HESABU 21:7-9
Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.
Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.
Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.
MKUU.
Nakwambia sisi wa kulialia.Tutalia na Maombi Mpaka kieleke.
Wenye Imani haba ndio watatikiswa sana,
Lkn Hawa 👇👇Hawatatikiswa kbsa.
Zab 125:1-2
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.