SEHEMU YA KUMI
(Sehemu ya Nane na ya Tisa sijaziweka soma maelezo hapo chini)
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?*
#10
Muda ule ule ambao data za GPS zilikuwa zikionyesha kwamba Raymond Davis Allen alikuwa akitembelea maeneo ya Peshawar na FATA siku kadhaa baadae General Pasha naye alikuwa anasafiri kwenda Saudi Arabia.
Lakini pia katika kipindi hiki hiki cha safari za General Pasha kwenda Saudi Arabia ni muda huo pia Ufalme wa Saudia ulikuwa umetoa tenda kwa Booz Allen kuunda idara ya kufanana kabisa na NSA ya Marekani.
Kuna uhusiano na uwiano wa matukio haya..
Sasa,
Wapwa wamenikalia kooni... "bold hatuelewi".. Loh!!
Watu wengi mmekuwa mnanitumia ujumbe inbox kwamba mnatamani niende moja kwa moja kueleza nini kilitokea Wuhan Institute of Virology. Kwamba wengine wana hisi silengi shabaha pale panapotakiwa badala yake natungua maembe kwenye mbuyu.
Nahisi kuna watu hawajaelewa hata kichwa cha habari cha Makala hii.. "Deep State & Covid-19".
Kwenye sehemu hizi nilizoanza nazo dhamira yangu niwaonyeshe kwanza ni namna gani "Deep State" inafanya kazi kisha niwaonyeshe ni namna gani kuna dalili ya huu mlipuko wa Covid-19 ni karata yao muhimu. Lakini baadhi yetu naona wameshindwa kutanua misuli ya ubongo na limekuwa somo gumu sana kwao.
Nimekaa na kutafakari sana na kupata hitimisho sababu hoja hizi za wadau zimenikumbusha kitu kimoja hivi… niwape mfano maridhawa ambao hata wewe unaweza kukugusa binafsi.
Kipindi natoa tongotongo darasani moja ya wapo ya vitu ambavyo viliuteka moyo wangu kwa mahaba ilikuwa ni masuala ya 'quatumn mechanics'.
Moyo wangu ulitokea kutekwa na masuala yanayohusiana na quatumn mechanics sababu ni nyanja ambayo imejaa kiza kikubwa sana na siri ambazo bado hazivumbuliwa na wanafizikia. Nyanja iliyojaa siri ambazo bado zingali zinachunguzwa na wanafizikia mpaka sasa. Nyanja ambayo ina 'ideas' za kushangaza mno.
Moja wapo ya mada za kuvutia zaidi kwenye quatunn mechanics ni kitu kinaitwa "the observer effect".
Hii ni nadharia ambayo inafafanua kwamba unapoichunguza phenomenon (observable fact or event) unasababisha hiyo phenomenon ibadilike.
Kwa lugha nyingine ni kwamba phenomenon ina-behave tofauti inapokuwa yenyewe tofauti na inapikuwa observed.
Ili kuelewa nadharia hii huwa tunatafiti jaribio la kisayansi linaloitwa "double-slit experiment".
Yaani mfano chukua bati tambarare la urefu wa sentimita thelathini na upana wa sentimita ishirini alafu pale katikati kata tundu lenye urefu wa sentimita tano na upana wa sentimita moja. Kisha acha umbali wa sentimita tatu kata tundu lingine la ukubwa huo huo (urefu sentimita tano na upana sentimita moja).
Kwa hiyo hil bati lako litakuwa na matundu mawili (double slit).
Simamisha hilo bati alafu mbele yake kama nusu mita hivi weka ubao mkubwa.
Wanasayansi 'waka-shoot' goroli ndogo ndogo sana kwenye lile bati ambalo lina zile double slit.. gorili zilipopita kwenye yale matudu zikaenda kuganda kwenye ule ubao uliolo mbele na zikaganda kwa mpangilio wa mistari miwili kurandana na yale matundu mawili zilipopita.
Kisha watafiti waka-shoot "wave" kupita kwenye matundu haya. Lakini yalipotua kwenye ule ubao wa mbele ilitengeneza mistari mingi zaidi ya miwili. Hii ni kwa sababu kila 'single wave' ikipita kwenye yale matundu mawili inagawanyika na kutoa mawimbi mawili tofauti ambayo yakiendelea kusafiri kuelekea ubao ncha zake zina cancel each other na hivyo ile mistari mingi kwenye ubao ni point ambazo mawimbi yali-cancel each other.
Watafiti waka-shoot electron kupita kwenye yale matundu wakitegemea kwamba vikitua kwenye ubao ule wa mbele itatengeneza mistari mawili, lakini tofauti na matarajio kwenye ubao kukatokea mistari mingi kufanana na vile ambavyo ilitokea kwenye wave. Kwa nini?
Wakafunga vifaa maalumu kwenye chumba cha majaribio 'kuobserve' namna gani zile electron zinapita kwenye matundu ya bati.
Waka-shoot tena electrons… la haula electron zikatengeneza mistari miwili na sio mistari mingi kama ilivyofanya awali.
Watafiti wakaacha ku-observe… wakashoot tena electron… ikatengeneza mistari mingi kama wave kama mwanzoni. Wakarudia tena ku-observe, waka-shoot electron… zikaunda mistari miwili.
Watafiti walipigwa butwaa… kwamba hizi electron zina uwezo wa kufikiri kwamba sasa naangaliwa na hivyo zina-behave tofauti?
Jawabu pekee ambalo wakaja nalo ni kwamba wanapo-observe zile electron wana-cancel 'wave function' ya zile electron.
Lakini swali bado linakuja iweje 'mere observation' i-cancel wave function?
Hili swali na huu mjadala bado uko kwenye debate kubwa mpaka leo hii kwenye ulimwengu wa quatumn physics.
Lakini utafiti huu umetupatia moja ya theory muhimu sana kwenye quatumn physics… kwamba "the mere observation of a phenomenon inevitably changes that phenomenon". Na hii ndio twaita "the observer effect".
Mfano mwepesi kabisa ni kama vile unapotaka kuangalia pressure ya tairi yako ya gari. Kabla haujaweka kifaa cha kupima presha kwanza utafungua ile valve kwenye tairi. Ulifungua tu ile valve kwa sekunde chache upepo utatoka "pssssss". Maana yake mpaka unapima presha ya tairi tayari imeshabadilika kwa sekunde chache zile ulipofungua valve. Lakini kilichosababisha presha ibadilike ndani ya tairi ni ile hatua uliyochukua ya ku-observe.
Nadharia hii wengine wameenda nayo mbali zaidi kufasiri hata tabia ya binadamu… kwamba kwa nini binadamu akiwa peke yake ana-behave tofauti na akiwa mbele za watu.
Wewe wajua yawezekana ukijifungia peke yako chumbani unavyo jimwaya mwaya unacheza "simba baba lao" kama sio wewe lakini ukiwa ofisini ukimuona yule intern mwanafunzi wa chuo anasikiliza "baba lao" unamwambia mfanyakazi mwenzako "dogo ana mambo ya kitoto sana", utadhani sio wewe juzi chumbani ukiwa peke yako uliyekuwa unacheza 'shakushaku'.. Lol.!!
Observer effect. Kitu (phenomenon) kikiwa observed kinabadilika tofauti na kikiwa chenyewe.
Hali hii inatukuta hata sisi waandishi. Kuna muda kile kilichopo kichwani unachotamani kukieleza ni tofauti na kile ambacho unakiwasilisha kwa hadhira. Kuna muda you have these deep secrets lakini unahisi vijana wa kisarawe watakasirika hivyo ukiwasilisha unaficha ficha na kuzunguka mbuyu.
Kuna muda kuna mada wataka kuidadavua kwa umahiri mkubwa lakini unajua kuna watu watashindwa kuielewa hivyo unawasilisha kitu kwenye hali ya wepesi.
Kuna muda unalazimika ubadili kile unachotamani kukiandika ili watu wengi zaidi waweze kukielewa.
Nakumbuka mwaka jana hapa kwenye group nilikuwa nachambua chanzo cha mgogoro wa Rawanda na Uganda… ule mgogoro kwa sababu fulani naufahamu kiundani sana sana sana, actually nafahamu vitu ambavyo nahisi hata sipaswi kuvifahamu. Kuna siku nikiwa nachambua nikawa na-reveal identity ya mlinzi wa Ikulu ya Uganda ambaye alikuwa ni pandikizi la Paulo.. nikaweka nakala ya kitambulisho chake kinachompa access ya Ikulu kisha nikaweka na nyaraka nyingine ambazo zinamuhusu. Nikaweka na barua yenye muhuri wa siri ambayo Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa aliandika kwenda kwa Mzee M7 kuhusu utata wa identity za watu ndani ya Usalama wa Taifa Uganda.
Huko inbox kulikuwa kama mvua… hata ambao hawako kwenye group wakanifuata kuuliza hivyo vitu nimevipata wapi??
Matokeo yake ikabidi niimalize juu kwa juu ile mada.
Kile ambacho nilikuwa natamani moyoni mwangu nikiandike na kile nilichokiandika ilikuwa tofauti.
Observer effect. Kitu kinapokuwa observed kinabadilika tofauti na kikiwa chenyewe.
Kuna muda kama mwandishi unalazimika kupunguza ukali au uzito wa kitu ili kiweze kueleweka kwa 'umma' mkubwa zaidi.
Hivyo basi… kutokana na maombi ya wengi kwamba niende moja kwa moja kueleza nini kilitokea Wuhan Institute of Virology, nitafanya hivyo. Kwa hiyo sehemu ya Nane na ya Tisa sitazipost hapa kama ambavyo nimefanya kwa group la Whatsapp maana zote nafafanua zaidi lile tukio la Lahore Pakistan na Siku ile ya April 30. Sitaki kuwachanganya zaidi wale wenzetu wachache wanaolalama hawaelewi.
Kwa sasa niitaandika kwa undani kabisa nini kilitokea pale WIV. Nitakatisha kwa sasa hizi dots ambazo nilikuwa naziunga.
Najua mko wale amnao mliluwa mnanielewa kuhusu dots ambazo nilikuwa naziunga na mlikuwa mna-enjoy mtiririko ule... mniwie radhi kidogo... nipeni siku hizi chache nimalozane na 'umma' alafu nitakachofanya naimaliza hii haraka kisha naaza makala mpya ambayo exclusively itahusu "Deep State" pekee na namna gani inafanya kazi. Kwa wale ambao hawawezi kusoma mambo magumu, wale waliokuwa wanalalama kwamba mbona hawaelewi… naomba makala hiyo mpya nikiianza msiiguse kuisoma maana hamta elewa kabisa hata chembe, hata robo hamtaelewa.
Hivyo basi nitaandika sehemu hizi za mwisho ziwe inclusive tusimuache mtu nyuma… nawapandisha roketi tunaenda moja kwa moja kutua Msamvu. Kisha nikimaliza wale wenzangu tunaoweza kutafuna mambo magumu nitaanda makala maalumu kwa ajili yetu, nitawapandiasha gari twende kitu kwa kituo… tutoke Ubungo, kisha tuingie Maili Moja, Mlandizi, Ruvu alafu tufike Chalinze tununue mananasi, kisha Mdaula, Mwidu, Mikese, Nanenane alafu ndio tuingie Msamvu.
Now, let's do this… twende Wuhan.
Sasa,
Nimeeleza pale mwanzoni kabisa namna ambavyo Wuhan Institute of Virology ilipandishwa hadhi toka BSL-2 kwenda BSL-4 ambayo inakuwa na uwezo wa kuunda na kutafiti biological agents mpya ambazo hazijulikani kwenye ulimwengu wa baiolojia na kwa maana hiyo hazina tiba au chanjo.
Sasa, kwa miezi miwili iliyopita kama umefuatilia vyombo vya habari umeona namba gani vyombo vya habari vimekuwa vinatumia nguvu kubwa kukanusha madai ya Rais Trump ambayo pia yalitiliwa mkazo na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo kwamba kuna dalili kwamba virusi vya Covid-19 vimevuja kutoka maabara ya Wuhan Institute of Virology eidha kwa bahati mbaya au kwa makusudi.
Jambo la msingi au swali ambalo watu wengi nahisi hawajiulizi ni kwa nini Rais wa Marekani na Waziri wa mambo ya nje wamefikia hatua hii kutoa maoni ya namna hii hadharani. Ni nini hasa wamekiona?
Ni kwamba..
Mwaka jana kabla hata ya mlipuko wa balaa hili la Covid-19, kabla hata ya mgonjwa wa kqanza wa Covid-19 kuwepo, Wizara ya Ulinzi ya Marekani yaani DOD, walitoa tenda maalumu kwa moja ya kampuni wanaofanya nao kazi (contractor) inayoitwa Sierra Nevada Corporation kwa ajili ya kuchunguza mwenendo wa Wuhan Institute of Virology baada ya onyo ambalo lilitolewa na mtaalamu wa biochemistry Dr. Richard H. Ebright.
Kampuni hii ya Sierra Nevada Corporation ndani yake ina subsidiary inayoitwa MACE (Multi Agency Collaboration Enviroment) ambacho kitengo hiki hasa wakakabidhiwa jukumu hilo toka Wizara ya Ulinzi.
(Wale wapwa zangu wa "bold hatukuelewi" mngeniacha niendelee na ule utangulizi mngeelewa kwa nini ni kampuni hii ilipewa tenda hii na kuna significance gani kwa wao kupewa hii tenda na kwa nini Wizara ya Ulinzi Marekani hawakuwapa jukumu hili idara za intelijensia kama CIA. Roho inaniuma maana mnanilazimisha niwalishe ugali bila mboga maana baadhi hawana uvumilivu wa kusubiri masaa mawili 'maharagwe yaive'. Anyways, tutaenda hivyo hivyo)
Kazi hii walikuwa wamepewa baada ya DOD kuona kuna mienendo isiyo ya kawaida ndani ya WIV.
Kwa mfano kwa muda wa siku kadhaa DOD walikuwa na intelijensia kwamba kumekuwa na 'traffick' isiyo ya kawaida ya wataalamu kutoka nchini Singapore chuo kikuu cha DUKE-NUS Medical School kwenda WIV. Moja wapo ya wataalamu hawa kutoka Singapore ambaye uwepo wake hapo Wuhan Institute of Virology haukuwa wa kawaida alikuwa ni Dr. Lifa Wang ambaye ni msomi Shahada ya Uzamivu na Mkurugenzi wa Programu ya Emerging Diseases katika chuo kikuu cha Duke-Nus kule Singapore.
Nitawaeleza baadae kwa nini uwepo wake hapa WIV haukuwa wa kawaida.
Hivyo basi, kwenye hii kazi ambayo DOD waliwapa huyu contractor Sierra Nevada Corporation kuna mwongozo mahususi kabisa ambao walikuwa wanataka waufuate.
Kwanza DOD walitaka Sierra Nevada wafanye uchambuzi yakinifu wa 'telemetary data' ya Wuhan Institute of Virology na maeneo ambayo yanayazunguka. Nitafafanua.
Pia waliwataka watazame 'traffic patterns' ndani ya WIV pamoja na kufanya 'Life Analysis'… vitu vitatu ambavyo DOD waliamini vinaweza kuwapa fasiri ya nini hasa ambacho kilikuwa kinaendelea ndani ya kituo cha WIV.
Kama ambavyo nimeeleza tenda hii ilitolewa kwa Sierra Nevada Corporation ambao wao nao wakaitoa kwa subsidiary yao inayoitwa MACE.
Ni muhimu kukumbuka kwamba kazi hii ilikuwa inafanyika mwaka jana mwezi wa kumi kabla hata ya mlipuko wa Covid-19 na kabla hata ya kuwepo hata kwa mgonjwa wa kwanza wa Covid-19. (Unaweza kutazama kutangazwa kwa tenda hii kwenye tovuti ya DOD).
Kama ambavyo nimeahidi..nataka nimalize hii haraka ili sisi wengine turejee kwa kuanza makala mpya kudadavua "Deep State" na namna inavyofanya kazi.
Hivyo kuanzia sehemu hii mpaka sehemu ya mwisho kwa makala hii nitachambua kuhusu "Wuhan" na maudhui yote ambayo niliyandaa ndani yale kuhusu Deep State nitayaondoa.
Naamini nitakuwa nimeeleweka.
So stay here…
Habib
To Infinity and Beyond
Sent using
Jamii Forums mobile app