Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Tunaweza fanya analysis ya matokeo ya maombi ya siku tatu kwenye Corona?
 
tupo kanisani mda huuu ni full maombeziii...alafu baadae kujifukiziaaa..
 
Mungu kanuni zake za utendaji mbele ya mwanadamu ziko wazi.
Yale maombi ya siku tatu yalijaa siasa kabisa.
Viongozi wa dini wakageuka na kuanza kuwasifu miungu wawili.
Viongozi wa dini ambao walikaa kimya kipindi cha utekwaji watu, walikaa kimya kipindi Tundu Lisu anapigwa risasi mchana kweupe mahali ambapo serikali imeweka ulinzi wake.
Watumishi wa umma kutopandishwa mishahara miaka 4-5 mfululizo viongozi wa dini walikaa kimya.
Siku wanatangaziwa maombi ya kuombea taifa wakaanza kumwaga sifa ili kulinda nafasi zao za ulaji.
Watumishi wa Mungu wa kale walikuwa wakweli na hawaogopi kifo wala jela.
Simba wa kutengenezwa alipokuwa anatumwa kumuua mtu kule kwetu Kusini miaka hiyo akija kijijini huanza na watu wengine kwanza na akimfikia mlengwa simba hupotea au huuwawa kiurahisi.
Tubuni maana hamjui siku wala SAA.
Tanzania ibarikiwe, na kila pando ambao Mungu wa mbinguni hajalipanda ling'olewe.
 
Hivi watanzania tulivyotangaziwa kufunga na kuomba siku tatu mfufulizo baada ya kuondolewa kuepushwa tatizo la corona tulifunga na kumshukuru Mungu? nachomekea tu au siyo ndugu zangu!!!
 
Jiwe yupo mbele kwa kila kitu, tulitoa shukrani zetu na tukafanya bonge wa tamasha huko dodomanian
 
Hivi watanzania tulivyotangaziwa kufunga na kuomba siku tatu mfufulizo baada ya kuondolewa kuepushwa tatizo la corona tulifunga na kumshukuru Mungu???????????nachomekea tu au siyo ndugu zangu!!!
kuondolewa, kuepushwa na janga la corona? una maana gani?
 
tuachane na Corona... hapo mbele si ungemalizia na Kiswahili tu mkuu. Kimalkia hakijakupenda.
 
Humu watu sio wajinga! Ni ngumu kujadili uongo wa Corona
 
Wakuu
Naomba kuuliza ninyi mliopita shule ujue nawaza hiyo noma inahitaji zaidi maombi tu au inahitaji tafiti za kisayansi?
Na kipi tuanze kukiamini kati ya maombi au tuamini tafiti zinasemaje?
Je wataalam wa masuala ya afya wanasemaje juu ya hizo mambo kwa hapa nchini?
 
Waliofanya tafiti za kisayansi marekani na ulaya wamefikia wapi?
Wana wagonjwa wangapi? Na waliokufa wangapi.
Na je waliomtegemea maombi ya mungu Wana wagonjwa wangapi na wamekufa wangapi.
Twende na data
 
Mungu anasema mfanye kazi. Maombi au ibada ni mambo tunayotakiwa kuyafanya kila siku katika maisha yetu katika magonjwa au furaha haijalishi na kusoma tuliamrishwa pia na Mungu someni. Science ni muhimu sana tena sana sio katika janga la corona tu kuna magonjwa mengi sana yalikuwa zamani yanauwa watu leo yana dawa zinasaidia. Katika maisha haya haya hatujaambiwa tuchague moja ni lazima tuheshimu science na elimu kwa jumla na ibada tumefanyiwa fardhi( lazima). Ibada ni lazima kwa wote haijalishi ila science sio sote tunaoweza sasa wanaofanya basi lazima tuwaheshimu sana tu hata tukiumwa kichwa tunakimbilia panadol.
 
Tatizo hii ngoma haisikii kitu kinachoitwa sayansi.
Tukimbilie wapi?

Back
Top Bottom