Corona: Tusinyoosheane vidole. Kama unaweza kusaidia, please do. Usisubiri uombwe - jitokeze saidia, vinginevyo nyamaza!

Uzembe wa serikali ya awamu ya Tano, lazima usemwe....uzalendo ni kuwa mkweli sio unafiki..

Korona serikali ilipata nafasi ya kuizuia isienee kwa kasi hii...ikazembee

Wacha watu watapike nyongo...tufe kwa Korona lkn ukweli usemwe na hatua za kujihami na kuenea kwa ugonjwa zichukuliwe...


Pitia Kauli za Makonda toka ugonjwa unaingia Nchini na muendelezo wake..

Tuko ktk mahangaiko haya, sababu ya uzembe wa Viongozi wa Serikali na Chama kama Ndg Polepole... Kuifananisha korona na Upinzani.. Ni stupidity


Uzalendo ni Ukweli.. Korona inaua na inazidi kuenea nchini....sababu ya kushindwa mapema kuchukua hatua.[emoji27][emoji27][emoji46][emoji46]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madaktari wameshindwa.
Na dawa pia zimeshindwa.
tumtegemee nani?

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Kwa hiyo kumbe shida yako ni upinzani?

Hili suala litapita bila hayo unayoyafikiria kutokea. Na mniandae kwa aibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ishu siyo upinzani, ishu ni seriousness na ugonjwa huu. Definetely utaisha lkn utaisha kwa vipi ndilo swali kubwa. Ukifyeka 40m rudi hapa useme umeisha! Nenda kambusu mwenye corona si kagonjwa kadogo! Nasikia mbunge mmoja kanasa kwenye ventillator, anapigana na uhai maana ameshavuka redline sasa anapiga dakika za mwisho! He might recover anyaway!
 
Ahsante sana Sambai!
 

..kwa hiyo mnataka MARIDHIANO?

..umeona jinsi Mbowe alivyokuwa na busara?

..kipindi kile CCM mlitukana kila aina ya matusi.

..hakika mngechukua ushauri wa Freeman Mbowe janga la covid19 lingetukuta tukiwa wamoja.

Cc Pascal Mayalla
 
Kwani makanisa yakifungwa unapata hasara gani?
P tunashukuru kwa mawazo yako lkn " Nyamaza" unavunja haki yetu ya kikatiba ambayo tunaitekeleza kwa kuzingatia kutovunja haki ya mwingine.

Neno " serikali ilaumiwe 100%" na nyingine si kuvunja haki na Uhuru wa mtu.

Hakuna kipindi ambacho tumeungana kama wtz kama kipindi hiki na wale wasiokuwa na mawazo ya msingi walinyamaza lkn kama wapo wanaotoa maoni yao na kuvunja haki ya kikatiba ya mwingine hakika tuwakemee na si uungwana. Hivyo waache.

Serikali na Rais kama baba analilowa na umma wote katika mawazo na nia mbali mbali hivyo si za kupuuzwa ama na rais au serikali yake.
Tulitegemea serikali ifanye kinachotakwa na umma na hapo ndipo tutaona Nguvu ya umma ipo na inaheshimika isippkuwa kwenye mikutano ya serikali na nyakati za uchaguzi. Tulitarajia ama wakubali au watoe clarification ya mawazo ya watu ili umma utafakari sawa na Rais na serikali yake.
Tunajua si rahisi kumridhisha kila mmoja lkn ni vema angalau tukafarijiwa na mshika mpini.
Daktari anakumbwa na maswali na maoni mengi toka kwa wauguzi endapo hali ya mgonjwa inapokuwa mashakan na ni kazi ya daktari kuondoa mawazo hasi, clarification ya maoni yao, kutoa tumaini na maamuzi kama yapo .
Je P Rais na serikali si daktari? Je , daktari akilaumiwa kwa kutotoa clarification, options, huduma na ushauri tarajiwa, si kosa analopaswa kulaumiwa endapo afya ya mgonjwa inapoendelea kuzorota?
 
Tunaweza kunyamaza lkn umma ukinyamaza hakika hata serikali haitatulia.
Huenda P unajua hali ilivyo jikoni lkn kama msambazaji chakula ni vema ukaanza kugawa appetitive soup ili tuendelee kusubiri chakula au ni namna ya kufunga mgawahawa ili chakula kisigawiwe?

Yote ya yote ahsante kwa ushauri.

Tutaonana toharani kama si jehanamu.
 
Mzee kuna kitu kinaitwa decisive response ama active response kutoka kwa yule mwenye instrument of powers! Hata kama leo umeamua kutetea serikalii kwenye hili hapana, nilitegemea reaction ya daraja la kiyegeya! Niko very disappointed nasubiria tangazo la maombi mapya! watu warudi nyumba za ibada wakeshe then number iendelee ku-skyrocket!

Wapotoshaji hawa hapa 👇 tayari wanauza sura! Wanasema wanataka kufanya maombi Jumapili "Operation kuifuta Corona" tena anadai kabisa! Anadai ugonjwa wa coronavirus ni mapepo! Tutapukutika aisee! Operation kuifuta Corona! Wangapi tunaenda Jumapili? Yaani hii nchi badala ya madaktari kupewa airtime kutoa somo ni vipi tuuepuke! Wanapewa hawa jamaa wengine wanadai wanaponyesha!

 
Ni muhimu kuwaonesha walipokosea na sasa taifa linakwenda kuingia gharama kubwa ya uhai wa watu. They should learn to take responsibility kwenye maamuzi yao. Huwezi kucheza betting na maisha ya watu!
 
Nimekuona kule mlima wa moto kwenye upepo wa kisulisuli muda si mrefu.

Any way umeeleweka mkuu!
BTW , hivi ni covid-19 case? Au shida nyingine? Maana waziri anasema leo wameondoka 3 bila kutaja umri wala jinsia. Anyway, RIP Mch.G. Rwakatare
 
Mkuu agiza kinywaji nakuja kulipa...extra mind
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Narudia kukwambia tena mkuu paskal, Mungu Adhihakiwi apandacho mtu ndicho avunacho, tawala yenu ya kisukuma imekuwa chukizo kwa Mungu, mapigo ya adhabu yameanza na mnaenda kudondoka
 
Kaka umeandika vizuri mno lakini kwenye hitimisho mie naona kama umeleta Siasa vile Mkuu wangu.Ebu soma Hitimisho kwa ulichokiandika,yaani yooote unayoomba watu wafanye yameshafanyika saana. For reference sikiliza hutuba za wabunge of likes Mbowe,Lema na wengine wataalam wa Afya haya yote unayooomba wamefanya. Ningeshauri Hitimisho lako liwe kuwaomba wenye mamlaka waache kiburi na wafuate ushauri wa wadau ambao ulitolewa tokea day one hata kabla ugonjwa haujanzaa kusambaa nchini, wenye mamlaka walipuuza kwa kauli za kejeli wapo waliosema eti "huu ugonjwa ni wa baadhi ya watu tu sisi tuna Mungu wetu atatulinda" tena madhabahuni na kwamba tuchape kazi tu. Wapo waliwatisha watu watakao kaa majumbani kujikinga na ugonjwa huu na kwamba watakufa maskini. Sasa kaka sijui unataka WaTZ wafanye nini. Hivi nani asiyejua kuwa wiki moja iliyopita kulikuwa na maadhimisho ya sherehe za PASAKA na yalikuwa na mikusanyiko ya kufa mtu na kwamba wenye mamlaka walitakiwa wasikumbwe na kupelekeshwa na upepo wa kisulisuli kutoka kwa viongozi wa dini? hatukuwa na usalama wa TAIFA, Je haukuliona hili? au kama uliliona je ulishauri nini? je ushauri wao ulifuatwa au ulitupwa kapuni? kama ulitupwa kapuni wanafanya nini ofifini hadi leo?.Kaka rekebisha hitimisho lako....
 
Pasco tangu mwezi wa pili tumepiga kelele sana kuhusu kuchukua tahadhari kwa sababu tunajua nchi maskini hazina uwezo wa kupambana na hili dude kwa hiyo muhimu ilikuwa kuchukua tahadhari lakini wapi sikio la kufa uliwasikia wakuu wenye mamlaka waliojawa kiburi walivyopuuza yote hayo na kuendelea na yao sasa ni wiki ya tatu rais ameikimbia Ikulu anaongea kwa kiburi toka kijijini kwao akiwaamuru watu kuchapa kazi. Wana kiburi mno na ni wakaidi hakuna ushauri watakaosikia tena isipokuwa kama wataathirika wao binafsi labda that will sink in their heart and mind

 
Mkuu Pascal , sikuelewi kabisa katika mabandiko yako mawili uliyonifanyia 'quote'' na ku 'implicate'' kana kwamba sijawahi kuandika kwa kina kuhusu Corona.

Kwa taarifa yako wakati watu wanakumbatia kusifia na uzalendo,nilisimama na kuukataa Uzalendo wa bandia.
Nilisimama na kusema tusifanye mzaha na Corona.

Soma:
Bandiko 161 Ninaukataa Uzalendo wa kutetea uzembe! Ninasimama na Sayansi

Wananchi wazalendo wamcharukia January Makamba kuuliza swali hili Waziri kuhusu Corona - JamiiForums

Wakati watu wakibeza ni mafua tu ya Wazungu nilitahadharisha kwa kueleza haya
Bandiko#18

WITO WA MWANAKIJIJI: Rais Magufuli Atumie Sheria ya Hali ya Dharura (1986) Kukabili COVID-19 (Corona Virus) - JamiiForums

Wakati akina Pascala Mayalla na MsemajiUkweli wakiukana ukweli (denial state) niliandika haya
Bandiko#114 Ninamshauri Pasco aombe radhi kwani maambukizi yatakuwa exponential
Makonda awataka wananchi kutulia na kutotangaza Mgonjwa wa Corona kwani hawana mamlaka - JamiiForums

Wakati Pascal akifanyia indhara kauli yangu ya ''mwezi May' amesahau huko nyuma niliandika haya
Bandiko#60 Ninaelezea Incubation period na jinsi gani tutaathirika
Makonda awataka wananchi kutulia na kutotangaza Mgonjwa wa Corona kwani hawana mamlaka - JamiiForums

Kabla ya Waziri mkuu hajatoa tamko la nani afanye nini, tulishauri hivi
Bandiko#4
IGP Sirro: Hatujafikia hatua ya kufunga mipaka ya nchi kutokana na ugonjwa wa Corona - JamiiForums

Na nyongeza hii

Bandiko#115
Corona: Meneja wa Diamond na Mwana FA watangaza kuugua Corona baada ya kupimwa - JamiiForums

Ninaeleza umuhimu wa serikali kuwa wazi
Star TV: Msemaji Mkuu wa Serekali, Dr. Hassan Abbas, azungumzia wajibu wa vyombo vya habari kuripoti janga la Corona - JamiiForums


Pasco mchango wetu si wa pesa ni mawazo, kwa bahati mbaya nani anawasikiliza kapuku wa JF?
Badala ya kutuhuma wanaoeleza ukweli ungetueleza yule aliyesema tuchape kazi ndio mchango unaoutaka?

Tulitoa hadi ushauri wa nini kifanyike katika bandiko moja kitaalamu na kwa weledi

Tumetimiza wajibu wetu wa Uzalendo wa dhati si ule wa kukosa majibu au kuchora picha.
 
Mkuu, mchawi tayari anajulikana. Kosa letu ni tamaa...... We chose WEALTH instead of HEALTH.
 
Ni wewe PM uliyeandika kuwa Meko ni shujaa? Leo mapum.. yamesinyaa unaweka uzi mrefu na links za kitoto?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…