Corona Virus imetengenezwa? Virusi hivyo vilibashiriwa katika Kitabu mwaka 1981

Corona Virus imetengenezwa? Virusi hivyo vilibashiriwa katika Kitabu mwaka 1981

Baada ya kukitafuta saana hatimae kitabu nimekipata baadhi ya maandiko haya hapaView attachment 1412025View attachment 1412026

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia hii
IMG-20200407-WA0000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia isipofikia mwisho sijui mtatueleza nini.
Hawakosi sababu hawa.

Kuna mtu mmoja alianzisha madhehebu ya dini, miaka ya 1840's akawaambia watu mwisho wa dunia unakuja.

Watu wakamuamini, wakauza majumba na mashamba yao, wakawa wanasubiri mwisho wa dunia.

Mwisho wa dunia ulivyokuwa hauji, akatoa sababu.

Akasema Mungu ni mwenye huruma sana amesikia maombi ya watu wengi, akaahirisha mwisho wa dunia iki kuwapa watu nafasi wamrudie!

Hapo kuna watu washauza kila kitu na kutoa sadaka hela zao zote wakiusubiri mwisho wa dunia.

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
Mwisho wa reli ni kitabu cha mwisho kwenye biblia agano jipya, Ufunuo wa Yohana. Kile kitabu kimeandika mavitu vitu mengine yanaeleweka mengine unayapita kama keyboards... na hii Rona pia imeandikwa kimafumbofumbo.

Soma, elewa nyakati na chukua hatua.

Kuna neno lilinipa wakati mgumu sana nikiwa mschana likilenga wanawake... NYAKATI HIZO, OLE WAO WANYONYESHAO.....

Tangu hapo nikaogopa kuzaa nikihofia kukutwa na hii ole, huku angalizo likisema HATUJUI SIKU WALA SAA...
 
Kiranga,

Hhehehehee umenikumbusha wasabato wa masalia waliokesha airport ya Dar wakisubiri kwenda ulaya bila kuwa na nyaraka ya aina yeyote. Sijui yule mchungaji wao yuko wapi na wale waumini waliishia wapi....

Nimejikuta nakumbuka hofu iliyotanda kwenye jamii niliyokuwepo wakati wa kuusubiria mwaka mpya 2000 kutoka 1999.... kuna waliolizwa kipindi kile na watabiri (Y2K)

Miaka ile Kakobe alikuwa anawaambia waumini wake hasa wanawake, kuvaa dhababu ni dhambi, zilete hapa tuziharibu, leta hela zako zote kwa Yesu upate zaidi. Sikuwahi ingia kanisa lake ila nina ndugu yangu mmoja (dada yangu mtoto wa mama mkubwa) alitekwa na imani ya Kakobe) maisha yake yalikuwa ya chini sana ni yule wa atoke akatafute akipata apike ale na mwanae, hata kodi ya chumba ilikuwa tia maji tia maji.

Alikolea imani akipata hela kutoka mihangaiko yake ananunua chakula, anapika kisha anapakua na kupelekea watumishi kanisani ilhali yeye hajala tangu jana yake na hapo nauli ya kwenda kanisani hana wala ya kurudia hana.... May her soul rest in peace.

Imani ina nguvu sana.
 
Kama kweli unacho hicho kitabu, hebu funua ukurasa wa 50 then andika jina lako la ki-JF (Steven_Shemeji) kwa kalamu ya wino tuthibitishe kweli kitabu hicho unacho mkononi na sio picha za ku-download mtandaoni.
 
Back
Top Bottom