Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Saint Anne, Nimeupenda moyo wako wa utayari kushirikisha unachokiamini.

Naomba kuongezea kwa kile ulichokiandika

Kutambua roho ya mtumishi wa Mungu wa kweli ni simple sana.

Kwanza angalia Kama maisha yake yamejaa Roho mtakatifu au mtakavitu!

Mwenye Roho mtakatifu maisha yake lazima yajae matunda ya Roho- upendo, amani, upole, kiasi, utu wema, bidii, na kujitesa kwa ajili ya wengine.

Ila mwenye roho mtakavitu chunguza mambo haya: ubinafsi, kupenda atumikiwe yeye tu, roho ya matisho, ukorofi, mnafiki (double standard) etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani et maombi!!! Inashangaza sn!

Yani walivyojaa makanisani huko walokole wanakemeana na mate kurushiana! Wait mtaelewa tu.
Et Mungu fukuza pepo corona, fukuza pepooooooo!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
HESABU 21:7-9

Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu.

Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi.

Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.

MKUU.
Nakwambia sisi wa kulialia.Tutalia na Maombi Mpaka kieleke.
Wenye Imani haba ndio watatikiswa sana,
Lkn Hawa 👇👇Hawatatikiswa kbsa.
Zab 125:1-2
Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele.
Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu, Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake, Tangu sasa na hata milele.
 
pureman2,
Mbona kama unataka kuwepo na TOTAL LOCKOUT? Unadhani that will work in our social - economic scenario?

Nashauri tuache parochial approaches zile za ku copy na ku paste, hazitatusaidia sana. Tumuombe Mungu na kufuata scientific directives na USHINDI DHIDI YA CORONA VIRUS UTAPATIKANA. Kama una amini seme AMINA!
Kwa approach hii waliochagua viongozi wetu ni kuamua kututoa sadaka kwa wananchi tuwe attacked na nguvu ya mazingira. Ukiondoka sawa, na ukishinda unabahati. yaani " survival of the fittest".

Hii natural selection, kitu ambacho nakiona kuwa hakiko sawa coz serikali inakua Kama inakwepa jukumu lake la kuwalinda wananchi wake , ambalo ndo jukumu lake la Kwanza la msingi.

Uchumi tunaoogopa kuupoteza una maana gani Kama hautumuki kulinda maisha ya watu ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
pureman2, Asante Sana
Hata maandiko yanasema mtawajua kwa matendo Yao.

Lakini pia hata hayo nilihotaja ndio msingi ulipo.. Roho wa Mungu akikaa ndani yako anakuambia Moja kwa Moja yupi wa kweli na yupi wa uongo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu alimnusuru Lissu dhidi ya umauti uliosababishwa na risasi za kutosha,watu walikatazwa kumuombea apone.

Leo tumwombe Mungu kutuepusha na janga la corona kwasababu linatishia uhai wetu na familia zetu,Kweli!

Mungu hadhihakiwi, tunachokipanda ndicho tutakivuna.
 
Jamaa anatia hasira sana, sijui atamaliza lini, kweli una tweet kuhimiza maombi badala ya hatua za kuchukua au kutoa update ya ugonjwa?

Hata kama kuna hatua zinachukuliwa but this tweet hapana.
 
Ukitka kupata reasoned jibu kwa swali lako, lazima ujibu kwanza swali hili: Je Mungu yupo? Hii ni kwasababu tunaaminishwa tu bila proof kuwa Mungu yupo. Huwezi ku assign duties kwa kitu ambacho hakipi. Tujiridhishe scientifically kama Mungu yupo.
Mafanikio ya MATAGA ni pamoja na kutuletea COVID-19.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii si vita ya kiimani, Laiti kama ingekua hivyo Vatican wangeongoza na pia wangefanya ibada ya pasaka kama miaka mingine. Nishauri tu tusali sana na tufuate taratibu zote za zinazopendekezwa.
 
macho_mdiliko,
Mkuu maisha ya kiafrika sio kama ya watu wa mataifa yaliyopiga hatua kiviwanda.

Sisi tuna uchumi wa wabeba zege, wauza vitumbua, wasukuma maguta, hatuna uchumi wa watu wenye akiba.

Ili ule lazima utoke nje juani ukatoke jasho. Majonda hakukosea kusema watu wafanye kazi.

Alisisitizia juu ya kuchukua tahadhari kila mara, kunawa mikono na tahadhari nyingine.

Tupunguze siasa za malalamiko, hili ni janga la dunia nzima, Makonda angekuwa hajazaliwa bado corona ingekuwepo na madhara yake yangebaki kuwa makubwa.
 
Phillipo Bukililo,
Na mimi wala sikusema watu wakatazwe kutoka. Nimesema misongamano ipunguzwe kadiri iwezekenavyo na viongozi ndiyo wanapaswa kuonyesha mfano.

Makonda kauli zake zilikuwa ni za kubeza ugonjwa na kusisitiza kunawa tu mikono. Na mbaya zaidi alikuwa anakusanya watu kipindi hiki ambacho ni cha hatari.
 
Na mimi wala sikusema watu wakatazwe kutoka. Nimesema misongamano ipunguzwe kadiri iwezekenavyo na viongozi ndiyo wanapaswa kuonyesha mfano. Makonda kauli zake zilikuwa ni za kubeza ugonjwa na kusisitiza kunawa tu mikono. Na mbaya zaidi alikuwa anakusanya watu kipindi hiki ambacho ni cha hatari.
Lawama hazina msaada wowote, tenda lile unaloliona ni la busara kipindi hiki.
 
Lol kwa hiyo watanzania mnamjua Mungu kuliko hata waliowa-introduce kwa huyo Mungu? Tuna safari mrefu sana.

IMG_20200328_163754.jpg
 
Kuomba kwa siku tatu kama alivyo agiza mheshimiwa Rais Magufuli Siyo: kuacha kuzingatia maelekezo yote ya kitaalamu, siyo kukubali kwamba serikali ipo sahihi kwa kila kitu! Siyo kuunga mkono juhudi, siyo kufumbia tatizo macho!

Kukubali kuomba ni kukubali kwamba janga hili ni kubwa, ni kuona jinsi ambavyo, hata nchi zenye maendeleo makubwa ya kitabibu na utaalamu, wamekwama! Ni kuamini kwamba mwenyenzi Mungu anaweza kutusaidia, kutokomeza ugonjwa, kutupa hekima ya kukabiliana na ugonjwa na kutulinda! It is a high time that we work together in unity, because we have a common enemy!

Tunatofautiana itikadi, imani na mambo mengi kimtazamo, lakini tuna adui mmoja anaye tushambulia kwa sasa, tuungane kumkabili! Kila Mtu kwa imani yake, Mh. Godbless Lema ametuwekea mfano.
 
Back
Top Bottom