#COVID19 Corona Tanzania ni vita kati ya Mungu na wasiomwamini kuwa aweza shinda Corona Mungu atashinda hajawahi shindwa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Corona Tanzania ni vita kati ya Mungu na wasiomwamini kuwa aweza shinda Corona Mungu atashinda hajawahi shindwa

Wasiomwamini wanachekelea wakisikia tetesi kuwa kuna Corona wanahoji Mungu kuwa nyie mliojitia kuomba kiko wapi ? Shetani mleta Corona kamshinda Mungu huyo Mungu wenu bure kabisa.

Hii vita Mungu wa Tanzania ataibuka mshindi tena kwa knock out

Wazungu wajiandae kutushangaa Watanzania kwa ushindi mnono awamu hii tena.

Tanzania kwa sasa ndio taifa teule limeibwaga Maka na Medina na Vatican na Israel kwenye vita dhidi ya Corona kwa kumtumia Mungu yaani using God factor on war against Corona a weapon that other countries have rejected.
 
Ugonjwa analeta shetani? Kumbee watu wanajiandikia kinachokuja kichwani
 
Upo sahihi sana ndugu yangu. Kikubwa ni imani thabiti kwa Mungu wetu huku tukifuata maelekezo yote kutoka kwa wataalamu wetu (wizara ya afya).
Hilo la wataalamu liweke kwanza pembeni hakuna nchi zenye wataalamu kama ulaya na marekani watu kule wanakufa kama kuku na barakoa zao na pamoja na kuzingatia tahadhari zote za mitaani hadi daktari bingwa wa Papá Vatican kafariki kwa Corona na Vatican inaongoza kwa kuzingatia masharti

Huu ni wakati Wa Mungu dio hopeless wataalamu wameshindwa kukabili Corona na Biblia inatamka wazi amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na kumfanya tumaini Lake

Hilo sio kipindi cha kuweka tumaink kwa mwanadamu yeyote hata ajiite mtaalamu vipi
 
Yupo sahihi kwamba ni taifa teule na imeibwaga Israeli siyo!
Upo sahihi sana ndugu yangu. Kikubwa ni imani thabiti kwa Mungu wetu huku tukifuata maelekezo yote kutoka kwa wataalamu wetu (wizara ya afya).
 
Sikujua hivi kumbe kila nchi ina Mungu wake, oukeyyyy.
Ndio aweza hama nchi akaenda nchi inayomtegenea ndio maana alikuwa Mungu wa Ibrahim na Isaka na Yakobo wakati kulikuwa na mamilioni ya watu duniani akiwemo farao lakini hakuitwa Mungu wa Farao

Mungu sio wa kila mtu ni wa wale tu wamtegemeao
Sisi Watanzania ni Mungu weti sababu tunantegemea kwenye vita dhidi ya Corona wakati wengine hawamtegemei
 
Tatizo ni kuwa haya maneno makuu kuhusu Mungu tunayasema kama matokeo ya kujifariji dhidi ya hofu iliyo ndani yetu,hatuyasemi kutokana na imani yetu na vile tunavyomjua Mungu,na tunvyompenda,
Hizi ni zama ambazo jina la Mungu linatumika vibaya sana kwa faida binafsi,
 
Sawa, lakini huyu ni Mungu wa WaTz, si wa Wazungu wala waarabu, ieleweke hivyo
 
Kwa kuthibitisha kwamba MAOMBI ni USELESS, PRAY that COVID-19 ends TOMORROW MORNING all over the world.
 
Ndugu yangu, na wewe upo sahihi. Wakati mwingine Mungu huwaokoa watu wake kwa kupitia watu. Utakumbuka wana wa Israel wakiwa jangwani, katika safari yao ya kwenda Kanaani, walimkosea Mungu, na Mungu aliamua kuwaadhibu kwa kuwashushia nyoka, na kila aliyeumwa na nyoka alikufa (simaanishi Mungu ametuletea Corona). Baada ya maombolezo, Mungu alimwambia Musa atengneze nyoka wa shaba na amtundike juu, na kila atayeumwa na nyoka na aende akamtazame nyoka huyo wa shaba. Tazama, kila aliyeumwa na nyoka na kwenda kumtazama nyoka huyo alipona! Kwa hiyo, nimesema Tuwe na imani thabiti kwa Mungu huku tukifuata maelekezo ya wataalamu nikimaanisha Mungu anaweza kuikomesha directly au kupitia kwa watumishi wake.
 
Kila mtu apambane kivyake kwanza kwenye hili la Corona sisi tumeamua tutumie Mungu
Nataka hapa twende kihalisia zaidi, we kama unaona maombi yanafanya kazi basi leo hii fanya maombi kua kufika hadi kesho asubuhi ulimwengu mzima hautakua na virusi vya corona

Unaweza ukafanya hivyo?
 
Mungu kakupa akili ujikwamue, ingekuwa hivyo basi omba Mungu fumba macho nenda kwenye barabara kuu ujaribu kuvuka uone kama hutogongwa.
Mkuu ingekuwa hivyo Magu aasingekuwa anamaindi madaktari waliokimbia hospital za serikali, angewambia haina haja wagonjwa wataomba tu wapone.
Ila jambo la msingi tuache kulia lia kila mtu ailinde familia yake kwa kadri anavyoona yeye, anayeona corona ipo afuate ushauri wa wataalam anayeona haipo basi aendelee na life kama kawa.
Maana duniani usipojifunza utafunzwa, ila usipojitunza hakuna atakayekutunza.
 
Nataka hapa twende kihalisia zaidi, we kama unaona maombi yanafanya kazi basi leo hii fanya maombi kua kufika hadi kesho asubuhi ulimwengu mzima hautakua na virusi vya corona

Unaweza ukafanya hivyo?
Charity begins at home wengine hawaamini katika maombi watanzania tunaamini
I cant waste my time praying for infidels countries who dont believe that God can remove Cotona in their countries wapambane na hali yao na upagani wao
 
Nataka hapa twende kihalisia zaidi, we kama unaona maombi yanafanya kazi basi leo hii fanya maombi kua kufika hadi kesho asubuhi ulimwengu mzima hautakua na virusi vya corona

Unaweza ukafanya hivyo?
Huko ni kumjaribu Mungu.
 
Mungu hapigani vita, lile atakalo ndio huwa. Mungu huamua yale ayatakayo na ndio huwa, (kama alivyoamua katika nchi yetu kwenye suala la korona), tukisema Mungu alipigana mpambano mkali/mgumu kisha akashinda kwa upande wa Tanzania maana yetu inakuwa ipi ? Kuwa mungu kashindwa kenya, Sudan na mataifa mengine ? Tumshukuru Mungu kwa kutuepusha lakini tusikufuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…