Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Atoke huko mafichoni aje tupambane huku wote, ni kosa kubwa Mkuu wa majeshi kwenda kukaaa Kijijini kipindi cha Vita, ingekuwa ni ulaya wananchi wangekuwa wameandamana vibaya mno ingekuwa ni big story

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maombi yoyote huanza kwa toba na kuomba msamaha,Hili ni kwa dini zote hata kwa wasio na dini

Hamuwezi kwenda mlimani au porini kuomba bila kuomba msamaha mlipokosea kwanza hii ni kwa wale wanaoamini mambo ya utamaduni

Kwa waaminio katika imani za dini huwezi kuanza kuomba bila kujitakasa kwanza madhaifu au uchafu wako
Siku tatu za sala na maombi aliyotoa mkuu wa nchi Rais Magufuli,Wanasiasa hasa wa Chama cha mapinduzi waliamua kufanya maigizo kila kona ya nchi

RPC mmoja wakati wa maombi aliingiza kauli za kusifia mtu kuwa yeye ameweza kuzuia corona ,Kejeli iliyofanyika kwenye siku tatu za maombi ya corona hakika inachekesha na kusikitisha sana

Huko Mbeya,Baadhi ya polisi walionekana wakicheka na kutabasamu wakati mwenzao akiomba ,Nadhani moyoni kilichowafurahisha ni kushangaa mwenzao kushusha maombi kama ana Professional ya uchungaji,Maigizo kama haya hayatufikishi sehemu

Ushauri,Taifa hili limeshagawanyika vipande vipande ndani ya ccm yenyewe,Serikali na wananchi kwa ujumla wote tumegawanywa na viongozi wetu,Hakuna umoja kama Taifa

Nashauri kiongozi mmoja mkubwa asimame na kuomba msamaha kwa yaliyopita kwa wananchi,Hatapungukiwa kitu akiomba msamaha na kurudisha taifa moja lenye kusikilizana halafu itangazwe siku ya sala na mapumziko

Leo matamko ya corona kila mtu anaonyesha umahiri wa kutoa kauli za kitaalamu kwa kutumia ubabe mungine vaeni mask ,Mungine msivae Mask

Huu ubabe sasa corona imefika mikoani,Mmoja anasema tuchape kazi wengine wanasema mikusanyiko haifai

Kwa huku kupishana kauli za kujikinga .Je wakati wa sala ni sala gani mliyosali isiyo na ukinzani

Nashauri Serikali mmoja wapo aombe msamaha halafu zitangazwe upya siku tatu za sala tena iwe siku ya kazi na watu wapumzike majumbani wasali

Tetesi zinazidi kusambaa kuwa vifaa kwa ajili ya wauguzi hasa huko mikoani hali ni tete,Wauguzi wapo mguu mmoja ndani mungine nje ,Yakizidi hata muda wa kushauriana hautakuwepo,Hizi taarifa zinasambaa lakini wananchi hawajui wamsikilize nani kwenye umoja uliobomoka
 
Acha uvivu nenda kachape kazi weye. Toba haimaanishi kulala au kukaa bila kazi. Hivi wajua kuna watu hutoka jasho kwa sababu tu wapo mezani wanakula?? Tuseme hilo jasho hutokea wapi kama si kwa sababu kula nayo ni kazi?? Basi, shauri hivi; Twende kazini kwa kuwahi sana halafu tuchape kazi kwa bidii kubwa. Huku tukimwomba Mungu kwa kuanza na toba. Ningeomba kiongozi mmoja asimame na kusema; Kazi na sala daima.
 
Baada ya maombi uchwara idadi ya wagonjwa imeongezeka kwa hasira, Mungu hadhihakiwi.
 
Jana nimesoma mahali kuwa sheikh wa huko kigoma akimpongeza magu kuwakumbusha kuliombea taifa dhidi ya corona.Taifa Lina watu wajinga na wanaojipe ndekeza kupita kiasi.
 
Ndio Mana Kuna andiko watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, ugonjwa unajulikana unaenezwa kwa hewa bado watu wanahudhuria mikusanyiko ka nyumbu then wanasali eti corona iwaepuka ka si kukosa akili Nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sisi tuombee nyumbani na kwenye lockdown, Mungu atasikia pia!
 
Taifa hili hivi karibu kumetokea dhambi kubwa mno, zikiwemo za kukamata watu na kuwanyonga wakiacha familia zao kwenye umasikini na masikitiko makubwa, watu walitumia bunduki kuuua, kuteka, kusweka watu gerezani, kupiga, kudhalilisha kunyanganya biashara za watu na kudhibiti vyama vya upinzani, hayo Yote ndio dhambi kuuu tunazotakiwa kuthubu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tubu kwanza dhambi zako mkuu.
Taifa ni watu. Dhambi za taifa ni zangu na zako.

Tubu dhambi yako ya kutokuzingatia masomo. Maana somo la kuandika lilikupiga chini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za wakati huu wapendwa.
Wakati tukiwa katika vita kubwa dhidi ya adui wetu corona hali imekua mbaya kama tunavyoona idadi imekua ikipanda na vifo kutamalaki.

Naipongeza pia serikali kwa kutoa elimu ya kuweza kukabiliana na janga hili pia sekta ya afya nayo wako mstari wa mbele.

Bila kupoteza muda ningependa kuelezea jambo moja bado sielewi mpka wakat juzi kati serikali imetangaza watanzania kwa pamoja tufanye maombi kwa ajiri ya taifa naam mimi binafsi niliguswa na habari hii.

Lakini sasa chakushangaza ninacho kiona hadi wakati huu ni mvua tu kikithiri sa sijui ndio mungu ametu jibu maombi kwa namna hii au kuna jambo jema tunarajie hapo badaye?

Nakaribisha mchango wenu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za wakati huu wapendwa.
Wakati tukiwa katika vita kubwa dhidi ya adui wetu corona hali imekua mbaya kama tunavyoona idadi imekua ikipanda na vifo kutamalaki.

Naipongeza pia serikali kwa kutoa elimu ya kuweza kukabiliana na janga hili pia sekta ya afya nayo wako mstari wa mbele.

Bila kupoteza muda ningependa kuelezea jambo moja bado sielewi mpka wakat juzi kati serikali imetangaza watanzania kwa pamoja tufanye maombi kwa ajiri ya taifa naam mimi binafsi niliguswa na habari hii.

Lakini sasa chakushangaza ninacho kiona hadi wakati huu ni mvua tu kikithiri sa sijui ndio mungu ametu jibu maombi kwa namna hii au kuna jambo jema tunarajie hapo badaye?

Nakaribisha mchango wenu.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu sidhani kama unaweza pata jibu la moja kwa moja kwani majibu ya sala yapo nje ya uwezo wa kibinadamu. Mvua kunyesha mkuu ndiyo msimu wake hivyo kuwa na subira
 
Back
Top Bottom