Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza!

Kunyoosheana kidole Ni tangu enzi za Adamu na Eva ....

Hata tukisema tusinyooshe ukweli haufichiki kwamba serikali yetu kwa namna moja ama nyingine imetufikisha hapa tulipo kwenye swala Zima la Corona.
Kuna screws hazikukazwa kutokana na kiburi, majivuno na kujiona.


Chukua mfano matamko ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam when cases were few watu wakahimizwa wafanye kazi
Later on, baada ya cases kuongezeka matamko yanaanza kubadilika.
Serikali ilibidi kuonyesha nguvu tangu day one...

Na najua deep down Serikali inajua imetukosea Sana watanzania Tena mno😔
 
Paskali jambo muhimu ni kuleta maelewano kwa manufaa ya wananchi wa taifa letu.
Na mtu wa kuongoza maridhiano ni Mh.Raisi Magufuli afungue ukurasa mpya katika utawala wake.
Tunatarajia Raisi Magufuli being a scientist he will adress Covid-19, basing on scientific evidence, proved facts and not otherwise.
Tunategemea ataogeza nguvu nyingi kwa kufanya Testing,Traising, Treatment na quarantine ikibidi,
ili wananchi wetu waweze kurudi haraka katika kufanya shughuli zao.
 
Ushauri wako Pascal Mayalla ni mzuri mimi sina cha kusaidia ila kupitia "COVID-19 World Update" Coronavirus Update (Live): 2,418,592 Cases and 165,741 Deaths from COVID-19 Virus Pandemic - Worldometer kuna nchi zinafanya vizuri sana katika kutibu watu wao waliokutwa na maambukizi mfano wa hizo nchi ni Austria (71%), German (63%), Iran (69%), Switzerland (64%), Australia (64%), Malaysia (61%), Thailand (72%) na Iceland (73%).

Ushauri wangu tutumie ofisi za Balozi zetu kwenye hizo nchi tujui wametibu watu wao kwa kutumia dawa zipi ili nasisi tutumie dawa hizo kuongeza idadi ya watu wanaopona na hivyo virusi
 
Exactly Sasa hivi tulipofika Ni kufanya mass testing kwa kiasi kikubwa ili walioambukizwa wapate msaada
I still don't know hizo bilioni 6 zimewekwa kwa ajili ya mapambo au
 
Litapita bila madhara makubwa? Hapa tulipofikia unahisi ni padogo? Ukweli serikali kunasehemu iliteleza, kwanini serikali haitaki kufunga mipaka? Kwanini hawataki kufunga nyumba za ibada?
 
Mbona Leo hujaweka ile thread yako ya kumsifia Mzee Magufuli, hebu iweke hapo pia. Tulishauri kuwa ni mapema sana kuanza kumpa mtu sifa, haya sasa! Tujisahihishe, tusijikweze, huu ni ugonjwa
 
Mkuu Paskali ugumu unakuja zile njia ambazo zinaweza kutuvusha tayari wapinzani wa kisiasa kwa chama tawala ndio wameshauri zitumike sasa chama tawala kinaogopa kufata ushauri wa wapinzani wanahisi watawapa hatua kwenye siasa, amini nakwambia hata hizi nyumba za ibada zinazofungwa ni amri ya serikali ila serikali hawaji wazi kwakuwa wataonekana wamefata ushauri wa wapinzani
 
Mkuu Paskali, kunyoosheana vidole ni muhimu sana. Wakati watu wanatoa maoni na ushauri, kulikuwa na tambo nyingi sana kwamba watanzania ni watu makini, wana kiongozi makini, shujaa mwenye maono.

Sasa linapobuma, inabidi tuwekane sawa. Tukumbushane waziwazi tena kwa kunyoosheana vidole. Hii itasaidia siku nyingine viongozi wetu wajifunze kuheshimu ushauri, watambue kwamba wao ni binadamu wa kawaida tuu na sio malaika. Wanahitaji msaada kamavwengine
 
Exactly Sasa hivi tulipofika Ni kufanya mass testing kwa kiasi kikubwa ili walioambukizwa wapate msaada
I still don't know hizo bilioni 6 zimewekwa kwa ajili ya mapambo au
Mass testing ni muhimu,nimesikia huko Italy wanatumia test kits za gharama ndogo na kupata majibu papo hapo,lakini inakupa negative,au positive au kama uliiwahi kuugua kuonyesha kama umejenga kinga yaani antibody.Wameenda mbele na kusema kuna watu walipitiwa na Covid-19 bila wao kuuguwa,bali wamepata antibodies.
 
Pasco! Umenena vyama mkuu!
Nadhani kila Raia wa Tanzania anawajibu wakujilinda bila kungojea serikali itoe matamuko.
Rais alitoa matamko haya akijua nature ya watanzani wanahofu sana. Watanzania hatunabudi kuwa na hofu zaidi ya kujikinga sisi wenyewe.
Duniani ni sehemu ya mateso na dhiki maandiko ya Mungu yanasema hivyo!
tupendane! Tujilinde! Tujikinge! Kulinda kizazi cha Taifa hili
 
Mimi kutoipenda CCM imekuwa nongwa wewe kuichukia Chadema sawa! Tuicheze ngoma mnavyotaka ninyi.
 
Mayalla naomba tupe mrejesho wa Yale mabilioni yaliyochangwa maana huku uswahilini hatujaona unyunyuziaji sawa wa maana zaidi ya watembea kwa mguu na vitangi vya mgongoni ambavyo hata sisi tunavyo! Tulitegemea serikali ingeweka matangi makubwa ya maji kwenye masoko, vituo vikubwa vya daladala na inao uwezo wa kugawa balakoa bure kama inavyoweza kugawa bure vibendera vya mkononi kwenye mikutano.
 
Asante sana Paschal, kwa ushauri ulioshiba taarifa sahihi. Ni bahati nzuri sasa hivi kila familia imeshaelewa ubaya na madhara ya janga hili. Japo watu wanamchukia Makonda, pamoja na ushauri wake, lakini juzi katoa ushauri mzuri sana, najua wengi hawakumfuatilia kwa sababu ya chuki. Alishauri wananchi wa Dar, kila familia ifanye kikao cha dharura nyumbani kwa ajili ya ajenda moja tu(EXTRA ORDINARY FAMILY MEETING).Ili kuja na mkakati mahsusi wa kifamilia juu ya nani atoke kwenda kusaka tonge na wengine wabaki nyumbani, na kama anatoka anaepukaje mikusanyiko wakati akisaka mkate na jioni akirudi ajitathmini kama alijichanganya au la. Kama huu ushauri pekee ukifanyiwa kazi naamini vita tutashinda na lawama hazitakuwepo.
La mwisho ni kwa wataalamu wetu wa AFYA, kwa sasa dunia nzima inagombania fursa ya kuja na dawa ya tiba kwa ugonjwa wa Corona, je wataalamu wetu tayari wamezama maabara kusaka dawa???.Hii ni fursa pekee ambayo nchi kama Tanzania tunao uwezo wa kuja na tiba, japo najua WHO wataweka Mizengwe lakini bado tuta fight kama kweli tumegundua na inaponya.Tayari vaccine imepata upinzani, kwa hiyo ndani ya kipindi cha miezi 18 (projected by WHO) ya kupata dawa, kama maprofessor wetu watatulia hii ni fursa ya kupiga pesa.
Asante PM kwa mada
 
Hongera Mayala. Kwa mara ya kwanza nakuona unatoa ushauri uliokwenda shule kwa serikali yetu. Nimekusikia kwa zaidi ya miaka25 lakini miaka yote nilikuona zuzu, sikuwahi kufurahia vipindi vyako wala mada zako. Lakini juzi Star tv nilifurahia ulivyotoa ushauri. Nitaanza sasa kukufuatilia, naweza pata kitu
 
"...Huu sio wakati wa kulaumiana na kunyoosheane vidole vya we didn't do this and that,..."
Nimeipenda hii kauli, umeandika kwa ustadi wako kukwepa kitu. Ni kweli yaliyopita si tija tena, na wala hakuna maana sana kunyoosheana vidole vya "we didn't do this and that", lakini kuna maana kubwa kuendelea kunyoosheana vidole kwa hili la umakusudi kabisa wa kuendelea 'kukaidi' kutochukua hatua kwa sasa! "Anyway" nisitoke nje ya mada, niulize tu Mayalla pamoja na kukubuhu kwako kutumia mitandao ya kijamii na "forums" nyingine za habari, una maanisha hujakutana na habari za kushauri? Kweli ndicho unacho maanisha ama umeandika ili 'tuonekane nasi tunajua kupuliza'? Kumbuka wapo wanaolaumu kwa kuwa washaona ushauri mara kadhaa, wamepigwa na mshangao kwa ukubwa wa 'ukaidi', sasa hawaoni nini zaidi cha kushauri.
 
Mkuu walio wengi wanaipenda nchi yao
Kwa nini tupo tulipo?!
Utawala ndio uliogeuza mioyo ya watu WaTz kupendana kujaliana kusaidiana
Leo watu wanafurahia magumu na mateso ya wengine
Angalia namna watu wamepokea kifo cha mbunge??! Unaambiwa kuna mwingine yupo mahututi watu wanashangilia (its sad but.. ....) ccm tuliwaambia Tz ni yetu sote wakashupaza shingo
Mkuu wa nchi ajirudi athamini kila Mtz wa rangi tofauti imani tofauti vyama tofauti
Aliowateua wamekuwa wanyama wamekuwa na kauli mbovu

Hii statement ielekezwe kwa watawala RPC RC Wabunge wa ccm Mawaziri nk sio wananchi wa kawaida mnawaonea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…