Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

Corona Virus: Tanzania yathibitisha kuwa na mgonjwa wa kwanza, ni raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji

lembu, Kwahiyo wachina mia Wazungu,Wairan,Waarabu,?
Haupo serious..yaani nchi zikubali zipate hasara yote hiyo kwa sababu ya propaganda tu..
Nakushauri kasome tena novel corona virus!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu haupo serious mortality inatofautiana kulingana na eneo!
Kusema wanakufa kwasababu ya uzembe wa kutowahi kutibiwa ni uwongo..maana wastqna toka kuugua na kufa ni wiki mbili..na wengi wanakufa kutokana na organ failure.. Kumbuka huu ugonjwa unaathiri mapafu,INI na figo..pia ukiugua inatakiwa upate Huduma za kueleweka na siyo kubahatisha..kumbuka wanatibu dalili tu.
Kaisome vizuri novel corona virus!
Mortality rate < 6%
Wakiugua 100 wanaokufa ni 3 to 5 tena kwa uzembe wa kutowahi kutibu Neumonia, Haya mafua jamani yamekuzwa mno. Tulikuwa nao muda mrefu huku ila sisi hatukuwa na popular media za kuutangazia ulimwengu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Al assad,
Inaambatana na Neumonia na Neumonia ndiyo inayoua watu. Mimi nilishaugua Neumonia muda wa Zaidi ya wiki mbili naufahamu vizuri unavyobana mbavu na pumzi. Wagonjwa wanapona wenyewe sio wote wanapata Neumonia wakiugua, vinginevyo rate ya kufa isingekuwa 3%.

Hili gonjwa ni la kisiasa Zaidi. Sasa hivi China na Marekani wameanza kuchimbana kisiri siri wakidai Korona imeanzia China lakini ililetwa kwa makusudi. Kwa sababu hii China imepiga marufuku media zote za Marekani na nchi za magharibi ambazo ndizo zinazokuza huu ugonjwa na kuwaogopesha watu.

Wazungu wenyewe na raia wa Marekani wameanza kutofautiana wenyewe kwa wenyewe kwa jinsi serikali inavyoharibu uchumi kwa kulikuza hili dude.

Spanish flu iliua milion of peple lakini iliishia kimya kimyta 2017. Mwaka jana tu flu iliua Wamarekani Zaidi ya laki 6 pamoja na kuwa flu ina vaccine
 
mh! ukipata muda utafuatilia hiki kisa mitandaoni. Alivyohojiwa alikiri kwamba alihisi anaweza kuwa nao kulingana na nyumba aliyofikia huko Ubeligiji mume wa mwenye nyumba alikuwa nao, hivyo aliona asiende kwake ili kuponesha familia yake. Aliona ni bora wafe wengine lakini sio familia yake, ndioo maana alivyohisi dalili akaenda Mount Meru Hospitali.
Angeenda hospital ningemwelewa zaidi
 
Believe me or not nawaambia hakuna mwafrika mweusi atakayekufa kwa Corona zaidi ya kuumwa tu na kupona.

Lakini simaanishi kwamba eti tusiache kubeba tahadhari.

Tuendelee kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za Wizara ya Afya hili litapita tu.

Lakini mark my words kwamba No any African will die due to Corona virus.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Believe me or not nawaambia hakuna mwafrika mweusi atakayekufa kwa Corona zaidi ya kuumwa tu na kupona

Lakini simaanishi kwamba eti tusiache kubeba tahadhari

Tuendelee kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za wizara ya Afya hili litapita tu

Lakini mark my words kwamba No any African will die due to Corona virus



Sent using Jamii Forums mobile app
Umeolewa..? Nataka nikuwowe!
 
Mimi nataka kufahamu yule victim wa Corona hapa bongo hali yake ikoje?

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Believe me or not nawaambia hakuna mwafrika mweusi atakayekufa kwa Corona zaidi ya kuumwa tu na kupona

Lakini simaanishi kwamba eti tusiache kubeba tahadhari

Tuendelee kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za wizara ya Afya hili litapita tu

Lakini mark my words kwamba No any African will die due to Corona virus

Sent using Jamii Forums mobile app
Ata mimi nina imani ya hivi tutaishia kuwa carrier tu, mgonjwa wa kwanza anakwambia siumwi chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania imethibitisha kisa kimoja cha virusi vya corona. Mgonjwa ni mwanamke wa miaka 46 raia wa Tanzania, aliwasili kutoka Ubelgiji kwa ndege ya shirika la ndege la Rwanda Air.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy Mwalimu, Mwanamke huyo alitoka Ubelgiji na alikuwa anaishi kwenye nyumba ambapo kuna mwanaume alipata virusi vya corona, baadae aliamua kurudi nchini na alipopimwa uwanja wa KIA alionekana mzima hana maambukizi kisha akaamua kujitenga na kujiweka karantini yeye mwenyewe na kukaa hotelini.

Baadae mwanamke huyo alianza kujisikia vibaya na kuamua kwenda hospitali ambapo alipopimwa akathibitika kuwa na virusi vya Corona.



View attachment 1389929
TAARIFA KWA UMMA

KUWEPO KWA MGONJWA WA CORONA NCHINI TANZANIA


Ndugu Wananchi, Mnamo tarehe 15 Machi 2020, tulipokea msafiri mtanzania mwanamke mwenye umri miaka 46, ambaye aliwasili na ndege ya Rwandair, akitokea nchini Ubelgiji. Msafiri huyu aliondoka tarehe 3 Machi 2020, ambapo kati ya tarehe 5-13 Machi alitembelea nchi za Sweden na Denmark na kurudi tena Ubelgiji na kurejea nchini tarehe 15 Machi saa 10 jioni. Msafiri huyu alipita uwanja wa KIA akafanyiwa ukaguzi na kuonekana kutokuwa na homa.

Baadae alianza kujisikia vibaya akiwa hotelini na kwenda hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mt. Meru ambapo sampuli ilichukuliwa na kupelekwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii iliyopo Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi. Vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyu ana maambukizi ya ugonjwa wa Corona (COVID-19). Mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu. Ninapenda kutumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa ili usisambae nchini. Aidha Serikali inashirikiana na Shirika Ia Afya Duniani (WHO) na wadau katika kuendelea kutekeleza mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huu.

Aidha, ninapenda kuendelea kuwataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huu kama tunavyowapatia taarifa na elimu mara kwa mara kupitia njia mbali mbali. Aidha, kwa kuzingatia Kanuni ya 46 ya Sheria ya Afya ya Jamii, 2012 (Reg. 46 of the Public Health Regulation (Sanitisation and Hygiene Practices), 2012); ninaelekeza mambo yafuatayo:-

I. Watanzania wasiokuwa na safari za lazima, wanashauriwa kwa sasa kusitisha safari zao kwenye nchi zenye maambukizi

2. Nazitaka Taasisi zote zikiwemo Shule, Hoteli, Maduka ya Biashara, Nyumba za Kulala Wageni (Lodges/Guest Houses), Makanisa, Misikiti, Ofisi za Umma na za Binafsi, Vituo vya kutolea Huduma za Afya, taasisi za fedha, vyombo vya Usafiri, pamoja na maeneo ya mikusanyiko ya watu kama vile masoko, viwanja vya mpira, na vituo vya abiria kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa maji tiririka na sabuni au maji yenye Klorini kwa ajili ya kuhakikisha usafi wa mikono. Aidha kwa kadri itakavyowezekana, maeneo hayo yawekewe vifaa maalum vya kuwekea vitakasa mikono (Sanitizer Dispensers)

3. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini au vitakasa mikono (hand sanitizers) katika mageti ya kuingilia hifadhini au mahotelini kwa ajili ya kusafisha mikono ya watalii na waongoza watalii wote.

4. Kuweka maji yenye dawa ya Klorini katika Vituo vya Mabasi ya abiria na Mwendokasi kwa ajili ya kusafisha mikono ya wasafiri.

5. Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono, kukumbatiana, kugusa pua, mdomo pamoja na macho kadri itakavyowezekana.

6. Hospitali zetu zihakikishe kuwa ndugu/jamaa wanaokwenda kuona wagonjwa waliolazwa idadi yao isizidi wawili kwa kila mmgonjwa

7. Kutoa taarifa kwenye Ofisi za Afya au Vituo vya Kutolea Huduma za Afya endapo watamwona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa COVID- 19

Imetolewa na: Ummy Mwalimu,Mb.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Dar es Salaam.

16/3/2020


PIA SOMA
Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi |Usambaaji, Dalili na Kinga


IMG_1475.JPG




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Believe me or not nawaambia hakuna mwafrika mweusi atakayekufa kwa Corona zaidi ya kuumwa tu na kupona.

Lakini simaanishi kwamba eti tusiache kubeba tahadhari.

Tuendelee kuchukua tahadhari na kufuata kanuni za Wizara ya Afya hili litapita tu.

Lakini mark my words kwamba No any African will die due to Corona virus.

Sent using Jamii Forums mobile app
Check out Botswana & Sudan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom