Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

na mgonjwa wetu bado yuleyule mama wa pale mount meru hospital arusha!? au takwimu zinasomekaje hadi wa leo!?

na mkoa ulioathirikka so far ni Arusha tu!?
 
Mimi kabsa huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi kuhusu hiyo likizo, haitaathiri ufanyaji wa mitihani ya kidato cha sita??


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa nini kuna kigugumizi kwenye kufunga mipaka au kulazimisha 14 days isolation kwa yoyote anayeingia? Hivi ukifunga shule huku umeruhusu watu kuingia hovyo nchini kuna faida gani? Kwenye inshu ya Corona serikali imekuwa legevu sana.
Kufunga mipaka ni wazo zuri Sana mkuu na njia sahihi kabisa ya kupunguza kasi ya maambukizi kwa kiasi kikubwa.

Lakini athari za kiuchumi zitakuwa kubwa Sana mkuu, hali ya maisha inaweza kuwa mbaya kuliko hivisasa simply because hizi nchi zetu bado ni importers tunategemea vitu vingi kutoka nje.

hata man power(professionals) kwenye nyanja mbali mbali bado tunategemea kutoka nje so hii inaleta ugumu sana kwenye kufunga mipaka. Japo afya za watanzania ndio kitu cha kwanza .
 
Tunaomba makanisa na misikiti pia vifungwe ili kulinda afya za waumini!!
Sasa tuone manabii feki watakula wapi hawataki kulima wao ni sadaka tuu. Ndipo watajua tunaposema vyuma vimekaza manake nini!!
 
Tunaamini wapo miongoni mwetu "watanzania" watakaojaribu kutumia ugonjwa huu wa Corona kuwatapeli au kuwadanganya watanzania kwa maslahi yao. Mfano tulisikia mtu akijitangaza kuwa na tiba ya Corona, tukasikia mwingine akijigamba Serikali impatie usafiri aende China Mungu amemuonyesha tiba ya Corona.

Sasa je hawa wamewekewa utaratibu gani?

Wapo wanaoweza kuibuka na tiba na kuwahangaisha wananchi, wapo watakaokusanya watu kwa migongo ya imani eti kuombea Corona wakati tumeambiwa mikusanyiko ni hatari kubwa kwa ugonjwa huu.

Mbili kuna watu wanajaribu kupotosha juhudi za kupambana na Corona kwa kuibua ama imani potofu juu ya Corona au kutengeneza habari ambazo zitawafanya watu kutokutilia mkazo hatari zilizopo bali kubaki kunyoshea vidole, mashetani, mizimu, wanasayansi, n.k

Wapo wengine unaona wanatengeneza video zinaonyesha watu wakitupa kondomu na kuvaa maski kufanya mapenzi. Lazima tuamini kupambana na Corona kusiwe sababu ya kuongeza maambukizi ya UKIMWI au ugonjwa mwingine wowote.

Tuombe kila kiongozi wa Serikali ajaribu kutazama idara yake itashiriki vipi katika kupambana na Corona. Mfano Jeshi la Polisi nalo linaweza kujitokeza kukemea wale wote watakaojaribu kutumia korona kufanya utapeli au kupotosha juhudi za kupambana na Corona.

Wizara ya Afya izungumzie kwa ujumla mpambano ya Corona kwa sasa ni namba moja lakini mapambano dhidi ya magonjwa mengine yanaendelea

n.k
 
mlioko karibu na PM hasa waandishi wahabari hebu muulizeni fasta.... sie tuliojazana kwenye mwendo kasi tahadhari ni IPI.?

halafu wengine bado wanapiga chafya na masks hakuna.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Take it easy lad! Huwezi kufunga mipaka ya nchi kwa case moja! Unless unataka kuliweka hili suala kisiasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila mtu mjuzi humu na kila mtu ana details zote za corona!

Kila mtu humu ni dokta, mwanasayansi na mjuvi wa maswala ya uchumi!

Kila mtu anapiga domo, huwezi jua serikali ni ipi wala ngumbaru ni nani! Kila mtu ana masharubu!

Waswahili hawa ni wajuaji kuliko mtu yeyote duniani!
 
Tunaomba makanisa na misikiti pia ifungwe ili kulinda afya za waumini!!
Sasa tuone manabii feki watakula wapi maana hawatakagi kulima wao ni kuzungukia sadaka tuu. Ndipo watajua tunaposema vyuma vimekaza manake nini!!
 
Dah! Shida inakuja kama mzazi alikuwa hajajiandaa kifedha halafu mtoto anatakiwa arudi nyumbani...
Nchi za ulaya hazina boarding. Wanapofunga, watoto wote wanabaki nyumbani. Sisi tunazo boarding. Ukifunga lazima tena wasafiri kurudi nyumbani kwa umbali mrefu. Kuna watoto wanasoma mwanza, nyumbani ni Iringa!

Serikali ilistahili kufahamu mazingira yetu yalivyotofauti na huko corona ilikoanzia. Je siyo rahisi kuwalinda watoto wakiwa shuleni kuliko kuwaruhusu kusafiri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…