Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Sielewi hili jambo litakuwaje... Msongamano ktk jiji la Dar nazani haukwepeki, nikiwaza kuhusu usafiri wa daladala ndio nachoka kabisa. Sijui itakuwaje.... Mungu atuepushe.
 
Kuna hoja zinafaa zitekelezwe kabla ya tukio na zingine baada ya case kuwepo nchini.... Kabla ya corona kuingia kinachotakiwa kufanyika ni labda kuzuia safari au sivyo kuandaa karantini... Lakini huwezi kufunga shule na vyuo kabla tatizo halijaingia nchini kaka...kuilaumu serikali kisa haijafunga taasisi za elimu kabla mdudu kutua ni kuionea.

Na kwa nini hawajafunga mipaka, kwa lugha nyepesi hamna hatua za muhimu zinazochukuliwa kwa wakati, maana mpaka saivi mipaka ipa wazi na tunaweza kuingiza case mpya muda wowote.
 
Umasikini ni mbaya sana! Serikali ya CCM mbona ni manunda sana hamsikii kilio cha raia wenu kuhusu kufunga mipaka
 
Hilo ni kweli. Hata hivi sasa serikali bado inakuwa reactive instead of being proactive. Given the fact hili suala limefahamika well in advance na tv etc wanazo. Nadhani serikali inaenda taratibu kwasababu wanafahamu janga litakaloukumba uchumi wetu kutokana na hatua hizo mfano Total lockdown.

Na tunapoelekea hilo halikwepeki, kwahiyo waliokuwa wakilalamika vyuma vimekaza, wajindae maana vinaenda kupata kutu kabisa.

Kwa uzoefu wangu, hata serikali ikiwa proactive, kuna wataosema ‘serikali inatisha watu, serikali ina panic, nk.

Hata iweje, binadamu haridhiki.

Sikupingi. Bali nasema tu kulingana na observation yangu ya tabia za binadamu.
 
Sasa ile mikutano nchi nzima ya Mh.Mbowe ya tarehe 4/4/2020 itakuwaje au itasogezwa mbele?
 
Umasikini ni mbaya sana!
Uganda maskini wenzetu wanalazimisha yoyote anayetaka kuingia atakaa siku 14 isolation, hutaki rudi ulipotoka, kwa nini sisi tuwe na kigugumizi, kwa nini tusijikinge ugonjwa kuingia ila tunajiandaa kupambana nao mtaani ambayo ni vitu ngumu Zaidi.
 
Back
Top Bottom