Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Coronavirus: Rais Magufuli awaomba Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu

Watanzanja ujumbe umemetufikia tayari. Sasa kuanzia kesho ni maombi ya kitaifa kila mmoja funga na kuomba. Kataa kula chipsi zozote wala chai....naomba kwa ambao hawakuchukulia sirious wachukue hii.....iwe umeokoka hujaokoka,una house boy au house girl mwambie akiache chakula.

Rais amefanya kama mfalme wa ninawi alivyofanya......waliingia wote maombi ya kufunga, wakamlilia BWANA katika dhiki zao,
Akawaponya na shida zao.zaburi 107:6

Nasi tunaenda kumpazia MUNGU sauti zetu kwa pamoja na kwa umoja ili atuvushe ktk msimu mgumu kama huu.

Naomba share kama mlivyoshare ujumbe uliopita, nimeona karibia WATU 2000 mmesambaza.......sambazeni na huu tafadhari. Nakuombea wewe mwenge kufanya kazi hii na kutii kuingia maombi haya Yesu akunusuru na mabaya yote.

_ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao_ .


Sent using Jamii Forums mobile app
Tunapaswa kuingia mtaani na kumwomba jiwe achukue hatua stahiki kama kuzuia mikusanyiko mikubwa na miingiliano kati ya mkoa na mkoa. Hayo yasipofanya kazi ndio tumwombe Mungu.
 
Imani yako haiwezi kuwa sawa na ya wengine.Tumemjua Mungu hata kabla ya Mzungu.
Haha mungu yupi? wa kwenye miti? acha utani hujui historia wewe, au hiyo nayo utasema imeletwa na mzungu? maana wabongo kila kitu mnasingizia mzungu, hata uende chooni gogo likatae utasikia mzungu kanipa dawa.
 
Jambo jema kumludia muumba wetu kwenye mtatizo Kama haya, maandko yanasema bisheni hodi nanyi mtafunguliwa
 
Hi ni dalili ya kukata tamaa
Ongezea na kutoelewa nini kifanyike. Amesha bugi mzee wa watu. Huu ugonjwa si wa kuaibisha. Kama ameshindwa kudhibiti vyanzo vya maambukizi, si mbaya hata akiomba ushauri kwa waliomtangulia kuuguza. Tofauti na hapo, kwisha kabisa. Mungu yupo lakini kwa hii Covid, sijui katoka kidogo.
 
Hi ni dalili ya kukata tamaa
Kweli una maana Pamoja na jitihada ambazo serikali inafanya na zijazo plus hili la kila mmoja wetu kwa imani yake akàombe dua na sala ni dalili ya kukata tamaa? Kweli? Na cases ni chini ya 100.
 
Kuna watawala kadha wa kadha walipokabiliwa na hatari na maadui ambao hawana uwezo nao, walitumia njia hii ya kumwomba Mungu na Mungu akawapigania na kuwashindia. Naamini hata sasa, Mungu aweza (ikiwa ni mapenzi yake) kupigana upande wetu dhidi ya Corona na tukapata ushindi
 
Rais JOHN POMBE MAGUFULI ameomba tutumie hizi siku 3 Ijumaa -waislam waswali kweli kweli
Jmos -wasabato wafanye yao kwa uhakika
Jpili - wale warumi....makanjanja na wooote wa kwenye vibanda umiza wafanye ibada za kweli.


My take.
Vingozi wa dini wakumbusheni waumini njia za kujikinga na maambukizi mapya.
Pia
wakusanye sadaka za mwisho mwisho maana kuna hatari ya kutosali weekend ijayo
 
Kuna watawala kadha wa kadha walipokabiliwa na hatari na maadui ambao hawana uwezo nao, walitumia njia hii ya kumwomba Mungu na Mungu akawapigania na kuwashindia. Naamini hata sasa, Mungu aweza(ikiwa ni mapenzi yake) kupigana upande wetu dhidi ya Corona na tukapata ushindi
Mwenyezi Mungu mpaka apende kutokomomeza hili gonjwa na wala halazimishwi!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia mbaya zipi tunazopaswa kuzitaja mbele ya Mungu wetu ?
Huu ni wakati wa kutubu na kuacha kila njia mbaya na dhambi . Tufanye hivyo si tu kupona Corona Bali kuamua kurejesha uhusiano na Mungu kwa maisha yetu yote and not just temporary

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu ni raisi wa ajabu kuwahi kutokea katika uso wa dunia.

Sent From Galaxy S9
 
Back
Top Bottom