Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza!

Mmhhh
 
Hii thread inaeneza corona, nashauri ivalishwe mask

Anayetaka kuisoma aoshe mikono kabisa

Acha kukaa kihasara hasara
 
Wakae karantini kwa gharama za nani ?

Acha kukaa kihasara hasara
 
Ulishawahi kujiuliza hao USA walizuia hizo ndege wakati gani?!

Unapiga ban international flights wakati tayari ugonjwa umeshaingia mtaani halafu bado unatarajia hiyo restriction itasaidia?!

Kwa mfano Tanzania kwa hapa ilipofikia... hata wakipiga ban international flights na kufunga mipaka leo hii unaamini itasaidia wakati ugonjwa umeingia hadi Uswahilini ndani ndani huko?!

Kwamba eti sijui kama maambukizi yaliletwa kupitia airport au kwa njia za panya, that explains a big problem we have!

Ina maana hufahamu kwamba hata Patient Zero alipitia KIA, na pale akawa cleared lakini kwa busara zake tu akaamua kujipiga quarantine!!!

Ina maana umeshasahau yule mgonjwa ambae alipitia Uwanja wa Ndege wa Dar lakini akafika hadi Mwanza wakati kumbe tayari ana maambukizi!

The question is: Ni wasafiri wangapi sawa na huyo wa Mwanza ambao wanapitia kwenye viwanja vyetu lakini wanaingia mtaani bila kuwekwa quarantine?!

Jibu analo huyu mama:-

Utaona hiyo ni Tweet ya March 25 na huyo mama akilalamika uzembe wa pale airport!!!

Sasa pamoja na yote mnataka tusiwanyooshee vidole waliotufikisha hapa?!
 
Hayo yameshatokea sio kipindi cha kulaumu yaliyopita. Suala la msingi huu mlipuko wa ndani tunaudhibiti vipi? Na kila mtu aonyeshe uzalendo. Sio kulaumu na kutukana viongozi.
 
Yaani watu wafanye ujinga ambao unagharimu maisha ya watu halafu tuache kusema.

Hata kama mnatetea matumbo yenu this is too much.
 
Hayo yameshatokea sio kipindi cha kulaumu yaliyopita. Suala la msingi huu mlipuko wa ndani tunaudhibiti vipi? Na kila mtu aonyeshe uzalendo. Sio kulaumu na kutukana viongozi.
Kwanini tusilaumu wakati juzi tu hapa kwa mara nyingine Magufuli ameendelea kuaminisha watu kwamba coronavirus haiwezi kuingia nchini endapo watu wataendelea kwenda makanisani na misikitini?

Hivi Pasaka si imefanyika juzi tu hapa na bado JPM akaendelea kuhamasisha watu waendelee kujitokeza kwenye sala?!

Hivi kuna mtu anayeweza kuamini unaweza kufanya social distancing kanisani, tena wakati wa Pasaka ambao hata yule asiye na utamaduni wa kwenda church, hiyo siku anaenda!!!

Kama hiyo ya pasaka haitoshi, akahamasisha Siku 3 za Maombezi!!

Hivi kwa Rais aliyekuwa anahamasisha watu waendelee kujitokeza kwenye nyumba za ibada, hizo Siku 3 za Maombezi alitaka zifanyike vipi kama sio watu kwenda kujazana tena misikitini na makanisani kwa ajili ya hayo maombi?!
 
Wewe una chuki zako binafsi.
 
Tumejenga utamaduni wa hovyo kabisa wa kutotaka kuwa sehemu ya majawabu ya changamoto zetu zinazotusonga.
Kila kitu tunageuza ni siasa. Poor us
 
Ata baada ya mtihani mnafanya masahiisho...Wanaccm tujifunze usikivu,kushaurika,busara nk Mfalma akivuliwa nguo jamii yake ndiyo inayo pata aibu
 
Mkuu ina maana ili ni swala la Kisiasa? Sikujua kabisa...basi kama ni hivyo lazma tuiweke kwenye Ilani kabisa ili Oktoba tuitumie dhidi ya wapinzani uchwara.
 
Huwez
Huwezi sikia Mganda anamlaumu Museven kwa hatua za kuzuia wakazi wa Kampala ndani tangu mapema. Tatizo la waTZ lilianza pale kiongozi wao alipochukulia jambo hili kwa mzaha sana hasa pale aliposema ni kaugonjwa kadogo tusitishane. Huku wapambe wakishangilia bila kujua hili ni janga la kimataifa.

Kwa hatua hii tunamtaka Rais aombe radhi raia kwa upotoshaji na kusababisha wengi kutochukua tahadhari kwa uzito wake jambo linalosababisha janga kuwa kubwa. Na bila hatua mathubuti za yeye kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa mapema tutaisha.
 
Kwamba watanzania ni mamburula kiasi hicho mpaka wapewe amri tu ndio wafanye?
Ndiyo.
Ushahidi: Angalia wito wa watu kutumia barakoa bila shuruti.

Mimi nimekuwa nikivaa barakoa muda mrefu kabla ya tangazo la RC Makonda, nikitoka ndani kila mtu ananishangaa na mwingine anahisi nina mnyanyapaa anapokea pesa yangu kwa kukinga na kitu lakini akija mteja asiekuwa na barakoa anapokea kwa mikono tu.

Watu wengine wote toka nyumbani kwetu nawakumbusha kuvaa barakoa, wakienda sehemu wale wa kike wanaanza kuchekwa na kusimangwa.
 
Wakuu why this panic all of sudden, habari njema survivors ni wengi sana kuliko vifo, we will survive this one.
 
Huyu Paskali leo nimeanza kumwelewa vizuri, siku zote nilikuwa nayathamini sana mawazo yake hapo wengi walikuwa wqnamwita majina mengi MF:- Njaa, Kinyonga, Mnafiki, Tiss nk.

Kiumri ni lazima nimweshimu kwani kanizidi (He is my brother not father)

Ushauri. wangu kwako Paskali, Usipende kutumia elimu na heshima yako uliyonayo kuyumbisha yumbisha watu kisa Title yako ni kubwa humu Jf.
Asubuhi unaandika ukionyesha msimamo huu, jioni unakuja kivingine, kesho unajisahau unarudia ya Jana ilimradi tu utuchanganye kwa faida unazozijua mwenyewe.

Nimeanza kutilia shaka wewe ni mtu wa aina gani, nimewahurumia kina Kabendera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…