Kumuomba MUNGU ili akuepushe na janga ukiwa umeita vyomba vya habari vinakumlika ni unafiki wa kiwango cha lamii, yaani unamuomba MUNGU kwa kujianika kwenye TV kwa kugaramia ili uonekane kwa bwana yule kuwa unaomba, huu ni ujuha, huyo MUNGU mnaemuomba kwa staili hiyo mnamjua kweli?
Kibaya zaidi, hawa watu walionekana kuanza mumshukuru bwana yule kabla ya maombi, yaani badala ya kumuomba MUNGU kwa kuwapatia nafasi hiyo, matokeo yake wakaaanza kumshukuru bwana Yule huku wakikodolea kamera ili kuhakikisha bwana Yule anawashika sura zao wasije wakawa wamemaliza maombi na bwana Yule akawa hajawafahamu.
Aiseee tuna kazi kubwa sana ya kufanya nchi hii walahi.
OK namalizia kuuliza swali:
Je, hiyo amri ya take away inahusu na sisi wanywaji? Je, kwa maaana hiyo tukienda bar tuwe tunafungiwa na kuondoka? Khaaaa! watoa muongozo wamepangaranyika mapema sana na ikitokea hili janga likafumuka hata huyu Makonda walahi hutamuona hadharani atabaki ndani akichungulia dirishani kama Bashiru Ally na Polepole.
Sent using
Jamii Forums mobile app