vitakapogunduliwa.

Tanzania kwa upande wake inaamini kuwa ugonjwa huu umeshakwisha hali hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazochukuliwa kuumaliza au kuuzuia kuendelea kusambaa. Msisitizo umekuwa zaidi kwenye kulinda uchumi, yaani kwenye kuwataka watu wake kuchapa kazi tu. Ya kuwa corona ni kaugonjwa kadogo tu kanakopita.

Katika EAC wanayatambua yote haya mawili tokea WHO vilivyo, isipokuwa kwa Tanzania tu.

Nchi nyingine zote katika EAC zinatambua umuhimu wa kuwaweka wananchi wao salama dhidi ya ugonjwa huu hata kama ni kwa kuuweka uchumi wa nchi zao hatarini.

Nchi nyingine zote katika EAC haziko tayari kusubiria wananchi wao kufa kwa Corona, bali wako tayari kufa wakati wakipambana nayo.

Nchi nyingine zote katika EAC ziko tayari kuishi na Corona iliyodhibitiwa. Katika hili, nchi hizo haziko tayari kuruhusu mgeni yeyote kuingia katika nchi zao bila ya wao kujiridhisha kwanza kuhusiana hali yake ya Corona ikoje.

Ukiangalia mfululizo wa protocols hizi ni wazi kuwa hapa pana "mwana mkaidi ambaye huyo yeye kufaidi ni mpaka siku ya Iddi!"

Tanzania tunapaswa tujitathmini. Hayupo mchawi bali ni sisi wenyewe. Tumekuwa kama watoto watukutu.

Wala tusimsubiri mno wa kuja kutufunga paka sisi kengele! Mbona sasa tunapitiliza mno?

***** ***** zote hizi huko mipakani, ni wazi kuwa washari ni sisi.

Kama sisi tumeamua kuishi na Corona tukiichukulia poa tusilazimishe hilo na kwa wengine pia.

Kama hatukubali raia wetu waendao kwa wenzetu kupata ruhusa za kuingia kwa kufuata masharti yaliyoko huko, basi na tuifunge tu hii mipaka. Vinginevyo migogoro hii isiyokuwa na tija itaendelea huku mkiwahimiza waathirika wa mitafaruku hii kuwalipa nyie kodi na vitisho vya mafaini juu.

Kwani hamzioni biashara za watu zinavyodorora huko mipakani? Kwani mnadhani wafanyabiashara hao watatoa wapi pesa za kuwalipa nyie kodi tena kwa wakati na kwa shuruti zenu?

Kupitia hoja zako.

1. Tanzania inatambua ni janga la kimataifa ndio maana kupitia serikali imetangaza hatua mbali mbali za kukabiliana nalo kama zilivyofanya nchi zingine na kwa njia tofauti katika kuwalinda wananchi wake km baadhi ya nchi zilivyofanya. Lakni pia TANZANIA INATAMBUA NDANI YA JANGA HILI KUNA VITA VINGINE NDANI YAKE VINAPIGWA KUPITIA HILI HILI JANGA kama ulivyotaja na sio kitu kibaya kwani kila mtu ana ubongo wake na kila serikali ina mamlaka yake katika kufanya maamuzi na kuchanganua yanayo endelea.

2. Tanzania haijawahi kusema kama kuna Dawa ya Corona hoja hizi ni wewe ndio umeamini hivyo, hizo nyungu na vitu vya asili ni vitu vilivyotangazwa ikiwa ni moja ya hatua za mtu kufanya ili kuweza kujiepusha au kufubaza corona km utakua nayo kutokana na dalili zake na magonjwa yanayoambatana baada ya mtu kuambizwa vitu hivyo vinasaidia mtu kumaliza hizo dalili. Kwanza kati ya vilivyopigiwa upatu, vingi vimetoka huko huko kuliko anzia.

Kuhusu protokali unayosema, nchi zote za EAC zimefunga mipaka huku Tanzania ikiwa katikati.. ifunge isifunge hao raia wake wataenda wapi kwenda nje ya nchi wakati nchi hizo zimefunga mipaka yake?

Na ukumbuke nchi hizo hizo zilitangaza kufunga mipaka isipokua malori ya mizigo na bidhaa na nchi zote hizo zinategemea vitu hivyo kutoka Tz. Tanzania imekubali kupeleka malori hayo na bidhaa hizo ni zao nchi hizo.

Tanzania ilizuia wananchi kusafiri nje ya nchi kwa kufunga Airport zake zote.. vivo hivyo nchi jirani zilifunga pia.

Sasa kama wao walitaka malori yawe yanaenda walita yajiendeshe..? Na kama hawakutaka dereva wetu wasiende wana corona kwann wasingekuwa wanaleta malori yao na madereva wao..?

Nchi hizo zimefunga mipaka na kufungia watu ndani lkn kila kukicha ni wao wao wanaotangaza kuwa na wagonjwa kila kukicha japo wamewafungia watu, hio corona inasambaaje sasa kama watu wako ndani?

Hakuna sababu ya Tz kulaumiwa nchi hizo zina wivu tu na Tz.
 
Kinacho wasumbua jirani zetu ni mikopo waliyochukua kwa ajili ya mapambano ya Covid 19. Masharti ya mikopo hio ni magumu sana ndio maana wanakuwa wakali kwa Tz kwasababu tu ya wivu na si kitu kingine.
 
Muda wote nakuona unawaambia wachangiaji wajikite kwenye hoja husika ila kumbe wanakuiga wewe. Maana naona unaruka ruka tu kwa ishu mbali mbali. Hapa ishu ni corona na mipaka.

Sasa hao kenya waliingia kwenye makubaliano ya nini kama hawaamini vipimo vyetu? Na hata hivyo kwa nini hawakuwa wazi kwamba wanavunja makubaliano kwa kufuata njia sahihi badala yake wakaanza kupima upya?

Unadhani kenya ina mamlaka makubwa kuliko nchi yako? Kwamba inaweza tu yenyewe kuvunja makubaliano bila kufuata taratibu? Unadhani kwenye hili saga ni upande upi uko sahihi?
Jamaa kafungua thread alafu ana majibu yake nawaonea huruma mnayebishana naye.

Huyu mpiga ramli kaanza mda mara lockdown,mara maambukizi yataongezeka wakitoa lockdown sasa hivi kaanza kulaumu.

Mtu mwenyewe habari hatazami,watu wamefanya mkutano wakakubaliana kila mtu apime watu wake na cheti atakachopewa dereva kiheshimike na pande zote.Sisi vyao tunaviheshimu wao vyetu hawa viheshimu,sasa utafanyaje zaidi ya ww kufunga.Manake kama makubaliano kayavunja mwenyewe Kenya kwa kutokuheshimu vyeti vya TZ.

Manake unailamu Tanzania anasahau,Kenya nao wana mgogoro na Uganda unaofanana na huu.

brazaj endelea kupiga ramli lakini chombo ina yeya,kama vip hamia Kenya manake kitu kidogo "umeona Kenya" ukishindwa jifungie ndani ucheze kidali poo na mkeo pamoja na watoto wako.
 
Manake unailamu Tanzania anasahau,Kenya nao wana mgogoro na Uganda.

brazaj endelea kupiga ramli lakini chombo ina yeya,kama vip hamia Kenya manake kitu kidogo "umeona Kenya" ukishindwa jifungie ndani ucheze kidali poo na mkeo pamoja na watoto wako.

Huyo jamaa kama umemsoma vizuri kuna kitu anakitaka, yuko after something. Sasa majibu aliyoyapata humu kutoka kwa wachangiaji mbali mbali yanamtosha. Nadhani picha kamili kaipata.
 
Mkuu kwa takwimu za masaa 24 yaliyopita marekani wenye states takribani 52 walikuwa na vifo 97 na maambukizi mapya 4026.

Kama jimbo moja ni mithili ya nchi moja, basi kila state (yaani nchi) ilikuwa na vifo takribani viwili na maambukizi mapya yasiyozidi 77 kwa jana peke yake.

Inawezekana kuwa hali ya vifo na maambukizi ya Corona marekani ni ndogo zaidi kwa jana hiyo kuliko huku kwetu. Yaani si Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda nk ambako uwezo wa kupima ni dhaifu achilia mbali nia ya kuficha takwimu sahihi ilivyo kubwa tunaweza kuwa na takwimu zenye kuelekea kuleta matumaini kama hivyo.

Beberu marekani? Huyo mbona siyo size yetu mkuu? Kwamba hata tunayo haja ya kumhurumia? Mbona itakuwa kujimwambafai pasipokuwa na mashiko?

Tupambane na hali yetu tu mkuu. Hofu na mashaka yetu tukiyaelekeza zaidi kule Sumve, ikungu lya bashashi, Gamboshi huko nk, tutakuwa tumejitendea haji zaidi nadhani.
iNAWEZEKANA,ILA KWA SASA WATU WANAHOJI BAADA YA HAYA AANDAMANO YALIYOTOKEA SEHEU MOJA,HALI YA MAAMBUKIZI ITAKUA VIPI.
 
Huyo jamaa kama umemsoma vizuri kuna kitu anakitaka, yuko after something. Sasa majibu aliyoyapata humu kutoka kwa wachangiaji mbali mbali yanamtosha. Nadhani picha kamili kaipata.

Mkuu kama umedhani kuwa niko after anything umenoa.

Uzi uko wazi kwa title na contents. Penda usipende kila kitu kimesimama.

"Mtanzania wa leo siyo wa jana." Mwisho wa kumnukuu.
 
Jamaa kafungua thread alafu ana majibu yake nawaonea huruma mnayebishana naye.

Huyu mpiga ramli kaanza mda mara lockdown,mara maambukizi yataongezeka wakitoa lockdown sasa hivi kaanza kulaumu.

Mtu mwenyewe habari hatazami,watu wamefanya mkutano wakakubaliana kila mtu apime watu wake na cheti atakachopewa dereva kiheshimike na pande zote.Sisi vyao tunaviheshimu wao vyetu hawa viheshimu,sasa utafanyaje zaidi ya ww kufunga.Manake kama makubaliano kayavunja mwenyewe Kenya kwa kutokuheshimu vyeti vya TZ.

Manake unailamu Tanzania anasahau,Kenya nao wana mgogoro na Uganda unaofanana na huu.

brazaj endelea kupiga ramli lakini chombo ina yeya,kama vip hamia Kenya manake kitu kidogo "umeona Kenya" ukishindwa jifungie ndani ucheze kidali poo na mkeo pamoja na watoto wako.

Upupu mtupu. Dalili za wazi kuwa elimu ndogo kabisa.

Hakuna hata haja ya kupoteza muda kukujibu wewe.
 
Unajiona una elimu kumbe kilaza,humu JF hatuweki vyeti tungeweka vyeti naamini ungekuwa mdogo.Namiliki vyeti vya ndani mpaka vya nje.

Hufikii kabisa level niliyokuwa nayo kielimu mpuuzi.
 
Kinacho wasumbua jirani zetu ni mikopo waliyochukua kwa ajili ya mapambano ya Covid 19. Masharti ya mikopo hio ni magumu sana ndio maana wanakuwa wakali kwa Tz kwasababu tu ya wivu na si kitu kingine.

Kama hayo ya wivu ni kweli kwa nini tung'ang'anie kuwapimia wageni wao? Hawataki. Sababu za msingi za kutotaka wanazo labda kibongo bongo tuamue kukataa kuwa hawana.

Bado karata ya mwisho si ipo? Kama hawataki tunayoona ni haki yetu kuwapimia wao wageni wao si tufunge tu mpaka yaishe?

Taabu iko wapi?
 
Na sababu za sisi kutaka kupima watu wetu tunazo,
1. Hatuna uhakika na vipimo vyao kwani vimeshaonesha kubambikia watu wetu majibu ya uongo ili kutuchafua.

2. Makubaliano ambayo wao waliyaomba ilikua ni kila mtu apime watu wake, kwann sasa wanakataa sasa hivi wakati kwao wao ndio wana maambukizi makubwa kuliko sisi.

Unaposikia vita ya kiuchumi na kisiasa ndio kenya wanaleta.. wanataka watutangazie ili kuonesha nchi yetu imechafuka kwa corona na kuonekana tz ni wakiukaji wa tahadhari wakati sio kweli.
 
Unajiona una elimu kumbe kilaza,humu JF hatuweki vyeti tungeweka vyeti naamini ungekuwa mdogo.Namiliki vyeti vya ndani mpaka vya nje.

Hufikii kabisa level niliyokuwa nayo kielimu mpuuzi.

Una vyeti fake mkuu? Huoni wenzio wenye vyeti kuwa hawana Corona vinapigwa chini? Wewe unadhani elimu ni makaratasi?

Kama ilivyokuwa kwa Corona ipo tofauti kubwa ya kuwa na cheti na kuwa umeelimika.

Kama hujui vyeti ni makaratasi tu, kuelimika ndiyo ngoma.
 
Back
Top Bottom