Corona: Tusidanganyane hatuko sawa sote mbele ya ugonjwa huu

Corona: Tusidanganyane hatuko sawa sote mbele ya ugonjwa huu

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana na tuambizane ukweli tu, kwani haisaidii kuukimbia ukweli. Pia msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

Hongera Dar kwa kuanza kutupia barakoa kujaribu kujihami na kuwahami wengine japo kwa jitihada binafsi. Inatia moyo kwani mmedhihirisha "kifaranga hafunzwi kuchakura!"

Ninaamini mngekuwa ninyi msingemkubalia kuvua barakoa yule mkurugenzi wa kule Moshi.

Heko kwa kufanya yaliyopo katika uwezo wenu. Changamoto sasa inabakia kwenye kuepuka misongamano pia kuwapa ulinzi maalum wazee na wote walio kwenye hatari zaidi.

Penye nia pana njia, bila wao japo kwa ugumu tufanyeni yanayowezekana. Walisema waungwana: "yatima hadeki."

Kuna nyomi kwenye ma dala dala, mabasi, mwendokasi, magulioni, masokoni, minadani, migodini, kwenye ma ferry, makanisani, misikitini, mashuleni, nk.

Kifaranga aliyetelekezwa na mamaye anachakura vipi ili kujihami yeye na wapendwa wake wote katika hali hii? Kazi ipo na hii mbombo ni nkafu!

Pana kodi zilizoboreshwa kwa wigo wa ukubwa wa viwango vinavyotulazimisha kuliingia bwawa lililojaa luba bila kujaa hatari yake.

Hatuko sawa mbele ya sheria. Pana wenzetu kodi haziwahusu na hata kula yao haitegemei uhangaikaji wa kila siku, tushukuriwe sisi tuliobebeshwa majukumu ya kuwabeba wao kwa mujibu wa sheria.

Ugonjwa huu si hatari ikiwa huduma za afya hazijazidiwa (overwhelmed). Kama pana wahudumu wa kutosha na vifaa vya kutosha, ugonjwa huu ni kama ka upepo au ka mafua tu kunako pita. Ngoma ni pale changamoto za kupumua zinapokosa msaada wowote au usiotoshelezwa.

Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu!

Kunapokuwa na uhakika kuwa mtu akiugua atapatiwa huduma zote zinazostahili na kwa wakati, mbona wala ugonjwa huu si tatizo?

Maalim Seif, mkewe na wengi wanaaotuhamasisha kuupuuza ugonjwa huu, wanaangukia kwenye kundi hili. Wale wasiokuwamo na ni kwa kutokujitambua tu. Ikumbukwe kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.

Wapo hapa hapa wenye majina yao, nyadhifa zao, nafasi zao, pesa zao nk ambao kwa hakika kwao medical facilities haziwezi kuwa overwhelmed kwao.

Maalim atakosa vipi ventilator? Si ikibidi itang'olewa hata tokea Bugando au huko aliko kwa ajili yake?

Kwamba hatuko sawa mbele ya gonjwa hili ni muhimu tukaufahamu ukweli. Dhana ya mwenye shibe kutomtambua mwenye njaa ni dhahiri.

Tangu lini mabadiliko kwa maslahi ya wengi yakaletwa na walio nacho?

Ninawasilisha.
 
We jamaa inaonekana unapenda sana story za CORONA. Huwa nahisi huangalii BBC wala CNN, ungeona wazungu wanavyodondoshwa na COVID ndo ungeelewa wanaosema bongo hakuna Corona wanaweza kuwa sahihi.

Tanzania haijaathirika hata kwa 2% ukilinganisha na nchi za wazungu. Watu wanaendelea na maisha yao na very soon hizo barakoa hutaziona.
 
We jamaa inaonekana unapenda sana story za CORONA unakaa unawashwa washwa kuhusu CORONA. Huwa nahisi huangalii BBC wala CNN, ungeona wazungu wanavyodondoshwa na COVID ndo ungeelewa wanaosema bongo hakuna Corona wanaweza kuwa sahihi. Tanzania haijaathirika hata kwa %2 ukilinganisha na nchi za wazungu. Watu wanaendelea na maisha yao na very soon hizo barakoa hutaziona.

Takwimu zako za kuwa Tanzania haijaathirika hata kwa %2 kama usemavyo unazipata wapi? CNN au BBC ipi ya hapa yenye hata ruhusa ya kutangaza hali ya hapa?

Hujui kuwa Tanzania corona haipo au kuwa ilikwisha? Au ndiyo kutumiwa kwenyewe na mabeberu? %2 ipi unayoiongelea?

Wewe utakuwa kwenye lile group ambalo kimsingi ugonjwa huu haikuhusu au ni lile la wale kenge wanaowashwa washwa kwenye ule msafara wa mamba?
 
Pole, let them Rest in Peace

watu close na mimi wamekufa this week, Campaign mpya should be JILINDE kwa manufaa ya FAMILIA yako,usingoje Magufuli au Gwajima kasema nini,hawatakuwepo kulea familia yako utakapokufa..................za kuambiwa changanya na zako.
 
Jana katuthibitishia anajua kiingereza sasa atuambie Ben Saanane yupo wapi
 
We jamaa inaonekana unapenda sana story za CORONA unakaa unawashwa washwa kuhusu CORONA. Huwa nahisi huangalii BBC wala CNN, ungeona wazungu wanavyodondoshwa na COVID ndo ungeelewa wanaosema bongo hakuna Corona wanaweza kuwa sahihi. Tanzania haijaathirika hata kwa %2 ukilinganisha na nchi za wazungu. Watu wanaendelea na maisha yao na very soon hizo barakoa hutaziona.
Hata %2 ni nyingi nadhani ni %0.0002 au chini ya hapo, barakoa kwa Dar inatafutwa kwa tochi.
 
Takwimu zako za kuwa Tanzania haijaathirika hata kwa %2 kama usemavyo unazipata wapi?

Hujui kuwa Tanzania corona haipo au kuwa ilikwisha?

Wewe utakuwa kwenye lile group ambalo kimsingi ugonjwa huu haikuhusu au ni ile wale kenge wanaowashwa washwa kwenye ule msafara wa mamba?
Kaa chini jitathmini mkuu una matatizo ya kisaikolojia. Tangu April mwaka jana ulikomaa sana na ishu ya Lockdown. Ni mmojawapo wa watu mliokomalia sana lockdown mkisema wazungu sio wajinga lazima tuwe lockdown kumaliza tatizo, vipi walioweka lockdown waliishia wapi!?

Nimekwambia unawashwa washwa sababu unaletaga threads za CORONA kishambenga shambenga Kama wadada wacheza singeli wa uswahilini.

Threads zako hazieleweki zinalenga nini!? CORONA bongo itapotea naturally kama mwaka jana. Hakuna lockdown, vaccines, vipimo vya kila Kona wala matangazo ya waathirika.

Zamu hii hata shule hazifungwi tunadunda tu. Kama mnaipenda sana CORONA pandeni ndege mkaifate ilipo. Huwa nahisi una matatizo ya akili sio kwa kuiwaza CORONA kiasi hicho.
 
watu close na mimi wamekufa this week, Campaign mpya should be JILINDE kwa manufaa ya FAMILIA yako,usingoje Magufuli au Gwajima kasema nini,hawatakuwepo kulea familia yako utakapokufa..................za kuambiwa changanya na zako.

Changamoto zaidi kwa mayatima sisi ni kwenye kuepuka misongamano isiyoepukika kwenye ma ferry, mwendokasi, magulioni, masokoni, mashuleni nk.

Hasa hasa kwenye mihangaiko ili kumpelekea kaisari ambaye yeye yuko kwenye isolation salama salimini.

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu!
 
Hata %2 ni nyingi nadhani ni %0.0002 au chini ya hapo, barakoa kwa Dar inatafutwa kwa tochi
Huyu jamaa namkumbuka sana alipigia sana kelele lockdown. Ni mojawapo ya watu waliomnanga sana JPM wakimlaumu kutoweka lockdown, Ila mpaka Sasa halioni aibu lilivyoumbuka kila siku lipo humu kukomalia ishu ya CORONA.

Nahisi ana matatizo ya akili, anaumia sana kuona jinsi Tanzania inavyotatua ishu ya CORONA kwa style ya kivyake. Uzuri ni kwamba kiuhalisia hakuna anayesikiliza kelele zao.

Watu wanajifukiza kimya kimya wenyewe wamekomaa na story za ventilators na vaccines. Ni watu wa kuwaacha tu wajione wajinga. Ila kabla ya May watakuwa wameshamwelewa JPM Kama last year.
 
Huyu jamaa namkumbuka sana alipigia sana kelele lockdown. Ni mojawapo ya watu waliomnanga sana JPM wakimlaumu kutoweka lockdown, Ila mpaka Sasa halioni aibu lilivyoumbuka kila siku lipo humu kukomalia ishu ya CORONA. Nahisi ana matatizo ya akili, anaumia sana kuona jinsi Tanzania inavyotatua ishu ya CORONA kwa style ya kivyake. Uzuri ni kwamba kiuhalisia hakuna anayesikiliza kelele zao. Watu wanajifukiza kimya kimya wenyewe wamekomaa na story za ventilators na vaccines. Ni watu wa kuwaacha tu wajione wajinga. Ila kabla ya May watakuwa wameshamwelewa JPM Kama last year.
Kwa hio kama alikosea mara ya kwanza kuhusu lockdown ndio anyamaze hata this time? Watu wanakufa sana na corona,na kama duniani kote wanahangaika na corona nyie ni nani msio na maambukizi?? au mnaishi kisiwa cha peke yenu?
 
Kaa chini jitathmini mkuu una matatizo ya kisaikolojia. Tangu April mwaka jana ulikomaa sana na ishu ya Lockdown. Ni mmojawapo wa watu mliokomalia sana lockdown mkisema wazungu sio wajinga lazima tuwe lockdown kumaliza tatizo, vipi walioweka lockdown waliishia wapi!??.. nimekwambia unawashwa washwa sababu unaletaga threads za CORONA kishambenga shambenga Kama wadada wacheza singeli wa uswahilini. Threads zako hazieleweki zinalenga nini!?,.. CORONA bongo itapotea naturally kama mwaka jana. Hakuna lockdown, vaccines, vipimo vya kila Kona wala matangazo ya waathirika. Zamu hii hata shule hazifungwi tunadunda tu. Kama mnaipenda sana CORONA pandeni ndege mkaifate ilipo. Huwa nahisi una matatizo ya akili sio kwa kuiwaza CORONA kiasi hicho.
Unawashwa washwa nini usiku wote huu kwenye nyuzi zisizo eleweka?

Wewe ni mnufaika wa zile kodi zetu ambazo nyie hamlipi hata ndururu?

Wakati nyie mkituwekea mazingira magumu tusiweze kuiepuka misongamano hata kama tungetaka, kwamba nyie mko salama huko mliko kwani hamna sababu za kuwajibika?

Nyie ni wale wenye ventilator zenu peke yenu pale karibu na COSTECH? Au nyie ni wale wenye exclusive rights ya ventilators zote bila kujali zilipo nchini? Kwamba popote zilipo kipaumbele mtapewa nyie hata kama tayari zina wagonjwa?

Au wewe ni wale kenge kwenye msafara wa mamba na kuwa sasa upo kwenye kuwashwa washwa kwako kwa kutokujitambua ukijidhania na wewe umo humo kumbe hola?

Bure kabisa!
 
Kwa hio kama alikosea mara ya kwanza kuhusu lockdown ndio anyamaze hata this time? Watu wanakufa sana na corona,na kama duniani kote wanahangaika na corona nyie ni nani msio na maambukizi?? au mnaishi kisiwa cha peke yenu??

Kwani hata tulikosea nini na lockdown. Kwani leo kutumbukizwa hata kwenye level 4 ni kwa ajali?

Bangi tuliyoipanda tutaivuna yote. Mbona hakutabaki hata mbegu shambani?

Sana sana huyo mburula ni katika lile kundi ambalo kwenye mada linatambulika kama kenge kwenye msafara wa mamba.

Kutojitambua tu.
 
Pana kodi zilizoboreshwa kwa wigo wa ukubwa wa viwango vinavyotulazimisha kuliingia bwawa lililojaa luba bila kujaa hatari yake.

Hatuko sawa mbele ya sheria. Pana wenzetu kodi haziwahusu na hata kula yao haitegemei uhangaikaji wa kila siku, tushukuriwe sisi tuliobebeshwa majukumu ya kuwabeba wao kwa mujibu wa sheria.
 
Tangu lini mabadiliko kwa maslahi ya wengi yakaletwa na walio nacho?
 
We jamaa inaonekana unapenda sana story za CORONA unakaa unawashwa washwa kuhusu CORONA. Huwa nahisi huangalii BBC wala CNN, ungeona wazungu wanavyodondoshwa na COVID ndo ungeelewa wanaosema bongo hakuna Corona wanaweza kuwa sahihi. Tanzania haijaathirika hata kwa %2 ukilinganisha na nchi za wazungu. Watu wanaendelea na maisha yao na very soon hizo barakoa hutaziona.
watu close na mimi wamekufa this week, Campaign mpya should be JILINDE kwa manufaa ya FAMILIA yako,usingoje Magufuli au Gwajima kasema nini,hawatakuwepo kulea familia yako utakapokufa za kuambiwa changanya na zako.
 
Watu close na mimi wamekufa this week, Campaign mpya should be JILINDE kwa manufaa ya FAMILIA yako,usingoje Magufuli au Gwajima kasema nini, hawatakuwepo kulea familia yako utakapokufa, za kuambiwa changanya na zako.
Maji tiririka ni anasa kwa wengi hasa vijijini. Mama anaamka saa 10 alfajri kufuata ndoo ya maji na anarudi saa nne asubuhi. Atakuelewa kweli umwambie yanawiwe mikono kwa njia tiririka.
 
Back
Top Bottom