SEHEMU YA TANO
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#5
Here we go… take notes.
Nilikuwa naongea kuhusu Booz Allen.
Nichomekee kitu kidogo kabla sijaendelea.. kidogo tu kama haya moja au mbili.
Twaona kinachoendelea duniani.?
Mmeona habari habari iliyotikisa mwanzoni mwa wiki tuliyoimaliza, kuhusu Marekani kusitisha funding kwa kituo cha utafiti cha Wuhan Institute of Virology? Yes WIV ambayo nimeiandika mwanzoni kabisa kwa makala hii.
Unahisi kwa nini Marekani wamesitisha ufadhili kwa kituo hicho cha utafiti? Umejiuliza hilo swali? Umeona kile ambacho najaribu kuandika kwenye makala hii??
Na je, umeona kwenye ukurasa wa twitter wa bilionea Elon Musk ambavyo anafoka kuhusu "ufedhuli" unafanywa na watu fulani nyuma ya pazia kwa mgongo wa hii COVID-19?? Hebu tembelea ukurasa wake utazame… karibia siku ya tatu leo yuko kwenye 'rant' kuhusu COVID-19.
Ukisoma wachangiaji kwenye 'posts' zake hizo wanamshambulia tu wakimuona kama mfanyabiashara mwenye hasira kwa biashara zake kusimama kutokana na hili sekeseke la COVID-19.
Lakini kitu kimoja watu wengi hawajui kuhusu Elon… watu wengi hawajui au tuseme hawajajisumbua kukifuatilia... Elon Musk ana tofauti moja kubwa sana na mabilionea wenzake wengi wakubwa. Kuna taarifa ambazo Elon Musk anaweza kuziona ambazo matajiri wenzake wengi hawawezi kuziona.
Kwa nini?
Nakumbuka mwaka juzi Elon alikuwa amehudhuria kongamano fulani hivi la vijana kutoka kila pembe ya dunia ambao ni manguli wa masuala ya teknolojia.
Alipomaliza kuwahutubia akatoa fursa ya wahudhuriaji kumuuliza maswali ya papo kwa papo.
Kuna dada mmoja kutoka Netherlands akamuuliza kwamba kwa nini kampuni yake ya SpaceX imekuwa ya kibaguzi mno sababu waajiriwa wake wote ni raia wa Kimarekani? Kwa nini hawatoi fursa kwa vijana wengine kutoka pande mbalimbali za dunia kufanya kazi kwente kampuni hiyo adhimu?
Wahudhuriaji walishangilia kweli kweli kwa swali hilo mwanana?
Elon Musk akampa jawabu ambalo sidhani kama kuna mtu alilitarajia maana ukumbi wote wa mikutano ukawa kimya ghafla kuonyesha mshangao wa jibu ambalo hawakulitegemea.
Elon akawaeleza kwamba nchini Marekani masuala ya urushaji roketi angani imewekwa kwenye sekta ya "Advanced Weapons Technology". Hivyo katika nyanja ya kiusalama kampuni ya SpaceX inawekwa kwenye kundi moja na makampuni ya masuala ya ulinzi na usalama na hivyo hawaruhusiwi kuajiri mtu ambaye si Mmarekani sababu wafanyakazi wao wote wanapaswa kuwa na 'security clearance'.
Nilipomsikia Elon anasema kauli hii nikajiuliza kama mfanyakazi wa kawaida tu wa SpaceX labda ni muhandisi au programmer anapswa kuwa na 'security clearance' ambayo kwa nchi kama Marekani itakuwa clearance level ya CU na kama labda ni muajiriwa wa wadhifa wa juu wa kampuni lazima watakuwa na walau PTP Clearance… sasa najiuliza je, Elon ambaye ndiye mmiliki wa kampuni ana 'clearance' ya ukubwa wa level gani. Maana huyu bwana anamiliki kampuni ya SolarCity ambayo inahusika na uzalishaji wa nishati lakini pia anamiliki Tesla ambao licha ya kutengeneza magari lakini pia wanatengeneza vifaa vya kuzalisha nishati (Solar Roofs)... kwa nchi ya Marekani ili aweze kuendesha biashara hizo za Nishati kwa 'large scale' kama ambavyo yeye anafanya ni lazima walau awe na L au Q Clearance sababu pale Marekani masuala ya nishati ni mambo ya Kiusalama.
Sasa jumlisha na kumiliki kampuni ya SpaceX ambayo kiusalama iko kwenye kundi la 'Advance Weapons Technology'.. jiulize huyu mtu clearance yake iko level gani? Ukiniuliza mimi kwa uzoefu nitakujibu kwamba huyu mtu security clearance yake sio chini ya SCI au walau TS.
Ninachojaribu kusema ni kwamba huyu mtu kutokana Clearance aliyonayo ana access ya taarifa ambazo mimi na wewe kamwe kwenye maisha yetu yote hatutawahi kuja kuzijua. Taarifa nyeti kabisa. Kuna vitu vingi sana anavijua ambao watu wanaoishi kwenye ulimwengu huu wa chai na sukari hawatakuja kuvijua kamwe ubaya ni kwamba hawezi kuvisema, sababu pale kama ni afisa Usalama basi kiapo chako pia kinagusia kutunza siri, na pale Marekani kama ni Raia wa kawaida hauko kwenye vyombo vya usalama na umepewa Security Clearance ni lazima usaini NDA.
Kwa hiyo ninapomuona Elon anafoka mtandaoni kwamba Uhuru wa dunia "unabakwa"… kwamba kuna vitu viko nyuma ya pazia… ninapoona anafoka namna hii inatakiwa kuamsha hari ndani yetu na kusugua mbongo ili walau tujue hata punje tu anachojaribu kukisema kwa mafumbo.
Nahitaji haswa kuongeza kasi ya hii makala maana kuna vitu vingi sana vinatokea sasa hivi ambabyo wiki moja au mbili nyuma nilitaka kuwaeleza humu kabla hata havijatokea.
Wiki hii pale Marekani kwenye nyanja ya masuala ya usalama habari kubwa zaidi ambayo ilikuwa imeshika kasi ni kurejeshwa mahakamani kwa Generali Flynn. A three Stars General ambaye alikuwa ni mshauri wa Rais wa masuala ya Usalama wa Taifa (National Security Advisor).
Wiki moja iliyopita nilitaka kubashiri kutokea kwa jambo hili na nilipata hisia kwamba jambo hili litatokea baada ya kuona James Comey (Mkurugenzi wa FBI aliyefukuzwa mwaka juzi) amerusha mtandaoni picha fulani hivi… picha yenyewe huwa naiwekaga sana hata humu kwenye group nikipost baadhi ya Episode za Simulizi ya Vipepeo Weusi. Picha fulani ya mtu anatembea yuko kwenye korido nyefu yenye giza. Picha fulani ya black and white. Kama unasomaga Simulizi yangu ya Vipepeo Weusi basi utakuwa umeshaijua ni picha gani naiongelea.
Wiki moja iliyopita James Comey akaweka picha hiyo kwenye mtandao (bado ipo unaweza kwenda kuiona kwenye ukurasa wake). Alafu akaandika Good day for a walk (with household member).
Ukisoma maoni ya watu pale chini kwenye ukurasa wake watu wanamuuliza ana maana gani mbona haeleweki.
Of course haeleweki sababu haupaswi kuelewa… kwa asilimia tisini siku ile nilipoiona niliamini kabisa Shushushu huyu kuna ujumbe anajaribu kuwasiliana na watu fulani mahususi. Sijui ni akina nani au ujumbe ule alioandika ulikuwa unahusu nini… lakini niliamini kabisa kuna 'move' inafanyika juu ya General Flynn. Kwa nini? Ile picha ina stori fulani hivi behind it.. ndio maana binafsi huwa napenda kuitumia. Stori hiyo iliyo nyuma ya ile picha kuna vitu kadhaa vina shabihiana na skandali ya General Flynn mwaka 2017. So I knew, precisely kwamba kuna kitu kinatokea kwa General Flynn japo sikujua ni nini hasa kitafanyika, lakini nilihisi ni suala kuhusi Flynn. And Boom.. wiki mbili baadae (yaani wiki hii) tunaambiwa kuna dalili ya General Flynn kuachiwa huru baada ya kesi yake kurudishwa mahakamani.
Is it a coincidence? Absoulutely not…hizo ndio nawaambia, ni "Deep Events".
Natamani ningewaambia hili wiki moja iliyopita ili mpate pia ule mshawasha wa udadisi ambao ulinikuta wiki hii.
Huko mbeleni labda nitaeleza kwa undani nini nini kimetokea kwa General Flynn na namna gani kinahusiana na Deep State. Maana nimedhamiria haswa nieleza kwa urefu na upana namna gani hii kitu inaitwa "Deep State" inafanya kazi na namba gani wana ratibu matukio muhimu yanayoibadili dunia ambayo tunataita "Deep Events".
Najua.. inawezekana sieleweki kwenye utangulizo huu wa leo maana nimegandamiza masuala kadhaa kwa pamoja nga nga nga nga.!!
Niko overexcited, nina vitu kama elfu mbili kuhusu hiki ninachoandika alafu nahisi vinaflow kwa pamoja kichwani.. Loh!!
Let's slow down a little bit..
Nilikuwa nawaeleza siku ile ya White House Correspondents Dinner nini kilitokea kuhusu ile PIN iliyopotezwa na mfanyakazi wa Ikulu na kupelekea kubadilishwa kwa maafisa usalama wote wa kumlinda Rais. Zile sura mpya katika security detail ya Rais walikuwa akina nani?
Tukamaliza kwa kitendawili cha Booz Allen. Kwa nini Wakurugenzi wa Intelijensia ya nchi wote wa wili, ambaye alikuwa anatoka John McConell na yule aliyeingia James Clapper wote wawili walikuwa wanatokea kampuni ya Bozz Allen.
Sasa,
Pale Marekani kuna karibia watu wapatao 874,000 (laki nane elfu sabini na nne) ambao si watumishi wa serikali lakini wana Security Clearance. Idadi hii ni kubwa kuzidi watumishi wa kawaida serikali wenye security clearance ambao hawako kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama.
Yaani kwamba ukiondoa waajiriwa wa serikali ambao wako kwenye vyombo vya ulinzi na Usalama (Majeshi, Idara za Intelijensia n.k) ukajumlisha watumishi wengine wote wa serikali wenye security clearance hawafikii idadi hii ya watu laki nane na ushee ambao ni watu kutoka makampuni binafsi wenye security clearance.
Watu hawa zaidi ya Laki nane wengi wao ni waajiriwa wa 'private contractors' wa serikali ya Marekani.
Nataka uone 'magnitude' ya uhusika wa kampuni binafsi katika ufanyikaji wa mambi nyeti mno.
Sasa, hawa Booz Allen pekee wao wana waajiriwa wapatao 1,500 ambao wana TS au SCI clearance. Hizi TS na SCI ndio ngazi za juu kabisa za Security Clearance mtu anaweza kupewa pale Marekani.
Sasa inakuwaje kampuni moja binafsi na kiraia wawe na wafanyakazi wengi namna hii wenye Clearance ya juu kabisa?
Turudi pale kwenye tukio la Correspndents Dinner.
Baada ya kupotea kwa ile PIN kutoka kwa mfanyakazi wa Ikulu muda mchache kabla ya Rais Obama kuhudhuria hafla hii ya chakula, tukio lile likachukuliwa kama 'breach' na kwamba kwa siku hiyo Secret Service ilikuwa 'compromised' kuweza kuweza kumlinda Rais.
Nilisema pale nyuma kwamba suluhisho sahihi kabisa ambalo walikuwa wanatakiwa kulifanya ni kibadili kila kitu, maafisa, procedures, protocols n.k. Lakini kutokana na ufinyu wa muda hilo lilikuwa haliwezekani kufanyika.
Kikafanyika nini?
Nilisema kwamba kikafanyika kitu ambacho hakikuwahi kufanyika kabla japo Rais Nixon aliwahi kujaribu kukifanya kwa ngazi fulani mwaka 1985 lakini si kwa kiwango cha mwaka ule 2011.
Zile sura mpya unazoziona kwenye picha ile ya Obama ya mwaka 2011.. wale walinzi ni makomando kutoka kampuni binafsi inaitwa Triple Canopy. Yes, zile sura mpya unazozioana si maafisa wa Secret Services… ni makomando wa Kampuni binafsi inaitwa Triple Canopy.
Kama unaelewa masuala haya lazima utasema kwamba hiyo haiwezekani… haiwezekani ulinzi wa Rais ukawekwa mikononi mwa kampuni binafsi. Ni sahihi kabisa. Haiwezekani… haiwezekani ulinzi wa Rais ukawekwa mikononi mwa watu binafsi. Na ni sheria kabisa.
Pale Marekani Rais hana uwezo hata wa kukataa kupewa ulinzi. Yani suala la yeye kulindwa si hiari bali ni lazima kwa sababu ya Usalama wa nchi na uchumi. Endapo kama ikitokea kwa sababu fulani Rais anakataa kupewa ulinzi, Secret Service wana uwezo wa ku-invoke vifungu fulani vya kisheria ambavyo vinawaruhusu 'kum-detain' Rais kinyume na matakwa yake kwa ajili ya usalama wake.
Maisha ya Rais, Makamu wa Rais na familia zao yamewekwa kwenye mikono ya Secret Services kisheria. Hata inapotokea labda Rais anatembelea mahala fulani na Secret Service wanahitaji nguvu ya nyongeza labda ya Delta Units toka jeshini… mara nyingi makomando hao toka jeshini wanawekwa kwenye 'outer perimeter' ya Ulinzi. Siku zote… mara zote, inner perimeter iko mikononi mwa Secret Service, na ni sheria.
Sasa inakuwaje sio maafisa wa jeshi… au FBI au Navy SEALs… bali makomando wa Kampuni binafsi wakapewa jukumu lisilowezekana la kumlinda Rais siku ile ya April 30, 2011.?
Usisahau… nilisema kuna jambo kubwa zaidi lilikuwa linaendelea nyuma ya pazia. Jambo ambalo hata wewe unalifahamu. Lakini kwa wakati ule, yaani siku ile, ilikuwa pengine ni siri kuu zaidi kuliko siri yoyoye..
Sasa, hii kampuni ya Tripple Canopy inamilikiwa na kampuni mama inayoitwa Constellis Group…
Inaendelea….
Habib - 0718 096 811
Sent using
Jamii Forums mobile app