#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

#COVID19 Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga

Status
Not open for further replies.
Ukweli kuwa ukiwa na kinga imara( strong body immunity) of white blood cell. Kama leucocyte baada ya kupatwa janga hii ni lazima upone. Kwasababu kinga hii ya mwili inauwezo kabisa kupambana na kuua virusi vya corona.

Ndio maana wenye kinga imara wanapona haraka. Ili uwe na kinga imara.lazima ule vyakula vitamini A Na madini kama Zinc ,pata vitamin D Pata mwanga jua( sun source of vitamin D) .,Pata maji salama , usingizi wa kutosha
 
Kirusi cha korona kabla yakuanza kuleta maafa kina jificha kwenye matezi mdomoni na kwenye pua na kusababisha mtu kupiga chafya na kukohowa ktk kipindi hicho mtu anapopiga chafya na kukohowa sio rahisi kujitambuwa au kumtambuwa amesha athirika lakini at that time ndio anasambaza ugonjwa kwa kasi pasipo julikana. kwa bahati mbaya sana akisha ingia kwenye matez anakuwa bado ajaingia kwenye dam hivyo ukifanya test ya huyo mtu huwezi kuona kirusi ndani yake ila anasambaza.

Baada ya muda kirusi kupitia njia ya hewa huingia kwenye mapafu nakuanza kushambulia ndio ktk muda huu hali huwa mbaya sana na joto kupanda sana na kama mtu akikosa huduma nzuri huishia kufa.

Watu wengi wenye covi19 hawajijuwi na ndio maana kuna kila dalili watu wengi wataumwa ikiwa hatutofanya test muda huu. ili kukigunduwa kirusi at stage 1 unachukua ute wa kamasi puani na kwenye matezi ndio uweze kukigunduwa kirusi nje ya hapo jamaa humuoni mpaka awe afika stag 4 jambo Tz litatutesa tunatoa report y stage 4 while stage 1 ndio wengi na wanazidi kusambaza hivyo siku za mbeleni hali yaweza kuwa mbaya zaidi.

Kuwa makini na mtu mwenye mafuwa na kikohozi kikavu.
 
Nchi zote ambazo kuna baridi kama US,Canada, kinga(Immunity) hupunga moja ya sababu kukosa vitamin D Mwanga wa jua, ndio maana CHina wanahangaika sana kula vyakula virutubisho. China ni nchi ambayo wanakula kufuata sayansi lishe. Na nchi inayoongoza kwa RECOVERED CORONA CASES DUNIANI
 
Nimeyajibu maswali haya kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID-19) kwenye video hii:
1. Je vitamini husaidia kinga ya mwili dhidi ya Ugonjwa wa Corona?
2. Je kusukutuwa mdomo na maji ya chumvi husaidia kujikinga na Corona?
3. Je virusi vya Corona vinaweza kusambaa kwa mfumo wa mawasiliano wa 5G?
4. Je virusi vya Corona ni silaha iliyotengenezwa na China?
5. Je taarifa potofu kuhusu ugonjwa wa Corona hutoka wapi?

 
Wakuu,

Najua humu kuna ma dokta wabobezi - nimehangaika kutafuta namna hasa kirusi kinavyoingia katika cell mwili na kujijenga hadi mtu anaumwa hadi mauti yanampata...

Ni maelezo ya Kiingeleza - naomba DR. yeyote humu atufafanulie tuelewe vizuri... kwani elimu haina mwisho !! SARS-CoV-2 ndiyo COVID-19.

SARS-CoV-2 shares between 80% and 90% of its genetic material with the virus that caused SARS – hence its name. Both consist of a strip of RNA enclosed in a fatty shell through which protrude many protein spikes.

The spikes lock on to receptors on the surface of cells lining the human lung – the same type of receptor in both cases – allowing the virus to break into the cell. Once inside, it hijacks the cell’s reproductive machinery to produce more copies of itself, before breaking out of the cell again and killing it in the process.
 
Kwa kifupi Covid-19 anashambulia eneo la gas exchange kwenye mapafu na kusababisha inflammation hapa ndiyo mwanzo wa mapafu kukosa hewa na pia kujaa maji hali ijulikanayo kama pneumonia.
 
Pole pole tutafika.....wacha niunganishe unganishe data mdogo mdogo...


The pleura is a thin membrane that lines the surface of your lungs and the inside of your chest wall. When you have a pleural effusion, fluid builds up in the space between the layers of your pleura


Pleura.JPG
 
CORON VIRUS UNACHO TAKIWA KUZINGATIA.jpg


KUZUIA COVID19.jpg



Ukimaliza kusoma share kuokoa maisha ya wengi.

Jina la ugonjwa: COVID-19

Jina la kirusi: SARS-Cov2


Kwa kifupi ugonjwa huu wa Corona ulipewa jina la COVID-19 huku kirusi kinachosababisha ugonjwa huu kikipewa jina la SARS-Cov2. Kwa hiyo tusichanganye tena haya majina mawili.

kwa kiasi kikubwa jamii haijatilia maanani swala la kunawa mikono kwa maji na sabuni mara kwa mara kama watalaamu wanavyotushauri.

Kwa nini sabuni na maji vimekuwa ni ngao muhimu sana kujikinga na ugonjwa wa COVID-19?

Je ni sabuni yoyote tu ama sabuni maalumu?

Je kipi bora zaidi kati ya sabuni na vitakasa mikono katika kuangamiza kirusi cha SARS-Cov2?

Kabla ya kujibu maswali hayo nianze kwa kukielezea kirusi cha SARS-Cov2.

1. Kirusi cha SARS-Cov2 kinaingia mwilini kupitia sehemu tatu.

Machoni, puani na mdomoni.

Kirusi kikiwa bado nje ya mwili wa binadamu inawezekana kukiangamiza(kikiua: kwa lugha rahisi).

Kirusi kikishaingia ndani ya mwili hakuna dawa yoyote ya kukiangamiza ndio maana tunasema hakuna dawa ya kutibu huu ugonjwa.

2. Kirusi kinafikaje machoni, mdomoni na puani?

Kwa kiasi kikubwa kirusi kinafikia maeneo hayo matatu kiurahisi kabisa kwa kusafirishwa na viganja ama mikono yako mwenyewe kikitokea sehemu yoyote kilipoachwa na anayeugua COVID-19!

Kwa nadra kirusi hiki kinaweza kufika machoni, puani na mdomoni endapo mtu mwenye virusi amepiga chafya ama kukohoa mbele yako na kurusha majimaji ambayo yanatua usoni kwako yakiwa na virusi tayari.

Njia nyingine ni through kissing ambayo inazuilika kirahisi.

3. Kirusi kinaweza kukaa sehemu yoyote hata kama imekauka kikisubiri mikono yako iguse tu kinate ili kipate usafiri wa kukipeleka puani, mdomoni ama machoni.

Kirusi kinaweza kuachwa na kukaa kwenye mbao, chuma, plastiki kwa masaa mengi ama hata siku kadhaa kikiwa na uwezo wa kuambukiza.

Na karibu kila kitu tunachoshika ama kutumia ama kimetengenezwa kwa plastic, chuma ama mbao.

4. Kwa lugha rahisi, Ngozi ya binadamu ni sumaku ya kirusi cha SARS-Cov2.

Yaani inauwezo wa kuvuta na kuvinatisha virusi kwenye ngozi yako ukishika tu vilipo.

Hivyo ukigusa tu kitu chochote ambacho kina virusi basi virusi hivyo vyote vinavyutwa na kuganda kwenye mkono wako.

Kumbuka mpaka hapa hujaambukizwa japo virusi vipo mkononi.

Utaambukizwa tu iwapo utanyayua mkono wako kushika macho, pua ama mdomo kwa sababu yoyote ile.

Hatari ni kwamba watu wengi hushika uso wao (Pua, mdomo ama macho) kila baada ya dakika 2,3,4 au 5. Ukishika tu tayari umejiambukiza mwenyewe.

Lakini pia tafiti zimeonesha ni vigumu sana mtu kutoshika uso wake kabisa. Ni kitendo anachofanya kila binadamu tangu utotoni.

Kitendo cha ngozi ya binadamu kuwa kama sumaku kwa kirusi hiki ndio sababu kubwa kabisa ya kwa nini kirusi hiki kinasambaa na kuambukiza kwa kasi ya ajabu kuliko virusi vingine vyote ambavyo vimekuwepo muda wote kama SARS-Cov, MERS nk.

5. Kirusi cha SARS-Cov2 kimeumbwa na mkusanyiko wa vimelea vitatu.

RNA, Protein na Lipids.

Hapa ndipo uchawi wote wa sabuni unapopatikana.

Ili tuelewane:

tukichukulie kirusi sawa na nyumba iliyojengwa kwa matofali.

Kwa ufananisho huo:

Protein ni sawa na matofali.

Lipids ni sawa na jointi zinazounganisha matofali(kifupi ni gundi ya kugandishia matofauli ili yashikane vizuri) na baadae lipids ni kama plasta ya nyumba kwa ukuta mzima.

RNA ni sawa na kitu chochote kinachohifadhiwa ndani ya nyumba. Hiki hatutakijadili hapa.

Kazi kubwa za lipids katika kirusi cha SARS-Cov2 ni tatu.

Moja: kuunganisha vimelea vya protein kujenga ukuta wa kirusi.

Pili: Kuweka ulinzi ili ukuta wa kirusi usiharibiwe. Sawa tu na kazi ya plasta kwenye nyumba.

Tatu: Lipids ndio inafanya mashambulizi ya kukiingiza kirusi ndani ya seli nyeupe mwilini baada ya mtu kuambukizwa na kupelekea mabalaa yote tunayoona.

Kwa hiyo ukiangamiza lipids basi kirusi kitaporomoka mithiri ya nyumba ya udongo inayoporomoka baada ya matofali kulowana na maji.

Tumalizie na sabuni sasa.

6. Sabuni yoyote bila kujali kama ni ya maji, ya mche ama ya kimiminika kizito ina kemikali ziitwazo kitaalamu amphiphiles ambazo huwa zinafyonza ama kuyeyusha lipids yote ndani ya sekunde 20 tu.

Hii ndio teknolojia inayotumika kuondoa uchafu kwenye nguo unapofua ama kwenye mwili unapooga.

Kwa sababu kirusi cha SARS-Cov2 kimejengwa na kupigwa plasta kwa kutumia lipids na sasa tunajua sabuni zote zinauwezo wa kufyonza hizo lipids ndani ya sekunde 20 tu. Hivyo,

Ukinawa maji na sabuni yoyote ndani ya sekunde 20 tu kirusi ambacho kipo mikononi mwako kinasambaratika chote muda huohuo mithiri ya nyumba inayoporomoka na kuanzia hapo ndio mwisho wa kirusi hicho.

Sabuni inayeshusha ama kufyonza lipids zote na kusababisha protein zote na RNA kusambaratika vipande vipande, na kuanzia hapo hicho si kirusi tena. Kwisha habari yake.

Hii ndio sababu ya kwa nini watalaamu wanashauri tupake sabuni na kusugua vizuri povu lake kwa angalau sekunde 20 ili kuruhusu kemikali za amphiphiles kukifikia kirusi na kufanya chemical reaction na kukiharibu kirusi kwa kukisambaratisha kabisa.

Hii ndio sababu tunashauriwa kunawa kwa maji na sabuni mara kwa mara kwa kuwa tunashika vitu vingi mara nyingi vinavyoweza kuwa na SARS-Cov2.

7. Kama hakuna sabuni na maji, inashauriwa kutumia sanitizer(vitakasa mikono).

Lakini sabuni na maji lazima viwe chaguo la kwanza kabisa kwa kuwa ni bora kuliko sanitizer.

Vitakasa mikono vimetengenezwa kwa mchanyiko wa alcohol kama ethano ambayo nayo inauwezo wa kufyonza ama kuyeyusha lipids na kukisambaratisha kirusi endapo itakuwa na alcohol nyingi sana kati ya 60% mpaka 80%

Lakini watalaamu wanasema vitakasa mkono havina uwezo mkubwa na waajabu kama ule wa sabuni na maji ndio maana inashauriwa kwamba vitakasa mikono vitumike tu pale ambapo hakuna uwezano wa kupata maji na sabuni mfano ofisini, ukiwa ndani ya usafiri kama bus, treni, ndege nk. Ambako ni vigumu kuwa unawanawa mara kwa mara.

Kwa hiyo kunawa kwa maji na sabuni mara kwa mara ni silaha namba moja ya kuzuia kupata ugonjwa wa COVID-29.

Vitakasa mikono vipakwe kila mara unaposhika kitu chochote kinachoweza kuwa na virusi lakini tu kama huna sabuni na maji.

Vinginevyo nawa kwa sabuni na maji ndio komesha yake.

Sabuni na maji ni njia rahisi na isiyo ya gharama na wala hakuna haja ya kukimbilia hizo sabuni za gharama wanazopandisha bei baada ya kupata ufahamu huu wa kitaalamu.

Share zaidi kuokoa wengine.
 
Nipo naangalia DSTV Channel 208 SuperSport HD, mchezo wa ngumi kati ya Mohammed Ali na Joe Courtney, hakika hapajatokea bingwa wa masumbwi aina yake.

Ili kujikinga na kuambukizwa au kuambukiza COVID-19, zingatia ushauri wa wataalamu.

1) Pasipo na sababu usijiunge kwenye mikusanyiko ya watu.

2) Ikibidi kushiriki, jikinge kwa kuvaa barakoa (mask) au kukaa umbali ulio salama (mita² 1) na mtu mwingine.

3) Nawa mikono kwa maji ya kutitirika na sabuni (isiwe ya mche) au kitakasa mikono (sanitiser) kabla ya kugusa macho, pua au mdomo wako.

JILINDE NA WALINDE WENZIO.
 
Nadhani Kuna sababu ya MABASI ya abiria kuoshwa na kunyunyiziwa dawa kama ilivyo kwenye viwanja vya ndege.

Ili kupunguza kuonea kwa virusi vya Corona na hiki nikipindi pale gari ikifika kituo kikuu kwa kila mzungunko, tutaweza kusaidia abilia wetu na watanzania kwa kutokuendelea kuambukizwa Corona.

Hii ni baada ya watu kufuata taratibu na ushaur kutoka serikalini na kutoka vituo vya afya namna na jinsi ya kujikinga na corona.

Sababu watu wanajilinda na kujizuia kutokuambukizwa lakini ukirudi kwenye usafiri wetu achana na levo sit bado kuna hilo tatizo ambalo kwangu imekuwa ninapata wakati mgumu kila niingiapo kwenye huu usafiri wetu.

Naombeni mapendekezo je itasaidia?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom