Cost comparison SGR Kenya vs SGR Tanzania

Ni sababu zipi hizo mkuu? Ziweke tuzijadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sababu zipi hizo mkuu? Ziweke tuzijadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu angejua kwanini WB wamelazimisha MGR asingeongea! Kiukweli ni sababu ya Ujerumani as one of WB donors, wants to keep his heritage intact within her old colony! Sababu ndio maana hata GoT ilipokuwa na nia ya kuanza SGR wakakataa ku-contribute funds walizopeleka NGR kwa SGR. Na wakati TRC inabomoa jengo la abiria Dar walipiga kelele! Ni Wajinga sana hawa jamaa! wangoje most of their inland NGR terminals zitabomolewa kupisha modern SGR terminals!
 
My friend, huko kukusanya kodi za kutosha hakutakuja tu kimiujiza. Yaani, siku moja tu tuamke na kukuta tunaweza kukusanya hizo kodi za kutosha. Bali ni mchakato ambao pamoja na mambo mengine ni lazima kuwekeza ili kujiongezea huo uwezo wa kutosha.

Naona hautaki kuzitaja hizo sababu zilizopelekea MGR na TAZARA kuzorota na kufa (kwa TAZARA) ila kimsingi tatizo haijawahi kuwa pesa bali utashi wa kuziendesha.

Kwa upande wa hiyo MGR (reli ya kati) ilikuwa lazima tufanye maamuzi magumu ili kuupa uchumi wetu competitive advantage kwenye eneo zima la maziwa makuu (Dar vs Nairobi).

Ikumbukwe kuwa soko letu la msingi kimataifa ni eneo hili hivyo ni lazima kuwekeza kwenye miundombinu ya msingi ili kuwapa wazalishaji wetu competitive adv. dhidi ya washindani wetu na hasa #254.

Vinginevyo tulikuwa tukizidi kujiweka kwenye very disadvantaged position na kama ile COW ingefanikiwa basi tungekuwa tushapoteza.

Kuhusu madeni kutolipika ni upuuzi na ujinga wetu wenyewe waafrika. Pesa nyingi tunazokopa huenda kwenye miradi uchwara isiyo na tija wala uendelevu.

Kwa mfano. Nchi ya kiafrika inakopeshwa dola milioni 300 kwa ajili ya mradi wa kuelemisha jamii kuhusu utunzaji wa mazingira. Hapo utakuta kuna uhusishwaji mkubwa wa hao wanaokopesha kupitia NGOs na makampuni yao ya consultancy.

Mikopo ya aina hiyo huisha kwa sehemu kubwa ya pesa hizo kurudi kwa mkopeshaji. Mzigo wa deni unabaki kwa mkopaji ambaye ataulipa kwa muda mrefu kupitia vyanzo vingine kabisa vya mapato.

Hapo hapo ukiwaomba wakukopeshe kwa ajili ya mradi wa kuzalisha umeme kwa mfano, ili kuyalinda hayo mazingira utaambiwa mradi hauna tija hivyo haukopesheki.

Sasa kwa mazingira hayo siyo kwamba ni makosa kukopa kwa ajili ya miradi kama SGR bali tuache kukopa pesa kwa ajili ya miradi isiyo na tija. Kama vile serikali hii inavyokataa mikopo ya aina hiyo kitu kinachowakwaza wakopeshaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuna uwezo wa kujenga MGR ila kuna mkopo wa World Bank unatumia kukarabati MGR.

Kukarabati MGR ni nafuu, ingawa haifiki specifications za SGR lakini inatosha kabisa kukidhi mahitaji ya nchi kwa miaka mingi ijayo.
Kwenye usafirishaji tunahitaji mambo matatu;

1. Reliability
2. Frequency
3. Speed

Sasa naomba u-weigh SGR vs MGR against hivyo vitu vitatu halafu uniambie ipi inahitajika zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Linganisha gharama ya kujenga SGR na kodi tunayokusanya. Pia mradi huu hautakuja kurudisha gharama za ujenzi wake.

Tungejiuliza kwa nini tumefeli kwenye MGR na TAZARA kabla ya kuwa na ndoto kubwa zisizo na uhalisia.
Ni kwa nini SGR haitakuja kurudisha pesa? Mradi kama huu, viability yake unaipimaje mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na huu ndio ukweli, ss leo Magu anakuja kubadili fikra za muafrika lkn bdo ukoloni unatusumbua, ila cna shaka na Magu cz amepewa moyo mgumu sn atapambana kubadili fikra mpk kitaeleweka tu, unajua baada ya hii covid-19 kupamba moto nmekuja kugundua Afrika inadharaulika kwa kiasi ambacho hakina kipimo, hvyo ni muda muafaka ss kwa waafrika kuwaonesha hao washenzi kwamba hata Afrika iliwahi kutawala dunia kupitia Egypty na tunaweza kuirudisha ile zama kupitia taifa lingine la Afrika km tutakuwa na fikra chanya.
 
Itafika lakini ni baada ya zaidi ya miaka 15, hatuna uwezo wa kiuchumi kwa sasa wala sidhani kama tunaweza kupata mkopo wa hela nyingi hivyo.
Uingereza (London) walipoona uhitaji wa reli za ardhini ili kutatua tatizo la usafiri wa mjini, hawakuwa na uwezo wala uzoefu wa kujenga mtandao mzima. Walichoamua ni kuanza na kipande kifupi cha km 8 tu! Wangetumia akili kama hizo za kusubiri full capacity nao wangekuwa kama sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Quote of the day, this is the best comment of the week.
 
Mapato kidogo kutokana na mizigo kidogo inayobebwa. Mapato kidogo maana yake ni poor maintenance. Hata kama reli ikijengwa idumu kwa miaka 100, maintenance ikikosekana baada ya miaka michache ufanisi unashuka.
Una uhakika mizigo ya Zambia-Malawi-Tz ni kidogo na haitoshelezi uhitaji wa Tazara? Kwa nini unazungumzia kitu usichofahamu? Sasa kama mzigo ni kidogo, ni kwa nini tusiifumue tukauze chuma chakavu?

Akili kama hizi ndizo zimezorotesha Tazara na reli ya kati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia attachment hii kuona tathmini ya World Bank kuhusu SGR na East African Community.

https://africog.org/wp-content/uploads/2017/06/World-bank-Report-on-the-Standard-Gauge-Railway.pdf

View attachment 1417573
Hao world bank walisema nini walipotembelea ujenzi wa SGR? Msipende kutegemea akili za wazungu nyie watu. Wewe uko na kaupembuzi kao yakinifu uchwara wenzako wamekwisha geuza gia angani wakausifia mradi na kusema wako tayari kuukopesha.

Tatizo la waafrika ni kudhani wazungu ndiyo watu sahihi kutupangia namna ya kuendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwa nini SGR haitakuja kurudisha pesa? Mradi kama huu, viability yake unaipimaje mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Jiulize kwa nini UDART, TAZARA na MGR hazina ufanisi. Hili swali wewe ndiye wa kulijibu siyo mimi.

Kama hata kuoperate km 21 za BRT unashindwa nini kinakupa matumaini ya kuendesha SGR?
 

Unapinga huo upembuzi kwa maneno ya wanasiasa. TAZARA wako hata mishahara wanasuasua kulipa.
 
Ili SGR iwe na tija haina budi kufika nchi jirani ili kuongeza wingi wa mizigo.

Tungejitahidi kukuza uchumi wetu na kuongeza ukusanyaji kodi. Tukiwa na uchumi imara na kipato cha kutosha tunaweza kupata mkopo nafuu wa kujenga network yote ya SGR.
My friend, ili huo uchumi ukue lazima kuwekeza kwenye miundombinu kama hii ili kuuchochoea. Hauwezi kukaa tu eti usubiri ukue.

Pia lengo la SGR siyo tu kuwasafirishia hao majirani mizigo bali pia kuwarahisishia wazalishaji wetu namna ya kupeleka bidhaa zao kwenye hizo nchi.

Hivi unayo hata idea moja ya uchumi kweli wewe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…