Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

technically, Kweli ujinga ni baba lao "maskini wa kufikiri". Ati unadai Dini isitumike kama kichaka cha kubweteka na kushindwa kujikinga na serikali kushindwa kubeba jukumu lake la kupambana na corona kwa kununua vifaa? Yaani, unasubiri serikali:
1) ikuvalishe barakoa!
2) ikusimamie kunawa mikono au kujipaka kitakasa mikono!
3) ikulazimishe kujifungia ndani!
 
Kama mlianza na kuidharau dawa ni kuwajibika tu sio maombi, kama karantini hotelini, watu wanatoroka karantini, mara karantini jihudumie mwenyewe kutokufunga mipaka ya nchi, anga hadi ndege zipungue ndio hatua ichukuliwe, dawa hapo ni kujihuzuru tu kwa kushindwa kuwakinga raia wako si maombi!
Sasa huyo mwingine kafanya nini ili tumpe yeye atuongoze?
 
Niliwahi kusema jamaa hakupaswa kuwa rais, bali mtendaji kwenye maeneo mengine. Urais ni zaidi ya hayo anayowaaminisha watu. Katika mazingira haya ndio utaweza kujua rais stahiki kwa nafasi ya cheo cha urais.
Ndio kawa rais sasa na cha kufanya huna.
 
Rais amepotoka?
Watasema hajaandika kwa nembo ya nchi. Hapana, nchi ina rais kila sekunde hapa tanzania hakuna raia anaitwa magufuli bali rais. Hivyo, kufanya maamuzi ya umma kwa kigezo cha dini ni upotovu?

Kama ndivyo, mbona hamkuwahi kulalamika marais wanaposema "Mungu ibariki afrika Mungu ibariki Tanzania"

Pia tumeshuhudia rais anakwenda makanisani na misikitini na hata kuandaa futari ikulu( chakula cha kidini) na kutoa statements za kirais na hatukuwahi kupinga?

Ninajua kuwa ni kosa rais kufanya maamuzi kama rais kwa kigezo cha dini. Je hilo ni ombi au sharti linalopaswa kutekelezwa?
 
Mungu Mwenyezi.
Nijaalie afya njema mimi na kizazi changu, ndugu na jamaa zangu, marafiki na maadui zangu.
Nijalie chakula kizuri mimi na kizazi changu, ndugu na jamaa zangu, marafiki na maadui zangu.
Niepushe na corona mimi na kizazi changu, ndugu na jamaa zangu, marafiki na maadui zangu.
Amina.
 
Maswala ya kusali yahamasishwe na viongozi wa dini.

Viongozi wa taifa watupe mipango kazi wanayotumia kuhakikisha tunapambana na Corona.
Hakuna mpango kazi zaidi ya kila mwananchi kudhamiria kulinda uhai wake na wa mwingine, kwa kuzingatia ushauri wa wataalamu.

Kupuuza kuzingatia ushauri wa kitaalamu, imekuwa vigumu kutokomeza virusi vya UKIMWI. Angalau kuna dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI. Lakini kwa COVID-19, ambapo virusi vyake vinasambaa haraka kama moto nyikani, atakayepuuza, au kusubiri Serikali, abebe lawama mwenyewe.
 
Hoja nyepesi muno
Kweli ujinga ni baba lao "maskini wa kufikiri". Ati unadai Dini isitumike kama kichaka cha kubweteka na kushindwa kujikinga na serikali kushindwa kubeba jukumu lake la kupambana na corona kwa kununua vifaa? Yaani, unasubiri serikali:
1) ikuvalishe barakoa!
2) ikusimamie kunawa mikono au kujipaka kitakasa mikono!
3) ikulazimishe kujifungia ndani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingia kwenye katiba juwa majukumu ya rais, sio kutenga siku za maombi!
Katika hili, kuna kifungu cha Katiba kimevunjwa? Inaonyesha pia hata wewe huijui Katiba

Raisi wa nchi, amewaomba Watanzania wote kupitia Imani zao bila kuzibagua Imani hizo zote, na ndiyo maana ametangaza Kwa siku tatu, ambazo katika hizo, ndiyo siku ambapo makundi ya waabudu Mungu hukutana,

Dini hizo zingine za kishetwani hazijulikani ni siku ipi hukutana, maana kazi Yao mara nyingi hufanywa Kwa Siri, agenda zao ni za Siri,

Kuwangia watu mchezo!!!! Inahitaji moyo wa chuma ndiyo ufanye utumwa huo
 
Kwani kasema nchi hii inadini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama commander in Chief anapaswa kutojificha nyuma ya dini anapaswa kutoa maamuzi magumu na kuzuia mikusanyiko hata kwenye nyumba za ibada!

Mimi binafsi nataka kuona concrete measures taken so far! Nataka kuona mass production ya sanitizer booths all across the country! Nataka kuona masks in millions zikigawiwa!
 
Hii ya namba moja kutoa matamko Twitter imekaaje ki- protokali na utekelezaji wa matamko ya namna hii umekaaje? serikali si huwa inaenda kwa barua.

Au ni amesema kama wana twitter wengine ila sio kama president

kwako Pascal Mayalla
 
Kwa udhaifu ulioko leo katika safu ya uongozi wa juu wa Taifa hili tuombe majirani zetu wasituvamie

Hata Zanzibar tu wakiamua watafika hadi Dodoma ndani ya masaa tu

Burundi ndio wala tusiitaje sijawahi kuuona uongozi goigoi kama huu
 
Back
Top Bottom