Mabibi na mabwana na tuambizane ukweli tu, kwani haisaidii kuukimbia ukweli. Pia msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.
Hongera Dar kwa kuanza kutupia barakoa kujaribu kujihami na kuwahami wengine japo kwa jitihada binafsi. Inatia moyo kwani mmedhihirisha "kifaranga hafunzwi kuchakura!"
Ninaamini mngekuwa ninyi msingemkubalia kuvua barakoa yule mkurugenzi wa kule Moshi.
Heko kwa kufanya yaliyopo katika uwezo wenu. Changamoto sasa inabakia kwenye kuepuka misongamano pia kuwapa ulinzi maalum wazee na wote walio kwenye hatari zaidi.
Penye nia pana njia, bila wao japo kwa ugumu tufanyeni yanayowezekana. Walisema waungwana: "yatima hadeki."
Kuna nyomi kwenye ma dala dala, mabasi, mwendokasi, magulioni, masokoni, minadani, migodini, kwenye ma ferry, makanisani, misikitini, mashuleni, nk.
Kifaranga aliyetelekezwa na mamaye anachakura vipi ili kujihami yeye na wapendwa wake wote katika hali hii? Kazi ipo na hii mbombo ni nkafu!
Pana kodi zilizoboreshwa kwa wigo wa ukubwa wa viwango vinavyotulazimisha kuliingia bwawa lililojaa luba bila kujaa hatari yake.
Hatuko sawa mbele ya sheria. Pana wenzetu kodi haziwahusu na hata kula yao haitegemei uhangaikaji wa kila siku, tushukuriwe sisi tuliobebeshwa majukumu ya kuwabeba wao kwa mujibu wa sheria.
Ugonjwa huu si hatari ikiwa huduma za afya hazijazidiwa (overwhelmed). Kama pana wahudumu wa kutosha na vifaa vya kutosha, ugonjwa huu ni kama ka upepo au ka mafua tu kunako pita. Ngoma ni pale changamoto za kupumua zinapokosa msaada wowote au usiotoshelezwa.
Na huo ndiyo ulio ukweli mchungu!
Kunapokuwa na uhakika kuwa mtu akiugua atapatiwa huduma zote zinazostahili na kwa wakati, mbona wala ugonjwa huu si tatizo?
Maalim Seif, mkewe na wengi wanaaotuhamasisha kuupuuza ugonjwa huu, wanaangukia kwenye kundi hili. Wale wasiokuwamo na ni kwa kutokujitambua tu. Ikumbukwe kwenye msafara wa mamba na kenge wamo.
Wapo hapa hapa wenye majina yao, nyadhifa zao, nafasi zao, pesa zao nk ambao kwa hakika kwao medical facilities haziwezi kuwa overwhelmed kwao.
Maalim atakosa vipi ventilator? Si ikibidi itang'olewa hata tokea Bugando au huko aliko kwa ajili yake?
Kwamba hatuko sawa mbele ya gonjwa hili ni muhimu tukaufahamu ukweli. Dhana ya mwenye shibe kutomtambua mwenye njaa ni dhahiri.
Tangu lini mabadiliko kwa maslahi ya wengi yakaletwa na walio nacho?
Ninawasilisha.