Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu, arosto yako ipo karibu sana isee, si sasa hivi tu umetoka kula vitu.....😀😀😀😀Arostooooooo
Acha kabisa mkuu ni hatariMkuu, arosto yako ipo karibu sana isee, si sasa hivi tu umetoka kula vitu.....😀😀😀😀
Hahaaa kumbe [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23]Bold bhana ...yaani kachanganya movie ya I AM THE LEGEND, GAMES OF HANGER NA CONTAGION na kutengeneza makala...aiseee
🖊🖊🖊🖋🖍📝📝deep stateDEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#4
Niko mzima wa afya… tuendelee.
Wengi tuko nyumbani sababu ya karantini… nitajitahidi niweke content ya kutosha karantini iwe mwanana.
Nilikuwa naeleza kuhusu "Deep State" na namna gani inafanya kazi.
Nikaeleza kuhusu kampuni ya Blackwaters Worldwide na alafu nikageukia kwenye hafla ya White House Correspendents Dinner ya mwaka 2011 mwezi April.
Rejea tena kile ambacho nilieleza kuhusu nyaraka mbili za siri kubwa pale Marekani lakini zote mbili hazina muhuri wa SIRI. Mojawapo ya nyaraka hizo naweza kuifananisha na "Site Post Assignment Log" ya ndugu zetu wa Kisarawe hapa Tanzania.
Kabla ya Rais Obama kuwasili kwenye ile hafla, watu wa Secret Service walipata taarifa kwamba kuna binti ambaye ni mfanyakazi wa White House alikuwa amepoteza PIN ambayo ilikuwa inampa access ya maeneo muhimu ya pale Ikulu ya Marekani.
Sasa,
Nilisema zile nyaraka ziko mbili… moja ni hiyo ambayo nimeieleza ya kufanana na hii yetu ya "Site Post Assignment Log", nyaraka ya pili ina shabihiana na hii ya kwanza lakini ina tofauti kidogo.
Nyaraka hii ya pili yenyewe inaonyesha movement zote za Rais. Kwa mfano katika siku husika inaonyesha atakuwa wapi. Atapita njia gani kufika mahala anakokwenda. Atatumia usafiri gani kama ni motorcade au chopa au ndege. Inaonyesha mpaka lifti gani atatumia kama ni jengo fulani atakuwa anakwenda.
Kama ni tukio fulani anahudhuria basi itaonyesha ni watu gani ambao atasalimiana nao na ni mahala gani ataketi na kadhalika.
Movement zote za Rais zinakuwa kwenye nyaraka hii.
Jambo la muhimu pia kukumbuka ni kwamba nyaraka hizi zote ziko kidigitali.
Sasa,
Hiyo PIN ambayo mfanyakazi wa White House alikuwa ameipoteza ni kama 'key card' ambayo inakupa access ya maeneo ndani ya White House.
Huyo binti mwenyewe alikuwa anadai kwamba alikuwa nayo hapo White House masaa machache tu ba hajui namna gani imepotea.
Nimeeleza kwenye sehemu iliyopita kwamba katika hafla hii kulikuwa na wahudhuriaji adhimu kweli kweli… Rais mwenyewe, Mwenyekiti wa Joint Chief Staffs, Magavana, Maseneta n.k. Donald Trump pia alikuwa mgeni mualikwa kwenye hafla ile. Ile video ilikwenda 'viral' Obama akimtania Trump…ilikuwa ni siku hii.
Hivyo kama kulikuwa na mtu ana nia mbaya basi hii ilikuwa ni 'target' yenye kumfanya atoke udenda kwa kuitamani.
Hivyo kitendo cha binti huyu kupoteza Key Card ya Ikulu siku ile ile ambayo Viongozi wakuu wa nchi watahudhuria kwa pamoja tukio kwenye eneo la kiraia, hii ilikuwa ni 'compromise' kubwa ya kiusalama sababu walikuwa hawajui hiyo Key Card imekwenda wapi na iko mikononi kwa nani kwa muda huo. Na kama iko kwenye mikono hatari je mtu huyo tayari atakuwa amepata access ya kiasi gani cha taarifa nyeti na pengine ku-compromise usalama wa Rais kama akihudhuria hafla hiyo?
Kiusalama huwezi kusema tu kwamba hii ni 'coincidence' tu… kwamba ni bahati mbaya tu imetokea siku ambayo viongozi wa juu wote wa nchi wanahudhuria tukio sehemu moja alafu kuna mtu wa Ikulu amepoteza Key Card ya kumpa access ya maeneo nyeti ndani ya Ikulu.
Linapotokea tukio kama hili kuna hatua tatu za kiusalama ambazo unaweza kuchukua..
Mosi, unafanya tathimini ya 'damage' ya kiusalama ambayo inaweza kuwa imekwisha tokea kama hiyo key card imedondokea kwenye mikono hatari.
Pili, ukisha fanya hiyo tathimini kama 'damage' ya kiusalama si kubwa sana unaweza kubadili protocols, procedures na masuala kadhaa kisha kuweka mkakati mpya na kuendelea na oparesheni (Rais Kuhudhuria hafla).
Tatu; kama damage ni kubwa ya kiusalama basi mnaweza kuhahirisha tukio hilo kwa siku kadhaa kwanza mjiridhishe ni nini kimetokea kabla ya tukio hilo kufanyika.
Au Rais anaweza asihudhurie na badala yake akatuma mwakililishi.
Katika tathimini hiyo watu wa Secret Service wakaona kwamba damage ni kubwa sana kama Key Card hiyo imedondokea kwenye mikono hatari sababu kama iko mikononi mwa mtu huyo basi ataweza kwa urahisi kabisa kupata access ya zile nyaraka mbili ambazo nimezisema awali sababu zote ziko kidigitali na unaweza kuona movement za maafisa usalama na Rais in real time.
Hivyo mbele yao wana machaguo matatu… eidha wabadili protocol na procedures na pengine agents waliopangwa kwa tukio hilo wote wabadilishwe.
Lakini hii isingewezekana maana ilikuwa yamebakia kama masaa mawili tu kabla ya hafla kuanza. Na kama ambavyo nilieleza suala la ulinzi kwenye matukio kama haya, Secret Service wanaratibu kwa kushirikiana na jeshi pamoja na local PD. Hivyo isingewezekana kufanya 'overhaul' ndani ya muda mchache namna hiyo.
Kwa hiyo chaguo pekee ambalo lilikuwa limebakia mezani ni eidha wahahirishe hiyo hafla na ifanyike siku nyingine au Rais Obama asihudhurie kabisa tukio hilo atume mwakilishi.
Lakini hii isingewezekana, sababu Obama sio tu kwamba alikuwa anahudhuria tukio hili sababu ya utamaduni na ratiba.. tukio hili pia lilikuwa linatumika kama 'diversion' ya tukio kubwa zaidi ambalo lilikuwa linaendelea kwa siri kubwa nyuma ya pazia.
Kulikuwa na tukio kubwa zaidi linaendelea, na Obama alikuwa anapaswa kuhudhuria hafla hii kama sehemu ya geresha kuziba tukio ambalo lilikuwa linafanyika nyuma ya pazia ambalo hata Secret Service hawakuwa na 'clearance' ya kufahamu tukio hilo.
Kwa sasa karibia wote duniani tunalifahamu tukio lenyewe na kama umelisahau basi baada ya haya kadhaa hapo chini nitalieleza.. lakini kwa siku pengine hakukuwa na siri kubwa zaidi kuzidi ufanyikaji wa tukio hilo ambali limekuja kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kiusalama yaliyotokea kwa miaka ishirini iliyipita.
Kwa hiyo ilikuwa ni lazima Rais Obama ahudhurie hafla ile.. na alihudhuria.
Kitu ambacho kilifanyika sidhani kama kimewahi kufanyika kabla na Rais yeyote wa Marekani. Mwaka 1985 Rais Nixon aliwahi kufanya kitu cha kufanana na hiki lakini si kwa ukubwa huu ambao ulifanyika siku ile April 30 mwaka 2011.
Ukipata nafasi igia mtandao wa Youtube au google… tafuta tukio hili ninalolieleza "White House Correspondents Dinner" mwaka 2011. Tazama motorcade ya Obama akiwa anawasili alafu kisha tazama ile 'inner perimeter' ya Maafisa wanaomlinda. Linganisha maafisa hao na maafisa kwenye matukio ya nyuma… utapata jawabu moja kwamba maafisa wale hawakuwahi kuwepo kwenye security detail yake hata mara moja kabla ya siku ile.
Kama ni mfuatiliaji wa masuala haya basi utakuwa unawajua 'body guards' wa Rais Obama enzi zile au Trump kwa sasa.
Ni kama hapa kwetu ambapo wafuatiliaji wa haya mambo ni kawaida tu watu wanawajua walinzi wa mzee… kuanzia yule mama kipindi mzee ndio ameingia madarakani, kisha yule jamaa aliyepelekwa TCRA, alafu huyu bonge black ambaye ni mwanasheria by profession, pamoja na huyu 'ustadh' wa siku hizi. Well, hatuwezi andika majina hapa kwa sababu ya maadili lakini 'vijiweni' huko wafuatiliaji wa habari za namna hii wanawajua.
Ndivyo kama vile ambavyo tulikuwa tunawajua mpaka kwa majina walinzi wa Obama na sasa Trump..
Sasa kama wafuatilia haya mambo nikuulize, ni mlinzi gani wa Obama ambaye amejizolea umaarufu sana mpaka sasa.?? Jawabu ni afisa Usalama anaitwa Dan Bongino ambaye kwa sasa baada ya umaarufu ametoka Secret Services na siku hizi ni political commentator.
Sasa tazama hiyo footage ya Obama akiwa kwenye hiyo hafla.. huwezi kumuona Dan Bongino na wenzake. Badala yake utaona sura mpya tupu.
Who were these guys?? Wametoka wapi… na nini kimetokea baada ya ile key card kupotea.??
Pale juu nimesema baada aya kadhaa nitaeleza kwa nini ilikuwa ni lazima Obama ahudhurie hafla ile.. sio tu sababu ya ratiba au utamaduni wa Ikulu, la hasha sababu pia alikuwa anatakiwa kuhudhuria kwa kuwa pia tukio hilo lilikuwa linatumika kama diversion.
Kwa sababu ya nini? Na tena, nini kilitokea…
Pale Marekani wenzetu wana utaratibu mmoja hivi mzuri sana kuhusu uratibu wao wa Intelijensia.
Wajua nchi zetu nyingi hizi za ulimwengu wa tatu na hata hapa kwetu bado ufanisi wetu wa uratibu wa intelijensia uko chini sana. Kwenye ulimwengu wa ujasusi haijalishi una taarifa adhimu kiasi gani… suala la msingi ni namna gani unafanyia kazi taarifa ulizonazo.
Mfano Jeshi la Polisi wa Idara za Intelijensia, Jeshi la Wananchi wana Idara ya Intelijensia, alafu pia tuna Idara ya Taifa ya Usalama… maana yake ni kwamba unakuwa na furushi kubwa sana la taarifa… sasa ni namna gani unameng'enya taarifa hizi ziweze kuliwa kwa urahisi na kiongozi mkuu wa nchi ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kutoa maamuzi makuu ya nchi?
Mparaganyiko huu wa intelijensia uliwagharimu sana Marekani na kutoa mwanya wa kutokea tukio la shambulio la Septemba 11. Kuna taarifa adhimu FBI walikuwa nazo kabla ya tukio lakini CIA walikuwa hawazijui… na kuna taarifa adhimu ambazo CIA walikuwa nazo lakini FBI walikuwa hawazijui. Pia NSA walikuwa na taarifa muhimu lakini pia FBI na CIA walikuwa hawazijui. Kila mmoja alikuwa anashindana kumlisha Rais intelijensia kwa muono wake.
Baada ya tukio la Septemba 11, Marekani wakaanzisha ofisi ya Director of National Intelligence.
Taarifa zote za ujasusi na Intelijensia toka idara zote zinapita hapa na kisha kumeng'enywa, kuangalia namna gani zina compliment each other.. kuzitafasiri and try to make sense out of it… Director of National Intelligence ndiye anakuwa kama link ya idara zote za Ujasusi na huyu ndiye anawasilisha Rais intelijensia yote ya nchi ikiwa imemeng'enywa na yenye maana.
Yani kwa ufupi huyu ndiye anaratibu intelijensia yote ya nchi kutoka vyombo vyote ambazo zinapaswa kufika kwenye meza ya Rais.
Sasa, nataka uone kitu fulani..
Kipindi hili tukio linatokea, Mkurugenzi wa National Intelligence alikuwa anaitwa James Clapper. Huyu ni Luteni Jenerali mstaafu wa vikosi vya Anga, Air Force. Huyu alishika wadhifa huo kuanzia mwaka 2010 mpaka mwanzoni mwa Urais wa Trump mwaka 2017.
Kabla yake Director of National Intelligence alikuwa ni bwana mmoha anaitwa John McConell. Huyu ni Vice Admiral mstaafu wa vikosi vya Navy.
Sasa kuna jambo la ajabu sana nataka ulione…
Kabla ya James Clapper (ambaye ndiye alikuwa Director of National Intelligence kipindi lile tukio la April 30, 2011 linatokea) kuteuliwa kushika wadhifa huo alikuwa ni Executive kwenye kampuni binafsi inaitwa Booz Allen. Alikuwa ni Executive huko Obama akamteua kuwa Director of National Intelligence.
Yule aliyemtangulia, yaani aliyekuwa anampisha kwenye wadhifa huo, John McConell alipoachia wadhifa wa Director of National Intelligence akarudi uraiani na kuwa mwenyekiti wa bodi wa Kampuni hiyo hiyo inayoitwa Booz Allen.
Yaani kama ingekuwa hapa kwetu… tuseme mzee alivyoingia magogoni, amchukue Mkurugenzi wa Vodacom alafu amuweke kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa. Alafu yule Mkurugenzi anayestaafu atoke usalama qa Taifa aende kuwa Mwenyekiti ya Vodacom.
Wakati wengine wanaisifu na kuipongeza Vodacom ni kampuni makini kwa kutoa watu adhimu… mimi na wewe ambao hatuishi kwenye ulimwengu wa 'maji na mchanga' tunapaswa kujiuliza why?? Kwa nini Vodacom?? Kuna nini pale kinaendelea??
Ndivyo hivyo unapaswa kuuliza… why Booz Allen?? Iweje marais wawili, kutoka vyama viliwi tofauti, wenye mitazamo tofauti kabisa wote wawili wachague "Wakurugenzi wa Usalama wa Taifa" kutoka kampuni moja binafsi ya kiraia inayoitwa Booz Allen.
Niliwaambia kwamba nataka nieleze Deep State ni nini na namna gani inafanyakazi…
Sasa hili tukio ambalo nawaeleza hapa ni mfano wa tukio tunayaita "Deep BEvents"... ni matukio ambayo yanahitaji jicho la tatu kuweza kuyang'amua.
Ni matukio ambayo yanapangwa with 'surgical precision' na yakishafanyika yanabadili kabisa upepo wa masuala fulani ya ulimwengu.
Bado sijajibu swali la zile sura mpya kwenye security detail ya Obama zilitoka wapi… na nini kilitokea. Na pia swali la msingi zaidi… kwa nini Booz Allen??
Naja..
Habib "The Bold" - 0718 096 811
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahhahha, kwamba umeconect dot!Kuitolea mfano vodacom kuna kitu nimejiuliza pale nakumbuka raisi alilalamika kwanini vodacom wanamuajiri mkurugenzi mpya wa kigeni kutoka Kenya wakati watanzania wapo wenye uwezo kama wake tusio jua tukamuona raisi mbinafsi mwenyewe majungu miezi ikakatika miaka ikakatika mara gafla kuna sauti zimerekodiwa za viongozi fulan kutoka chama fulani kikubwa na viongoz serikalini hapa Tanzania zikimteta raisi ambae ni mwenyekiti wao na boss wao wakisema mshamba ajui kuongoza nchi mkurupukaji ni mengi mabaya walimzungumzia Leo kwa mara ya kwanza ndugu Habibu B Anga nimekuerewa uchambuzi wako vizuri sana usichoke kuendelea kutupa vitu adimu kama hivi asante pia kwa uwongozi wa jf kumkaribisha mtu kama huyu asanteni
Inakera sana, unasubiria dakika kadhaa ndio uzi unafunguka, wakati mwingine mpaka unakata tamaa unaamua kufungua uzi mwingine.
Ni ya ukweli hayo? au watufitinisha na The Bold...Tulio wasap asaiv tuko sehemu ya tisa
Kwa hiyo wewe unaona walichofanya voda walikuwa sahihi?Kuitolea mfano vodacom kuna kitu nimejiuliza pale nakumbuka raisi alilalamika kwanini vodacom wanamuajiri mkurugenzi mpya wa kigeni kutoka Kenya wakati watanzania wapo wenye uwezo kama wake tusio jua tukamuona raisi mbinafsi mwenyewe majungu miezi ikakatika miaka ikakatika mara gafla kuna sauti zimerekodiwa za viongozi fulan kutoka chama fulani kikubwa na viongoz serikalini hapa Tanzania zikimteta raisi ambae ni mwenyekiti wao na boss wao wakisema mshamba ajui kuongoza nchi mkurupukaji ni mengi mabaya walimzungumzia Leo kwa mara ya kwanza ndugu Habibu B Anga nimekuerewa uchambuzi wako vizuri sana usichoke kuendelea kutupa vitu adimu kama hivi asante pia kwa uwongozi wa jf kumkaribisha mtu kama huyu asanteni