Tunaamini wapo miongoni mwetu "watanzania" watakaojaribu kutumia ugonjwa huu wa Corona kuwatapeli au kuwadanganya watanzania kwa maslahi yao. Mfano tulisikia mtu akijitangaza kuwa na tiba ya Corona, tukasikia mwingine akijigamba Serikali impatie usafiri aende China Mungu amemuonyesha tiba ya Corona.
Sasa je hawa wamewekewa utaratibu gani?
Wapo wanaoweza kuibuka na tiba na kuwahangaisha wananchi, wapo watakaokusanya watu kwa migongo ya imani eti kuombea Corona wakati tumeambiwa mikusanyiko ni hatari kubwa kwa ugonjwa huu.
Mbili kuna watu wanajaribu kupotosha juhudi za kupambana na Corona kwa kuibua ama imani potofu juu ya Corona au kutengeneza habari ambazo zitawafanya watu kutokutilia mkazo hatari zilizopo bali kubaki kunyoshea vidole, mashetani, mizimu, wanasayansi, n.k
Wapo wengine unaona wanatengeneza video zinaonyesha watu wakitupa kondomu na kuvaa maski kufanya mapenzi. Lazima tuamini kupambana na Corona kusiwe sababu ya kuongeza maambukizi ya UKIMWI au ugonjwa mwingine wowote.
Tuombe kila kiongozi wa Serikali ajaribu kutazama idara yake itashiriki vipi katika kupambana na Corona. Mfano Jeshi la Polisi nalo linaweza kujitokeza kukemea wale wote watakaojaribu kutumia korona kufanya utapeli au kupotosha juhudi za kupambana na Corona.
Wizara ya Afya izungumzie kwa ujumla mpambano ya Corona kwa sasa ni namba moja lakini mapambano dhidi ya magonjwa mengine yanaendelea
n.k