Mabibi na mabwana na hasa mlio waungwana. Ufuatao ni upotoshaji wa wazi. Tuukatae upotoshaji huu tunapoendelea kuchukua tahadhari:
1. Taarifa sahihi kuhusiana na ugonjwa huu zinaleta taharuki.
Ukweli ni kuwa taarifa sahihi zinatuweka katika hali muafaka ya kukabiliana na tatizo lililopo.
2. Taharuki au hofu ndiyo vinavyouwa.
Ukweli ni kwamba watu wanakufa kwa kushindwa kupumua. Ushukuriwe uwepo wa mashine za kupumua wala si nyungu.
3. Chanjo za ugonjwa huu ni mbinu ya mabeberu kupiga matrilioni ya pesa kutoka kwetu.
Ukweli ni kuwa kupitia WHO kuna mpango wa COVAX kwa ajili ya mataifa masikini kufikisha chanjo hadi kwa nchi masikini:
www.gavi.org
4. Chanjo hizi hazijathibitishwa na kuwa eti zipo kwenye majaribio.
Ukweli ni kuwa chanjo hizi zimethibitishwa baada ya kupitia hatua za majaribio na zinatoa matokeo yaliyokusudiwa.
5. Chanjo hizi zinaleta ugonjwa wa Corona.
Ukweli ni kuwa chanjo hizi zinauandaa mwili kupambana na Corona kwa mashambulizi yawezekanayo kuja.
6. Ugonjwa huu ni vita tu vya kiuchumi dhidi ya Tanzania.
Ukweli ni kuwa, hoja hii ni ya kipuuzi kabisa kuliko zote.
Tuuweke wazi upotoshaji wote unaokwenda na ugonjwa huu bila kuangalia makunyanzi ya mtu.
Wapotoshaji wote wakatambue mafumbo ni ya kufumbia wajinga!
Ninawasilisha.

COVAX vaccine roll-out
Deliveries of COVID-19 vaccines funded through the Gavi COVAX AMC to lower-income countries has begun.