SEHEMU YA PILI
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani.!?
#2
Jana niligusia kuhusu maabara ya Wuhan Institute of Virology - WIV inayoongozwa na mwanamama msomi wa Kichina na mwanasiasa Dr. Wanga Yanyi, nikaeleza kuhusu kupanuliwa kwake na kisha kupandishwa hadhi toka BSL-2 mpaka BSL-4 ambayo ndiyo daraja la juu kabisa la kiusalama kwenye maabara zenye kuhusika na urutubishaji, uundaji na utumiaji wa biological agents.
Kisha nikaanza kueleza kuhusu tukio fulani lililotokea mwaka 2011 nchini Pakistan jimboni Lahore.
Sasa,
Wakati yule Mmarekani aliyekamatwa kwa tuhuma za kuua Wapakistani wawili akiwa anahojiwa na Polisi, kitengo kingine kilikuwa kinafuatilia mawasiliano yake katika simu ambayo walimkuta nayo. Simu ile ile ambayo ndani yake zilikutwa picha za maeneo ya siri ya kijeshi yaliyoko mpakani mwa Pakistan na India.
Katika kuchunguza mawasiliano ya simu ya Raymond Allen polisi wakagundua kwamba aliwasiliana na simu nyingine ambayo ilikuwa maeneo ya barabara maarudu hapo Lahore inayoitwa Jail Road.
Ubaya ni kwamba siku ile ambapo Raymond anapata mkasa kwenye makutano ya barabara Qurtaba eneo hilo lingine ambalo kuna mtu alimpigia simu, yaani Jail Road nako kulikuwa kuna mkasa mwingine wa ajabu sana ulikuwa unatokea.
Watu walioshuhudia tukio hilo lingine hapo Jail Road walidai kwamba ilitokea gari aina ya Toyota Land Cruiser ndani yake kukiwa na wanume wanne wenye asili ya kizungu ambayo ilikuwa inaendeshwa kwa kasi mno huku ikifanya 'overtake' za hatari kabisa. Bahati mbaya barabara hii Jail Road huwa kwa kawaida ina foleni kubwa.
Mashuhuda wanasema kwamba baada ya gari hiyo kukwamba kwenye foleni, dereva aliitoa gari kwenye upande anaopaswa kuwa na kuanza kuendesha kwa kasi ile ile upande mwingine dhidi ya magari yanayokuja mbele.
Mashuhuda wanadai kwamba ilikuwa ni kama wanaangalia filamu kwa namna ambavyo dereva alikuwa akiendesha kwa kasi huku akikwepa magari ambayo yalikuwa yanakuja mbele yao.
Ikatokea kwamba wakati gari hii Land Cruiser ikiendeshwa hivi kwa kasi kwenye 'saiti' ambayo sio yao, kulitokea pikipiki ambayo yenyewe ikawa inakuja kwa kasi sana mbele yao. Gari ikashindwa kukwepa pikipiki hii na wakagonga vibaya sana kiasi kwamba pikipiki na dereva wake wakatupwa nje kabisa ya barabara.
Ajabu ni kwamba gari hiyo haikusimama bali iliendelea na safari kwa mwendo ule ule wa kasi na upande ule ule wa barabara ambao hawakupaswa kuwa wanaendesha.
Sasa, awali polisi walisikia kuhusu mkasa huu lakini hakukuwa na hisia yoyoye kwamba labda pengine matukio haya yalikuwa yanahusiana.
Lakini baada ya ripoti ya wataalamu wao wa teknohama kugundua kwamba Raymond muda ule ule ambao alikuwa anapiga watu risasi aliwasiliana na mtu kwa simu ya mkononi simu ambayo ilikwenda kwenye namba ya simu ya mtumiaji ambaye alikuwa maeneo ya Jail Road hapo ambapo pia nako walisikia kuhusu tukio lile la gari kuendeshwa kana kwamba kwenye filamu wakaanza kuhisi pengine kulikuwa na uhusiamino kati ya matukio haya mawili.
Lakini sababu ya pili ni vile barabara hiyo ya Jail Road ukiifuata inakwenda kutokea moja kwa moja pale makutano ya barabara ya Qurtaba ambako kulitokea tukio la Raymond kupiga Wapakistani wawili risasi.
Lakini sababu ya tatu ambayo ilikuwa ya kushangaza zaidi ni kwamba kwa kutumia camera za usalama mtaani polisi walifanikiwa kupata namba za ile Land Cruiser ambapo ilionekana kwamba imesajiliwa kwa namba LZN-6970. Lakini walipofuatilia namba hizi wakang'amua kwamba zilikuwa za bandia sababu namba hizo zilikuwa zimesajiliwa jimboni Punjab kwa jina la mtu anayeitwa Sufi Munawwar Hussain.
Wasiwasi wa Polisi kituo kikuu hapo Lahore ukaongezeka zaidi juu ya huyu mtu ambaye majina yake kwenye kitambulisho yalionyesha anaitwa Raymond.
Kuna majina matatu ambayo ni muhimu sana kuyakumbuka kadiri ambavyo tunaendelea na andishi hili.
Wale Wapikistani wawili ambao Raymond aliwapiga risasi mmoja alikuwa anaitwa Faizan Haider, ambaye alikuwa na miaka 22 na yule mwenzake alikuwa anaitwa Faheem Shamshad (pia alikuwa anajulikana kwa majina ya Muhammad Faheem) ambaye huyu alikuwa ni kijana wa miaka 26.
Yule jamaa aloyegongwa na Lad Cruiser pale Jail Road jina lake alokuwa anaitwa Ebadur Rehman (pia jina hili kwa ligha ya Urdu linatafsiri kama Ibad-ur-Rehman).
Yakumbuke majina haya matatu.
Juzi niliwaeleza kwamba katika kitambulisho ambacho Raymond alikutwa nacho kilionyesha kwamba alikuwa ni muajiriwa wa kampuni inayoitwa Hyperion Protective Consultants ambayo nilieleza kuwa hii ilikuwa ni shell Company ya kampuni mama ya Blackwaters Worldwide ambao nikasema hawa ni moja ya 'contractors' wakuu wa CIA.
Kuna jambo la msingi sana kulielewa kuhusu hawa Blackwaters Worldwide kabla sijaendelea mbele sana.
Kama umekuwa mfuatiliaji wa vita ya Iraq basi sina shaka utakuwa umewahi kusikia kisanga cha Nisour Square Massacre.
Kisanga hiki cha Nisour Square Massacre pengine ndio moja ya skandali kubwa ya kwanza kufanya Marekani wakosolewe vikali na hatimaye wafanye mabadiliko makubwa katika oparesheni zao za pale Iraq.
Kisanga hiki kinahusu vifo vya Wairaq 17 huku wengine 20 wakijeruhiswa vibaya kwa kupigwa risasi mchana na hadharani kabisa na Wanajeshi wa Marekani ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa Balozi wa Marekani pale Iraq. Tukio hili lilitokea mwaka 2007 mwezi Septemba tarehe 16…
Inaendelea
Habib - 0718 096 811 (WhatsApp Only)
Sent using
Jamii Forums mobile app