Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,717
- Thread starter
- #961
Ndani ya hiyo hard drive kulikuwa na files kadhaa… lakini file ambalo liliwashitua wale wafanyakazi wa chuo kwa mujibu wa taarifa ya FBI, ni file ambalo lilikuwa limeandikwa "Ang_Confidential.pdf."
Baada ya taarifa hiyo kuripotiwa, FBI waliweza kubaini kwamba hiyo hard drive inamilikiwa na mtu anayeitwa Simon Saw-Teong Ang.
Simon Saw-Teong ni Muhadhiri chuoni hapo Arkansas-Fayettiville na ni Profesa aliyebobea kwenye nyania ya Electrical Engineering.
FBI wanasema kwamba walipopekua hiyo hard drive wakakuta limehifadhi lundo la barua pepe ambazo mmiliki wa hiyo hard drive alikuwa akiwasiliana na mtu aliyeko nchi China.
FBI wanasema katika moja ya mfululizo wa barua pepe hizo Profesa Ang anamlalamika mtu huyo aliyeko China (ambaye inaaminika kuwa ndiye 'handler' wake) kwamba wanapaswa kubadili namna ya kuwasiliana na ufanyaji kazi wao kutokakana na upepo wa kisiasa kati ya China na Marekani kubadilika. Kwenye barua pepe hizo Profesa Ang anamwambia huyo mtu kwamba ana wasiwasi kwamba kama wasipokuwa makini kwenye protokali za mawasiliano na utendaji kazi wao yeye kibarua chake kinaweza kuota mbawa na anaweza kutupwa gerezani ikigundulika anashirikiana nao (China).
Hili likikuwa ni tukio kubwa kweli kweli na la hatari na kushitusha.
Sababu huyu Profesa Ang ana security clearance ya ngazi ya juu sababu licha ya kuwa muhadhiri hapo chuoni lakini pia ni moja ya wahandisi wa NASA.
Na huko nyuma nilishawahi kusema kwamba NASA licha ya kwamba wanajihusisha na masuala ya Sayansi ya Anga lakini iko kwenye fungu la sekta ya kijeshi (Advanced Wepons). Hivyo huwezi kufanya kazi NASA bila kuwa na Security Clearance.
Sasa, huyu Profesa Ang sio tu kwamba alikuwa anafanya kazi NASA bali alikuwa ni moja ya vichwa adhimu vya kutegemewa hapo NASA.
Kwa mfano kwa kipindi cha mwaka 2013 mpaka mwaka 2018 NASA walikuwa wamempatia Profesa Ang jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 12 (Dola milioni 5) kwa ajili ya kufanya tafiti mbali mbali.
Kwa hiyo, kubainika kwa huyu Profesa kwamba alikuwa na mahusiano ya siri ya kazi na China ilikuwa inatoa picha kwamba kuna tatizo kubwa kiasi gani na kiasi gani China alikuwa amejipenyeza kishushushu kwenye nyanja ya tafiti, gunduzi na sayansi ndani ya Marekani na nchi nyingine za magharibi.