Kuna siasa hapa inafanyika in the name of prayers.
Ufahamu na maarifa ndio nguvu ya msaada anayoitumia Mungu kufanya kazi zaidi katika majira na kipindi tunachokiishi ili kukabili changamoto zinazotuzunguka.
Himizo hili la kufunga na kuomba likiambatana na maamuzi ya kiimani yanayotokana na maarifa na uzoefu juu ya njia ya kujikinga na janga hili la dunia as medical emergency, hakika litafaa sana:
Haingii akilini Kama tunahitaji msaada wa Mungu hali Yale yaliyo ndani ya uwezo wetu hatutaki kuyafanyia maamzi.
Mbona bado tunaruhusu safari za mikoani?
Mbona bado tunaruhusu Bar, hotel, kumbi za starehe kuendelea na shughuri Kama kawaida?
Mbona hakuna udhibiti katika usafiri wa umma (public transport)?
Mbona hakuna hatua za kuzuia makusanyiko hasa katika maeneo ya biashara hasa masoko, minada na supermarket?
Mbona makusanyiko ya kiibada bado tunaruhusu?
Mbona tumeshindwa kufanya total lock down?
Kama hatua za social distance zinetushinda hakuna namna tunaweza kuhepuka athali za janaga hili.
Tukiruhusu maambukizi yaendelee kwa sehemu kubwa ya population lazima tuwe na uhakika gharama walizolipa mahala pengine duniani vikiwemo vifo vyetu sis, ndg na jamaa zetu lazima vitatokea tu.
Najua tutachagua kuvitangaza au lah ila kikombe hiki tutakinywea.
NOTE:
Moja ya maombi yetu iwe kumuombea Rais wetu na viongozi wa serikali ,Mungu awape ujasiri wa kufanya maamuzi magumu ili kulinda maisha ya watanzania.
Kutoogopa hofu ya lock down hiyo pia ni sehemu ya imani thabiti.
Mungu atupe ujasiri na maarifa.
Sent using
Jamii Forums mobile app