Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Kuna watu wameaminishwa kuwa maombi yaliyo amriwa na Rais kufanyika kwa siku 3 mfululizo lengo na madhumuni ni kumsifu na kumumtukuza Rais wetu kisha kama wajibu kidogo kumtaja na Mungu pia.
Jee ndio makusudio? Na jee wajuzi wa imani huo ndio utaratibu na mfumo wa maombi?
Katika hali kama hiyo jee tumejisogeza kwake kwa unyenyekevu kupata baraka zake au ndio tutegemee majibu tofauti ya tutegemeacho maana tumejiweka mbali zaidi?

View attachment 1423736View attachment 1423739

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ni upuuzi mkubwa. Ibada kama hizi ni ibada za kufuru na dhihika mbele ya Mungu anayetakiwa kuenziwa.
 
Huu ni upuuzi mkubwa. Ibada kama hizi ni ibada za kufuru na dhihika mbele ya Mungu anayetakiwa kuenziwa.
Mkuu katika hali kama hii tutegemee nini zaidi? Maana Mimi nimeingiwa woga kabisa hasa unapoona viongozi wa dini wale makini wako kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uishi Mileleeee Eeh Mtukufu John Pombe Magufuli
Baadhi ya Viongozi wa makanisa Tanzania wameamua Kuwa mashabiki(fanatics) wa ukristo badala ya Kuwa wafuasi wa Kristo. Amelaaniwa amtegemeaye mwanadamu na kumfanya awe kinga yeke. Maandiko yanatukumbusha. Niliyoyaona na kusikia kwenye maombi ya siku tatu Mungu aturehemu kwa kweli.
By; Rev Peter Msigwa
Iringa (urban) MP

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza,
Mkuu hii nchi inabidi igawanywe kuna baadhi ya watu hatutakiwi kuwa nao nchi moja. Wana laana za mizimu. Waachwe waishi wenyewe kama Burundi.
 
Shehe wa mkoa wa Kigoma amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwakumbusha wajibu wao wa kuliombea dua taifa, nao wameitikia wito huo na wametekeleza.

Naye DC Samson amemuomba shehe huyo wa mkoa kuendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Kigoma namna bora ya kujikinga na Covid 19.

Source Clouds tv
 
Ukiwa muumini wa ndimu na limao viwanda vya madawa vitafungwa.Idea ya ndimu inakausha damu imetoka viwandani ili kuwaogopesha watu wasitumie ndimu nao wakakosa biashara
Sure mimi damu yangu ni 14dl plus. Na afya tele. Ndugu wapo hapa home kwa stay home affair wanakula limao na ndimu plus others kama tangawizi, carrot, tango, turmeric etc.

Wengine mpaka lips I.e midomo afya imeimarikaka kabisa. Ukweli baada ya Corona hospital zitaandika maumivu maana kwa hizi recipes kings zitaponyesha magonjwa kama kisukari, cancer, hormonal imbalances etc zitapona.
 
*Extreme Kiranga* : Kuomba na kusali ni kichaka cha kujifichia viongozi wasio na mipango ya kukabiliana na matatizo ya watu. Religion is the opiate of the masses.

*Moderate Kiranga* : Katika nchi isiyo na formal psychotherapy structure, kuomba na kusali kunaweza kusaidia kuwapa watu matumaini, even a placebo effect cure, na ku preserve social order. But social distance must be observed.

*Reasonable Kiranga* : OK, kuomba na kusali kwa imani ya kila mtu ni haki ya binadamu iliyo katika Universal Declaration of Human Rights tangu December 10 1948. Sina tatizo na hilo. Lakini, serikali ina mkakati gani wa kukabiliana na janga hili zaidi ya kutegemea kudra za mwenyezi Mungu tu?
 
Ndio Mana Kuna andiko watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, ugonjwa unajulikana unaenezwa kwa hewa bado watu wanahudhuria mikusanyiko ka nyumbu then wanasali eti corona iwaepuka ka si kukosa akili Nini?
Mungu hachoki ndugu yangu! Yeye anapenda sana tumshirikishe kila jambo, ila ni kweli ni muhimu sana kuzingatia ushauri wa wataalamu kama ulivyo sema! Tumwombe Mungu atusaidie na awasaidie wataalamu wakati huu wa mpambano!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom