Ninaandika haya nikiwa binafsi naugulia moyoni kutokana na tukio lisilo la kiungwana la vyombo vya serikali Mwanza na yatokanayo.
Kutokana na hilo hapo juu inamfanya mtu awaye yote kughairi mambo mengi. Hata hivyo kutokana na thamani ya maisha ya binadamu, nisiache kuandika haya ambayo aghalabu hayako kwenye waraka wenu (umeambatanishwa chini).
Kuna habari KCMC kuna uhaba mkubwa wa oksijeni. Ilisharipotiwa hivyo Buhando pia Shinyanga.
Mengi ya maana yamekuwa yakitolewa ushauri wa maana ambao kwa bahati mbaya yamekuwa yakiangukia kwenye masikio viziwi ya vigogo wa serikalini.
Kwa kweli hawa vigogo sasa wametuchosha:
1. Wao na jamaa zao kwa habari zilizopo wamekwisha pata chanjo ile iliyo bora kabisa (Pfizer) tena kwa gharama zetu
2. Wao walipo sasa wako salama
3. Wao walipo Corona haipo tena wala haiwahusu
4. Kwamba sisi tuko hatarini hiyo haiwahusu tena.
5. Gharama za matibabu tunatwishwa sisi wakati gonjwa ni janga la dunia
6. Wanaendelea kutuongezea kodi na tozo mbalimbali za kulipa katikati ya janga hili wakati wao malipo hayo hayawahusu.
7. Wakati Waziri Mkuu anasema chanjo zipo tukachanjwe, wizara ya afya wanasema chanzo ni hadi Desemba
8. Wakati serikali wanazuia kongamano la Chadema sababu ikiwa kudhibiti maambukizi ya Corona, CCM wao hiyo haiwahusu. Viwanjani mashabiki wamejaa pomoni, mbio za mwenge, Nandi festival nk, hawa mazuio hayo (yana macho) hayawahusu.
Ni wazi kuwa kumbe tuna matatizo zaidi kuliko hata ugonjwa wenyewe.
Mnaposhindwa kama wizara ya afya kutambua ugonjwa huu ni kipaumbele, nani mwingine afanye jukumu hilo?
Uchumi gani mnaoungelea iwapo gonjwa hili tunalisabilia ili litumalize? Lini busara zenu zitajipambanua kama watu wenye dhamana ya kuyalinda maisha yote pasipo uwepo wa madaraja ya wenye umuhimu zaidi kuishi na wasiokuwa muhimu kufa?
Hapa chini ninaorodhesha maeneo yanayowahusu yenye kuhitaji maboresho. Hii ni ikiwa mngali japo na nia ya kuokoa angalau kinachiweza bado kuokotwa:
A. Mikusanyiko yote bila kujali ni ya nini na isimame sasa.
B. Gharama zote za matibabu ya Corona zibebwe na serikali katika utaratibu unaofahamika.
C. Kodi na tozo mbalimbali wanazotozwa wananchi ziangaliwe kuhusiana na hali ilivyo ya ugonjwa huu.
D. Takwimu za ugonjwa kwa mkoa ikiwamo idadi kamili, walioko hospitali, wanaopona, wanaokufa nk zitolewe kila siku.
E. Uvaaji barakoa kwenye mikusanyiko yote iwe ni lazima.
H. Suala la social distancing lihimizwe.
---------
Kuhusiana na chanjo:
I. Uelimishaji uimarishwe katika namna ambayo mawazo potofu yote yenye mwelekeo hasi utokanao na ujinga yatatokomezwa.
II. Chanjo iharakishwe ili watu hasa wanaoitaka, wachanjwe mara moja wakati uhamasishaji ukiendelea.
III. Chanjo iwe kutoka Ulaya na Marekani tu, (#IV ikizingatiwa).
IV. Chanjo isiwe kutoka Urusi au China.
----------