Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Kipindi mmemshambulia Lisu tulitaka kufanya maombi ya pamoja mkatukataza. Leo hii mnajifanya malaika mnaotambua umuhimu wa maombi wanafki wakubwa nyie.
Unapiga risasi hovyo hewani, utaua hata wenzako, mkuu! Ila chukulia tu kwamba ukimkwepa Mungu hapa mtakutana tu kule!
 
Mwambieni jamaa amuombe Lisu msamaha
Jamaa hatujuani! Mimi nahamasisha maombi tu, na pia nasisitiza toba, ambayo inajumuisha kuomba msamaha watu ulio wakosea! Kwa taarifa yako, nampenda sana TL, ni kiongozi shupavu, na sikubaliani na risasi hata moja aliyo pigwa!
 
Kuna watu wameaminishwa kuwa maombi yaliyo amriwa na Rais kufanyika kwa siku 3 mfululizo lengo na madhumuni ni kumsifu na kumumtukuza Rais wetu kisha kama wajibu kidogo kumtaja na Mungu pia.
Jee ndio makusudio? Na jee wajuzi wa imani huo ndio utaratibu na mfumo wa maombi?
Katika hali kama hiyo jee tumejisogeza kwake kwa unyenyekevu kupata baraka zake au ndio tutegemee majibu tofauti ya tutegemeacho maana tumejiweka mbali zaidi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa hatujuani! Mimi nahamasisha maombi tu, na pia nasisitiza toba, ambayo inajumuisha kuomba msamaha watu ulio wakosea! Kwa taarifa yako, nampenda sana TL, ni kiongozi shupavu, na sikubaliani na risasi hata moja aliyo pigwa!
Umesomeka
 
Viongozi wa dini karibia zote ni watu wa mshahara.

Mpeni Mungu yaliyo yake Mungu na mpeni Kaisari yaliyo yake kaisari!
 
mungu aliye chatu. Ndio maana kumbe tokea ijumaa hamu ya kula gafla imeongezeka nikajikuta nakula isivyo kawaida maana kila ijumaa huwa niko kwa ku fast na kuomba ila week hii imegoma kabisa.1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona baada ya Mkuu kujulishwa kuwa ile plan namba 1 ya kudhibiti Corona kwa watu wote wageni wanaoingia nchini kushindwa, na ugonjwa ushaingia mtaani. Mkubwa alikata tamaa na kuona njia mbadala ni kufanya maombi ya siku 3 labda Mungu atatuonea huruma. Na maombi yetu yasipojibiwa na Mungu huenda atakuja na plan namba tatu.
 
Kama aliyesema siku 3 za maombi aliongozwa na roho wa Mungu, basi maombi hayo yatapata majibu. Lakini kama alifuata utashi wake tu, matokeo tutayaona pia.

Kuna baadhi yetu wanaodhani kuwa utendaji wa Mungu ni sawa na wa binadamu. Kuwa eti Mungu ameshikilia rimoti akifungua na kufunga maambukizi ya korona kama binadamu anavyowasha na kuzima TV. Binafsi nazikataa fikra za aina hiyo.

Utendaji wa Mungu ni tofauti kabisa na fikra za binadamu. Kama binafamu, tumeumbiwa akili na uwezo wa kuyaelewa mazingira na viumbe vilivyomo. Tusijivue huo ufahamu kwa kumsingizia Mungu mambo ya ajabuajabu.

Mungu ana mpango wake usiyoelezeka kwa kutumia akili za binadamu. Mapenzi yake na majira ya kila jambo alilolipanga yatatimia kwa nyakati muafaka. Hakuna binafamu wa kumyingisha wala kumpangia Mungu. TUSEME MAPENZI YAKE YATIMIE.
 
Back
Top Bottom