Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
Wakuu,
Kwa taarifa nilizo nazo, ni kuwa muda si mrefu Rais Magufuli atalihutubia Taifa.
Kama hii itatokea, itakuwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani kuhutubia Taifa.
Tutarajie nini?
Stay tuned...
=======
LIVE:
VIDEO:
Rais Magufuli anasema;
=> Baada ya kuibuka Ugonjwa wa Corona Serikali iliaanza kujipanga ikiwemo kutoa Elimu na kuwaandaa Wataalam.
=> Nashukuru Wizara na Vyombo vya habari kwa kushiriki kutoa Elimu kuhusu Ugonjwa huu wa Corona
=> Serikali iliandaa Madaktari kukabiliana na Ugonjwa huu
=> Tuliimarisha Sehemu za Viwanja vya ndege na Mipakani na kupeleka Vifaa vya kupima wale wanaoingia na kutoka.
=> Hadi sasa Nchi yetu imethibitika kuwa na Wagonjwa 12 huku wanne wakiwa kutoka nje ya nchi. Wagonjwa wote Wanaendelea Vizuri, Bado hatujapata habari ya kifo nchi kutokana na Ugonjwa huu
=> Hata Mgonjwa wetu wa kwanza leo ameonekana hana Virusi vya Corona na Wale wote walikuwa na maradhi haya, leo imeonekana negative.
=> Kufuatia kuingia kwa ugonjwa huu hapa nchini, Serikali imeendelea kuchukua hatua, mfano kuzuia mbio za Mwenge na bajeti yake kupelekwa Wizara ya afya ikatumike kusaidia kupambana na ugonjwa huu,
=> Tarehe 17 na 18 mwezi Machi kupitia Waziri Mkuu, Serikali ilitoa Maelekezo kuhusu uamuzi wa Serikali kuzifunga shule zote na vyuo vyote kwa mwezi mmoja ikiwemo kusitisha mikusanyiko ya ndani na nje, tumezuia michezo yote na mashindano mbali mbali.
=> Leo hatua nyingine tulizozichukua ni kama ifuatavyo:
=> Tumeunda Kamati ya kukabiliana na Ugonjwa huu na kamati hii itakuwa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu.
=> Wasafiri wote wanaoingia nchini, Watalazimika kuwekwa Sehemu ya kujitenga [Karantini] kwa gharama zao wenyewe kwa siku 14 hata kama ni mwenyeji.
=> Wizara ya afya iboreshe maabara kuu na iboreshe vituo vya kuhudumia Wagonjwa ikiwemo kuongeza Vifaa.
=> Vyombo vya Usalama viimarishe USalama Mipakani kwa kuhakikisha watu hawaingii nchini hovyo hovyo.
=> Tumisitisha vibali vyote vya safari
=> Watu waendelee kufuata Maelekezo ya Wataaramu. nawasihi kuachana tabia ya kushikana mikono na kujishika pua na macho
=> Najua baadhi ya maeneo inawezekana mikusanyiko isiepukike kama sehemu za ibada, hospitali na makambini. Nawasihi watu wachukue tahadhari wanapokuwa maeneo hayo.
=> Nawasihi Watanzania kuacha kutoa utani na Mzaha juu ya ugonjwa huu ili kuzua taharuki na hofu. Watu watakao bainika wachukuliwe hatua.
=> Nawasihi watanzania tuepuke hofu zisizo na msingi. Kama tukifuata Uahsuri wa wataalam tutashinda adui huyu kama tulivyoshinda adui wengine
=> Nawahimiza tuendelee kuchapa kazi kwa bidii
=> Tuendelee kuchapa kazi kwa bidii kuijenga nchi yetu . Wakulima watumie mvua hizi kuchapa kazi ikiwemo Viwandani Wavuvi nk.
=> Napenda kutumia nafasi hii kutoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa kuliko wakati wowote. Hata Vitabu vya dini vinatufundisha kumuomba Mungu nyakati sura 7 mstari wa 14 pale wana wa Israel walipopatwa na Ugonjwa [2 Mambo ya Nyakati 7:14 inasema; Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.]
Quran Tukufu pia kitabu cha Al Baqara sura ya pili Mstari wa 155 [Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri ]
Waumini wote tusali na kuliombea taifa letu ili Corona isituvuruge.
Asanteni.