Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Coronavirus, Tanzania: Shule zote kuanzia za Awali, Msingi na Sekondari zafungwa. Mikusanyiko ikiwemo ya Kisiasa yasitishwa

Bado tuna manabii na mitume uhange wanaoendelea kuhubiri uponyaji wa Corona kwa kutumia upako na keki.Wanatuzingua kwa kusema imetokana na shetani na majini. Serikali inayajua haya? Au ndo huo uhuru wa kuabudu na kupotosha wananchi?

Halafu kuna nchi ambazo zimefunga mipaka yao na imepiga marufuku mikusanyiko yote, hata ya misikiti na makanisa. Sisi je?
small minds and dwarf lazima zitumike kama mitaji kwa watu wajinga wajinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa vile Uganda wamefanya na sisi tufanye sio?
 

Attachments

  • IMG-20200317-WA0044.jpg
    IMG-20200317-WA0044.jpg
    41.2 KB · Views: 1
Mazigazi,
Kisukari kinaambukaza? malaria inaambukiza? usikariri tu takwimu analyse issue.
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametangaza kusitishwa shughuli zote za mikusanyiko kuhofia Corona.

Hivyo shule zote zimefungwa kwa siku 30 kuanzia jana. Michezo kama Ligi Kuu imesitishwa kwa mwezi mzima.

Lakini ikumbukwe kwamba muungano wetu Tanganyika na Zanzibar una matatizo kama haya.

Suala la Afya si la Muungano. Suala la michezo si la Muungano.

Waziri wa Afya Zanzibar hajatangaza kuwepo mgonjwa wa Corona nchini mwake.

Waziri wa Elimu wa Zanzibar hajafunga shule za nchini mwake.

Kimsingi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijatangaza au kusitisha chochote kuhusiana na Corona.

Hivyo ile amri ya Waziri Mkuu wa Tanzania imekomea Bara tu na haina nguvu Zanzibar.

Jadili.
 
Nadhani tuuite muunganiko wa sekta chache
 
Back
Top Bottom