- Thread starter
- #141
Haiwezekani kukawepo na mfano wa nchi inayofanya kama sisi, hii ni kuonesha ni jinsi hani kila nchi inafanya mambo yake
Mfano Brazil hawakuweka mazuio kama zingine za Ulaya au Afrika
Narudia kuitaja Sweeden mara ya 3 haikuweka watu wake ndani wao waliamua kutumia Herd immunity kupambana na Covid. Canada pia haikufungia watu ndani na kama sijakosea pia katika nchi za kiskandinavia hazikufungia, ila sio kweli kwamba nchi sote zinaweza kutumia Mode sawa. Ndio maana hata Kenya wao wameweka zuio la watu kutotoka usiku tu na sio Total lockdown kama ya Rwanda na Uganda.
Kwa hivyo basi ni kwambie SIO KWELI KWAMBA TZ NDIYO CHANZO CHA MIGOGORO MIPAKANI, maana katika jibu langu la kwanza nilikujibu bila kutumia maneno hayo ya kukanusha hoja zako.
Nchi jirani zimeamua kutukomoa Tanzania kwa kujikuta wao ni wahukumu wa njia Tanzania inazotumia na kujiona wao wako sahihi kwa kukomoa kuzia madereva wetu wasipite, na ndio maana tulipojibu mapigo ni wao ndio walitetemeka.
Wakenya, wanyarwanda wao wanajiona wako sahihi na nakwambia tena kama hukusoma, Nchi hizi zimechukua mikopo kukabiliana na Covid na masharti yake ni magumu sana ikiwemo kutoa taaribu kila wakati, kitendo cha Tanzania kutochukua mikopo hio na maisha kuendelea kimewakasirisha hawa majirani ndio maana wanatumia hisia kali dhidi yetu.
Ukubali ukatae kuna mengi yapo nyuma ya kinachoendelea mipakani ambacho watu wa pale wanaelewa.
SIYO KWELI TANZANIA NI CHANZO CHA MIGOGORO, ni Nchi hizo jirani kutopendezwa na mbinu Tanzania imetumia kukabiliana na hili janga to which is hakuna madhara makubwa kushinda nchi hizo zilizoamua kuchukua hatua universal bro.
Kenya ni wachokozi, Rwanda ni wachokozi, Zambia ni wachokozi, Uganda ni wachokozi bitia historia utaona.
Mkuu ni wazi kuwa unaongelea mada tofauti au labda huna nia ya kujikita kwenye mada ambayo kwa ujumla iko wazi kabisa.
1. Unaongelea lockdown. Wapi umeona hilo kwenye uzi au mada hii tuliyo nayo mkononi?
Mada ni migogoro mipakani, kwa nini migogoro na nani wa kulaumiwa. Contents ziko kwenye uzi ambapo ningetegemea kanusho, boresho au rekebisho.
2. Unaongelea herd immunity ya Sweden. Hii inahusiana vipi na huu uzi? Huu uzi hauna cha kufanya na kinga yoyote ya mwili popote pale.
Zaidi pia labda niseme, unachosema "herd immunity" kuwa Tanzania imechagua. Hii ndiyo msimamo, tamko na sera rasmi ya serikali kuhusiana na ugonjwa huu?
Hii inastua sana, kwa maana wengine hatukujua hilo kabla ya bandiko lako hili.
Haya mambo ya kuchukua utaratibu kama huu bila kuulizana wala kushauriana mbona ni balaa jingine?
3. Wapi WHO katika nukuu zake zote mbili nilizokupa ambazo hukuzikanusha wala kuzikosoa umeona kuna lockdown au herd immunity?
Si Brazil, Canada, wala Sweden wenye tatizo na protocols hizo za WHO. Wote hawa bila shaka hata wewe unafahamu wazi wazi kwamba wanatambua kuwa wanaziheshimu protocols hizi za WHO kwamba:
A. Ugonjwa huu ni "pandemic which is a public health issue wala si state security issue."
Wanajua kuwa ugonjwa huu ni janga la kimataifa. Kuwa ugonjwa huu ni hatari, unauwa, hauna dawa wala chanjo ya kujikinga nao.
Yote haya ndani ya protocol #1 ya WHO kama nilivyokupa pale.
B. Ugonjwa huu tunaweza kuishi nao ukiwa umedhibitiwa vilivyo ndani ya protocols za WHO.
Hii kama ilivyo katika protocol yao #2 kama nilivyokupa pale.
Hadi sasa huna mmoja anayekiuka protocols za WHO kama nilivyokuomba umweke hapa. Wala anaye fuata misimamo ya Tanzania kuhusiana na protocols hizi kama nilivyokupa pale "in blue:"
Na jingine ni hili hapa:
Mkuu mengine niyaonayo kwenye bandiko lako ni mbwembwe tu nje ya mada ambazo hazitusogezi mbele hata kidogo kuhusiana na mada iliyopo.