#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
denooJ,
Mitaani mwananyamala Kinondoni mwenge sinza ubungo Mazense Magomeni Temeke yote ilala na vitongoji vyake vyote watoto na watu wazima wanajikusanya kucheza pamoja hakuna wa kuwakanya wala kuzuia hilo, na wengi hawanawi mikono wana kuvaa mask
 
Hapo jijini Dsm bado kuna mikusanyiko mikibwa ya watu hususani uswahilini na kkoo huku watoto wadogo wakiendelea kucheza pamoja pasipo kizuizi cha wazazi wao
 
Hawa nao wasitutishe bana kila mara ni taharuki tu yani dunia imekoswa utulivu kwa ajili ya huyu corona.. na iwe itakavyokuwa tu sasa tushachoka na matamko yao kila muda mara hivi mara vile heee..! Itakavyokuwa na iwe hivyo hivyo tusitishane sana.
 
Dr Akili,
Kimsingi wewe hapa unapinga kuvaa barakoa (wakati wowote?); na ndipo unapo potosha watu.

Hata kama ile taarifa ni feki, kuvaa barakoa ni 'logical' kwa kila hali, kinyume kabisa na wewe ulivyoliona..."yaani hata ukitafakari hilo tangazo kimantiki haiwezekani..."

Mantiki ni kwamba ukiwa kwenye mikusanyiko ya watu, hata hizo futi 6 za 'social separation' hazitoshi. Na kama ulivyoandika, virus ni mdogo kuliko matundu ya vitambaa vinavyotumika kutengeneza barakoa, kwa hiyo ni rahisi kubaki hewani, hata kama WHO watakuwa hawajasema kama tangazo linavyoonyesha..., hiyo ni mantiki; kwa sababu hiyo barakoa itazuia kiasi kadhaa cha virus kupita , na kama mtu aliyevaa kajitahidi hata kuongeza kitambaa au kanga juu ya hiyo barakoa, atapata kinga zaidi kwa sababu ya hizo layers zilizoongezeka juu yake. "Airflow dynamics, laminarflow au turbulent' zitasaidia kuzuia viral load itakayoweza kumfikia aliyevaa barakoa, kuliko ambaye ni mtupu.

Kuvaa barakoa hata bila kuwa 'guideline' iliyotolewa rasmi ni sensible kabisa kama sehemu ya kinga kuzuia maenezi ya ugonjwa.
Hizo sehemu zoote ulizoorodhesha, kama ukiwa unaoga, that's simply exaggeration and stretching of imagined scare.
 
Wiki mbili zimepita madaktar wetu kutoka wizara ya afya walitutangazia kuwa haina haja ya kuvaa facemasks kwasbb Coronavirus haienei Kwa njia ya hewa Ila kama ukiona dalili za Corona unaweza kuvaa mask ili kujilinda mwenyewe na wengine.......
Dr MAKONDA nae alituhasa tunawe mikono mara Kwa mara na sabuni inatosha sasa leo tuchukue ushauri wa Nani?
BBC News | Coronavirus: Why some countries wear face masks and others don't - Why some countries wear face masks and others don't.
 
nikiwa natoka kwangu kuelekea kwenye mizunguko yangu huwa navaa mask, cha ajabu wabongo huwa wananiangalia kwa jicho kali wakihisi kama najiendekeza au naringa.

yaani huku uswahili kwetu ukivaa kale kamask wabongo wanakuangalia kwa jicho la husda sana.
Kweli watakuwa wanakuona wivu, by the way naona wewe utakuwa ni the only few Tanzanians , who will survive this pandemic , maana wengi hawafai.
U r better than even Prince Charles, Mike Arteta, Owner of Olympiakos of Grece etc

BBC News | Coronavirus: Why some countries wear face masks and others don't - Why some countries wear face masks and others don't.
 
USISHIKE USO,USISHIKE MACHO,PUA,MDOMO BILA KUNAWA MIKONO KWA MAJI NA SABUNI,KAA MITA MOJA UNAPOONGEA NA MTU.

Leo 09:30am 12/04/2020.

Niwatakie heri na fanaka katika sikukuu ya Pasaka,Mungu wetu ni mwema, aliwaokoa wana wa Israel walipokuwa wanatoka utumwani Misri, aliwaokoa na ugonjwa wa tauni ulioua mamilioni ya Wamisri, akawaokoa na nyoka waliokuwa wanagonga kila mtu walipokuwa Jangwani,

Akawaokoa na mkono wa Pharaoh kwa kulizamisha baharini jeshi lote la pharaoh na leo Mungu wetu umetuokoa na gonjwa hili la corona, Mungu wetu tunakushukuru.

Dunia imebadilika si Marekani taifa kubwa wala si Tanzania Taifa dogo,uhuru haupo tena,hakuna good times tena,hakuna kuangalia mpira tena,hakuna live nude tena uko Marekani,hakuna vigodoro tena,hata mashoga akili imerudi wamefahamu wanaweza kuchomwa ndani ya dakika kama ilivyochomwa Sodoma na Gomola,

Watu wamejifungia ndani hakuna sherehe tena hata wapendwa wetu marehemu wanazikwa na watu wachache,Sasa kila mtu akili imerudi na ufahamu wa Uwepo wa Mungu umekuja kichwani kwa kila mtu,ushukuriwe Mungu uwezaye kubadili tabia zetu ndani ya dakika na tukakiri ukuu wako.

Ni muda sasa kukumbushana ili kumshinda shetani,kama kuna ulazima vaa mask,nawa mikono kila wakati, tumia sanitizer, usishike uso bila sababu za msingi,nawa ndio ushike uso wako,usiingize vidole vyako puani, Stay home if you can, Eat veggies kwa maana mboga za majani and fruits kwa maana ya matunda..

Always Pray,nirudie tena tubu na kusali kila wakati ukishukuru kwa maana Mungu ameshaliondoa janga hili katika uso wa dunia ni muda tu tutafurahi na kumsifu Mungu kwa kuliondoa janga hili la corona katika dunia.

Tukiweza kunawa kwa maji na sabuni kila wakati,hatutafika kwenye kufungiwa ndani,kila changamoto inatufundisha jambo,pengine changamoto zinakuja kutukumbusha kuwa yapo mataifa hayana amani na daima wamejifungia ndani mfano Syria,Kwa changamoto hii tusipoyakumbuka mataifa kama Libya basi hasira ya Mungu itatushukia.

Pengine changamoto ya corona imekuja kutufunza na kutukumbusha mambo tuliyosahau,tulijisahau hata kusahau uwepo wa Mungu,najua sasa watu watafahamu kuwa utajiri si kitu hata ubabe wa Marekani si kitu,Corona sasa inaitikisa Marekani hadi sisi mataifa madogo tunawaonea huruma,unaweza kusema hawajawahi kuonja tabu,au unaweza kusema achana nao hao ni Wamisri katika zama za tauni ambapo Mungu aliwaokoa wana wa Israel,

Sasa tumejua maana na matokeo ya kufungiwa ndani (lockdown). Turejee hapa Tanzania,Mungu ameonekana akitukinga hata sasa na saa hii unaposoma ujumbe huu,Tumsifu na kumuombea sana Rais wetu John Pombe Magufuli,hakika ni mtu wa imani,duniani kote ndiye pekee aliyeruhusu siku za ibada ziendelee na kwa hakika Mungu ametutetea na kutupigania,

Kiuchumi nchi yetu bado inapambana kutoka kwenye nchi masikini kuelekea uchumi wa kati,sasa tunaweza vipi kuzuia watu kuingia na kutoka Dar es Salaam,sembuse Tanzania ambayo sasa ndio Mwenyekiti wa SADC,sisi tumekuwa kimbilio tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere hata sasa,Mungu ameendelea kututunza na kutuepusha na yote mabaya,

Tutakapo funga mipaka ni sawa kukataa uwepo wa Mungu kwa maana tutakuwa bomba la baraka linalokataa kuwapa maji wenye huhitaji,Mungu ataondoa uwepo wake,tutabaki wenyewe kwa maana tumefungia wenzetu wenye shida na pia kufungia uchumi wetu ndani na kuhatarisha ukuaji wa uchumi ws taifa ambao unasababishwa na pato la mtu mmoja mmoja,

Sasa ni nchi gani Afrika ambayo itafunga mipaka au kufungia watu ndani bila kuwaathiri zaidi wenzetu wanaoishi kwa kipato cha kila siku mfano pale Ubungo Terminal na kwingineko kote katika jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima.

Ebu tuchangie mawazo changia mawazo jinsi asilimia 80% ya Wakazi wa Dar watakavyopata riziki zao kwa kila siku,tumeona kufungiwa ndani Marekani lakini ndio kwanza watu elfu mbili wanakufa kwa siku, Tumeona Kenya,Uganda na Afrika kusini,Africa lockdown haijatoa matokeo chanya! Utagundua Lockdown inasaidia zaidi middle class! Corona inatisha inaua lakini njaa inaua zaidi.

Kama tutazuia wananchi kuingia ama kutoka dar halafu control ifanyike sehemu ndogo tu ya jiji la dar es salaam basi kwanza tulete Utaratibu wa maisha ya wenzetu uko walipofungiwa ndani mfano Wuhan na Hubei ambao ni *hand to mouth* ulivyowapangia watakavyopata *daily bread ama milo yao ya kila siku* baada ya hapo tuwakumbuke wenzetu kule Syria halafu tuendelee na kufungiwa ndani lockdown.

Kwa imani hili gonjwa la corona limeshaisha ni sawa na kuzima moto na kubaki Moshi wake nao baada ya muda utaisha, tukikubaliana kwa imani basi hili gonjwa litatoweka kabisa maana litakosa kuwepo katika vinywa vya watu na litakiwa ratuba ya kuendelea kuwepo katika uso wa dunia,kumbuka tauni iliwaua wamisri ikatoweka bila kugusa wana wa Israel, hii ni fact na ukweli ni wewe na imani yako.

Coronavirus haina dawa, Mtu anapona kutokana na uimara wa Kinga yake, Wengi wanao poteza maisha ni kuwa kinga zao zimeshindwa kufight the virus.

Cha muhimu jitahidi kukaa nyumbani, epuka mikusanyiko, osha mikono na sabuni mara kwa mara. Kumbuka, watu wengi wanao pata Coronavirus wanapona. Ni kama less than 3% ndio wanakufa nao kwa sababu ya weakness ya immunity zao.

Naam, tusimuige tembo kwa kila kitu. Wahenga walitwambia. Afrika riziki ya masikini imo miguuni mwake. Ukimwambia asitoke kwenda kuhemea chakula umejiandaa kumlisha? Au unataka afe na njaa?

Kwenye hili Rais wetu wa Jamhuri bado anatuongoza kwenye njia sahihi. Amesema hakuna lockdown kwa sasa. Tumeshaona wenzetu walioamlisha lockdown na wanyonge wao wakitahabika sana.

Wakati ukifika itatulazimu. Kwa sasa hatujafikia pabaya kwa vile zimeonekana, jitihada za umma kujihadhari bila kutaharuki huku ukisikiliza maelekezo ya wataalam.

Kwa pamoja tutaishinda Corona,Mungu wetu yupo ni sisi kumuamini nae atatenda,atatuokoa na gonjwa hili la corona.

Nikutakie Sikukuu njema ya Pasaka.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam,
0755078854
 
Kukaa Mita moja Kati ya mtu na mtu ni kujidanganya jamani sidhani kama inawezekana kwenda Kwenye mikusanyiko ya watu alafu tukae Mita moja
 
Masharti sio magumu ila sio rahisi kutekelezeka iyo mita moja unakwepa korona unapigwa kabangi na scania kikubwa tuchukue tahadhari
 
August,
prevention is better than cure, whether i will survive or not that's God will. it's better to take precaution measures to avoid the infection ruther than doing nothing at all.
 
Inaonekana kuvaa mask ni mtihani mkubwa sana kwa watanzania, napita huko barabarani naona watu wawili au mmoja waliovaa mask, wengine tunajua Corona ipo, ila na sisi tupotupo tu, tunasubiri tusikie leo wameambukizwa wangapi, tushtuke kidogo, tupige kelele zetu, tumuachie Mungu, then maisha yaendelee, hatuchukui tahadhari yoyote.

Sijui tukoje!.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watz wengi ni wambea....
na wambea kuvaa mask/barakoa hawawezi...
mtihani huu...
 
prevention is better than cure, whether i will survive or not that's God will. it's better to take precaution measures to avoid the infection ruther than doing nothing at all.
Ni sawa Lakini si kwa kupiga kelele au kuwaona wengine ni hamnazo au mafala , hili suala linaenda na sustainability
 
Chanzo mwananchi. Waziri wa afya china alionya utoposha unafanywa na mitando.mfano Watu walisema kuimaisha kinga ya mwili ni kula vyakula vitamini C.

Ukweli ni kwamba ili mwili kujenga kinga white blood cell lazima upate vyakula vitamin A( Carroti, viazi vitamu, maini, supu ya samaki, mayai).

Upunguze mawazo au stress, upate usingizi wa kutosha , mazoezi na maji ya kuposha.na kupunguza vyakula viwandani
 
Hakuna rangi tutaacha ona mwaka huu
Chanzo mwananchi. Waziri wa afya china alionya utoposha unafanywa na mitando.mfano Watu walisema kuimaisha kinga ya mwili ni kula vyakula vitamini C. Ukweli ni kwamba ili mwili kujenga kinga white blood cell lazima upate vyakula vitamin A( Carroti, viazi vitamu, maini, supu ya samaki, mayai). Upunguze mawazo au stress, upate usingizi wa kutosha , mazoezi na maji ya kuposha.na kupunguza vyakula viwandani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWAHIYO HIYO NDO NJIA ILIYOTUMIWA NA CHINA??? 😀 MBONA KAMA MNATUCHANGANYA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom