Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Corona Virus: Rais Magufuli ahutubia Taifa - Machi 22, 2020 - Wagonjwa Tanzania wafikia 12

Meko anahofu ya uchumi jamani tufanyeni kazi tusidolole kiuchumi wakulima limeni getegete!
Ila kuna mahali nina dukuduku hao watakaowekwa karantini wataweka kwa gharama zao kwanini..?
Ni kwamba wanajaribu kupunguza wasafiri kuja huku au..??
Sasa mkuu ulitaka wakija na corona Nani akuweke katini mkui

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni Jambo la kheri kusikia Mgonjwa wa kwanza amepona kabla hata ya kutimiza siku 14 tangu apimwe.. Pascal anaweza kuwa sawa eeeh!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mahali taarifa zinasema wagonjwa hupona kwa siku 14,bali dalil za ugonjwa Kama uko ndani hujionyesha kwenye vipimo in 14 days jitahid Sanaa kuwa mwelewa mkuu, kupona even in single day covid can be killed ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hata leo kahutubia taifa, na Msigwa katoa clip na taarifa ya maandishi! JPM ni mkweli sana wakati akimalizia salamu zake ibaada ya leo kasema ... nitakuwepo hapa na watani zangu wagogo ...nitakuwepo hapa hadi mwisho wa maisha yangu...ina maana yasemwayo ya maisha yaja!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua kuhutubia taifa ,wewe ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Comment yake ya jana aliandika hakuna atakaye ambukizwa leo idadi imeongezeka.
Sio ya Jana tu mkuu Comment yake ya Nusu SAA iliyopita kasema anasimamia kauli yake Mara kumi hakuna mtanzania atakayeambukizwa akiwa Tanzania kwamba ugonjwa huu Ni wa nchi za Baridi sio tropical disease.

Tumuache kwanza mwandishi wetu Mwenye utaalamu wa Mambo ya afya atufafanulie huu ugonjwa wa wazungu usivyoweza kutuzuru watanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
WATU WA KUKAMATA WALIOFANYA MZAHA NA CORONA


1. POLEPOLE HUMPHREY

2. MWANA FA

3. MC PILIPILI.

4. SALLAM (MENEJA WA DIAMOND)
 
Huu ugonjwa pamoja na kuwa unashambulia maeneo mengine kwa muda huo ila unakuwa na kituo chake kikuu cha kazi (Kwa sasa ni Italy). Na ndiyo maana wakati unaua wachina wengi nchi kama Italy wala zilikuwa hazina habari. Hivyo swala la kijinga kusema eti Corona haitishi au eti haishambulii nchi zenye joto liishie huko huko kwa kina Mayalla na Polepolea na Magufuli.

Just imagine inaweza kutoka hapo Italy na kuvamia sehemu ikaweka hapo makao na watu wakapukutika kweli kweli. Mimi huu ugonjwa kwangu ni hatari kuliko kitu chochote na kiukweli nikiona hatari basi hayo mambo ya kuambiana tuchape kazi SITAFANYA! Kinachotokea sasa Italy ni tofauti kabisa na mwezi mmoja uliopita. Kilichokuwa kikitokea China hakikuwepo hata kwa jirani yake Hongkong. Hatutishani ila tunaelezana ukweli. Corona ni hatari tupu. Omba Mungu sana isiweke ikulu nchini mwako, utazika mpaka uishiwe makaburi!

Hivi Corona ikija hapa ikaweka kambi hata huyo Magufuli atatoka ndani? Dunia inapitia wakati mgumu na kila kitu kimesimama ili kupisha janga hili lipite salama.

Italy wiki mbili na nusu zilizopita ilikuwa na mgonjwa mmoja na akapona vilevile. Corona imeondoka China lakini Italy bado haijaamua kuondoka. Kule Iran jana tu wamedondoka watu 200 jamani huu ugonjwa ukikuvamia ni hatari tupu. Halafu hao wanaosema eti waliokufa walikuwa na magonjwa mengine sijui wazee ni upumbavu mtupu kusema hivyo.

Kama siyo Corona wangekuwepo japo wako na hali hizo. Ugonjwa unaoweza kuua watu elfu 1 kwa siku ndani ya nchi moja na haukomi, kesho yake unaua tena idadi hiyo hiyo ni ugonjwa wenye nguvu ya ajabu! Pengine ni ujumbe kuwa dunia ilijisahau kwa muda! Huu ugonjwa ni tishio. Nyie endeleeni kutoa kejeli kwa waliovamiwa na ukaweka ikulu kwao na wakati mkifanya hivyo mjue na wao walikuwa wakisema kuhusu wenzao.

Huu ugonjwa wakati unaivamia China haukuwepo mahali pengine popote pale duniani hadi tukaanza kuwakejeli kuwa ni ugonjwa wao walioupata kwa kula POPO! Corona ni hatari na ni janga kubwa duniani! Mimi binafsi hili ndilo jambo kubwa sana nililoshuhudia katika maisha niliyoishi! Kwangu naona hili siyo jambo la kawaida hata kidogo.
 
Back
Top Bottom