Nimeona ni Muhimu Kupost Matibabu Kamili ya Awali na Ya Kati, ya Wagonjwa wa Corona
ili ikusaidie ujue pa kuanzia iwapo utakuwa na Dalili za Corona.
Matibabu Ya Awali
1: Jitihada za Safisha Koo na Mapafu:
Fanya Mazoezi ya KuVuta Pumzi ndani Kupitia kwenye Mwanya wa katikati ya ngumi , Vuta PolePole mpaka Mwisho na KuBana Pumzi sekunde chache Halafu -KuKohoa . Zoezi hili Hulazimisha mapafu yako Yafunguke kwa Ulazima. Uwezo wa kupumua hupungua harala ukiwa na Corona au “Changamoto ya Kupumua”. Fanya zoezi hili Mara kama 20 kila saa, ili Uweze kusafisha Mapafu kabla Haujapata Pneumonia.
Zoezi hili Pia husaidia kuwasambararisha wadudu wanaoleta Pneumonia kwenye mapafu yako, Na Kuzibua Matundu ya Hewa yaliyozibwa na Uchafu mkavu wa Corona unaokuwepo ndani ya Mapafu yako. (Glass-like Opacities)
-Pia Fanya Mazoezi ya Cardio: kama KuRuka Kamba, kuTembea , Kimbia kidogo, Ili Kuweka Mapafu yako katika Hali Nzuri na Mwili wako Imara ukiwa mgonjwa.
-Pia Muhimu, Jifukize: Ilinusaidie Mapafu Kufunguka, na Mwili Kupunguza Homa Na Maumivu. (Fever and Inflammatory aches)
-Kunywa Chai ya MOTO ya Tangawizi , PiliPili Manga, na Asali. Unaweza Kuongeza Ndimu, pamoja na Karafuu: Ikiwa ya Moto Husaidia Koo Kutulia, na Pia Kusaidi Kohozi Chafu Kutoka kwenye Mfumo wa Hewa. (Expectorant process)
-Unapojiskia Umechoka sana, inawezekana Oxygen Imepungua mwilini, Nenda Hospitali kama hauna Kipimo cha oxygen Nyumbani ( kuna watu wanacho siku hizi) .Muhimu sana Ukilala lalia Tumbo, ili mapafu yapanuke zaidi kwa Huko Nyuma na uweze Kupumua Vizuri zaidi. Hospitali huwa tunawageuza hivi wagonjwa wa Corona wenye matatizo ya Kupumua na oxygen mwilini huongezeka (Proning)
****ChondeChonde : Tafadhali Usilale Lale Tu siku nzima. Amka Tembea Changamsha mwili. Zungusha damu, Fanya Mazoezi, maana Corona inaua Haraka usipojaribu kuusaidia mwili wako kupigana vita hii. Wiki 3 tu anaondoka Mwilini. Kwa hio kwa wakati huo Haulali kama kawaida, unaWeka Alarm: Kila baada ya Masaa 4-5 Unaamka, Unachangamsha mwili. MCHANA NA USIKU PIA
(Muhimu kulifahamu: Corona hugandisha ChembeChembe za Damu kwenye Miguu na Huhamia kwenye Mapafu na kuziba mishipa ya Damu ya Mapafu. Madhara yake ni Vifo vya Kushindwa Kupumua vinavyotokea kwa Ghafla na haraka sana. Jinsi ya Kuepuka na hili ni Kutembea kila mara, Mazoezi ya Kila mara, ili Kuhakikisha mzunguko wa Damu Kwenye Miguu unaendelea Vizuri. Na Ukiwa Umekaa chini; Kunja kunjua Miguu kila Mara, damu izunguke. Meza Aspirin kama hauna Vidonda vya Tumbo. Inasaidia ChembeChembe za Damu zishishikane na Kuganda.
2: Juice au Vidonge vya Vitamins Supplements Vinavyoongeza Kinga Mwilini
-Kunywa Juice Nyingi za Machungwa, Ubuyu ,na Nyingine unazopenda wewe. Pia Meza Vidonge vya Vitamins C & D na Zinc ili Kuboost Kinga Mwilini kwa Haraka zaidi ukiwa mgonjwa. Ota Jua - upate Vitamin D ya Bure.
-Kunywa Maji ya Kutosha ili kuisaidia Mzunguko mzuri wa damu, Figo kusafisha na kutoa uchafu mwilini, Blood Pressure yako Kubaki sawa,na Pia Mwili wako kupunguza Homa.
3: Dawa:
-Pia Meza Dawa za Kupunguza Homa Na Maumivu. Kama Paracetamol.
-Ukiwa na Dalili za Pumzi Kubana, Homa Kali Unaweza KuMeza Antibiotics za kuzuia Pneumonia ya Bacteria, pale kinga yako ya Mwili Inaposhushwa na Covid19. (Muulize Daktari wako na pia Pharmacy je ni Antibiotic ipi Itakufaa)
-Kama tayari Una Matatizo ya Kupumua na Homa Isiyokatika: Unaweza Kuongeza dawa ya kupunguza Mchafuko wa Mwili ( Inflamation). Dawa hizi huitwa Steroids. Zinasaidia mwili Kupona Kwa Uharaka zaidi. Unaweza Kutumia Dawa za Vidonge vya au Za Kuchoma Kwenye Mshipa, dawa ya Dexamethasone au Prednisolone: isizidi Dose ya siku tano.
(Kama una Diabetes: Kumbuka Dawa hizi za Steroids hupandisha Sukar juu , kwa hio Ukiwa na Diabetes’s Jipime Sukari mara kwa Mara ujue Sukari yako Ipo Kiasi Gani, na Utumie Dawa za Kupunguza Sukari ya Damu kadri ipasavyo)
Narudia Ushauri wa Tiba ya Corona kwa Ufupi:
-Fanya Mazoezi ya Kuvuta na Kubana pumzi. Fanya Mazoezi ya Kuruka Kamba, Kutembea na Kukimbia.
-Ukipumzika muda mrefu Kunja/Kunjua miguu damu izunguke na isigande. Zungusha hapo Unapokanyagia kama unaendesha gari vile; saidia moyo kuzungusha damu, na Kuzuia Usipate Blood
Clots.
-Jifukize Mara Moja Moja Utoe Homa Na Maumivu Mwilini. Nyungu Ni Dawa !
-Ukianza kukosa pumzi Lalia Tumbo upate nfasi zaidi ya Kupumua, nenda hospitali inawezekana ukahitaji Oxygen nyongeza
-DAWA:
-Ongeza Vitamin C (Juice) Vitamin D (ota jua) , Vidonge vya Zinc . Zote kwa pamoja Huboost Kinga Haraka. Chakula Bora chenye madini haya na Vitamin hutosha. Unatumie Supplements kuongeza tu kinga kwa kasi Zaidi
-Kunywa sana Maji ya Kutosha, Mwili Unayahitaji Maji zaidi ukiwa mgonjwa
-Chai Moto Ya Tangawizi/Karafuu/ PiliPili Manga Na Asali. Kuna Dawa za asili za Kikohozi zenye viungo hivi ndani yake, hizo pia zinafaa.
-Paracetamol kupunguza Homa/Maumivu
-Ukianza Kuhemewa na kukosa Pumzi inawezekana Pneumonia imekuanza , Ni Vizuri Kumeza dawa zake: Ukiweza Muone Daktari akupe Antibiotics na Steroids. Lakini kupona kwako Kunategemea zaidi wewe Kufanya Mazoezi ya Kuimarisha Mapafu yako ili upumue vizuri.
-Antibiotic: Uliza Dr Wako au Pharmacy Zipo aina Kibao. Mfano Azythromycin
-Dawa aina ya CorticoSteroids za Kumeza au za Kuchoma: Dexamethasone au Prednisolone. Doze siku 5 mpaka 7. Dawa hii huusadia mwili kupona haraka , tena nzuri kwa magonjwa yanayosumbua Mapafu.
-Dawa za kufanya damu iwe Nyepesi: (hizi dawa ni muhimu ukiwa na Corona na Ni Mgonjwa zaidi). Ukiwa mgonjwa sana na Corona una nafasi kubwa ya ChembeChembe za Damu Kuganda kwenye miguu (DVT) , na mgando huo wa damu Mwishoni kuhamia kifuani. Dalili yake ni Kushindwa kupumua Ghafla. ( Pulmonary Embolism) . Unaweza Kumeza Aspirin ndogo kwa siku, au Vidonge vya Kufanya Damu kuwa Nyepesi, au kuchomwa sindano Pia: Uliza Daktari wako. ( Dawa hizi hutumika muda mfupi tu - Haizidi mwezi)
Tafadhali: Ukiwa na Dalili za Coronavirus; Jikinge na watu hata unaoishi nao. Pia Usilale Lale tu siku nzima.. Fanya Mazoezi madogo Madogo ili KuZungusha Damu na Kupanua na kuSafisha Mapafu. Ukilala sana Unampa mdudu nafasi akushambulie. Changamsha Mwili