Tulionya na kutaadhirisha humu, lakini wapi! Lilikuwa ni suala muda tu. Nchi nyingine zilikuwa serious na walichukuwa hatua mapema, kwa mfano quarantine camps kwa watu wanaotoka nchi zenye wagonjwa wengi, kuzuia safari za ndege toka mataifa yaliyoathirika zaidi na kufunga mipaka.
Sie tukawa tunaongea nyenye nye badala ya ku take strong measures, ati naibu waziri Atashasta anasema wameongeza upimaji wa watu kwenye airports( upimaji wa temperature! ) wakati wengi tunajua incubation period ya Corona virus inaweza kuwa hata siku 14 ndio mtu aanze kuonyesha symptoms ikiwemo homa.
Haya sasa haya sasa, na tulivyo na health systems dhaifu, mbona tutakoma.
Pendekezo langu, tuwe wazi, data zianikwe daily. Tukificha ficha kama tunavyofanyaga ati kulinda utalii, nawaambieni tuta enjoy sana. Msisitizo, open government! Kama tulikimbia open government initiative kuficha ujinga ujinga na ubadhirifu, sasa hivi kuliko kipindi chochote kile tunapaswa kuwa wazi ili watu wajilinde na wengine watusaidie.