Taarifa zote hizi Marekani hawakuwa wanazijua mpaka Dr. Ye alipotoroka kurejea China.
Kwa miaka yote miwili ambayo alikuwa akiishi Marekani walikuwa wanamchukulia kama mtafiti tu na mwanasayansi pasipo kujua kwamba ni Dr. Ye alikuwa ni jasusi mbobezi kabisa.
Huyu Dr. Ye akiwa Marekani aliwahi kuhusika kwenye miradi kadhaa ya siri ya kisayansi, hivyo alikuwa na 'access' ya data nyingi za siri za jeshi na miradi ya kiusalama ya kibaolojia.
Uchunguzi wa FBI umebaini kwamba Dr. Ye akiwa Marekani alikuwa anatuma taarifa hizi za siri kwenda kwa mwanasayansi ambaye yuko china kwenye kile chuo chao cha teknolojia za Ulinzi (NUDT). Mwanasayansi huyu ambaye Dr. Ye alikuwa akiwasiliana naye pia naye licha yankuwa mwanasayani ni Kanali kwenye jeshi la China.
Mtu huyo inaelezwa kwamba pia alimuagiza Dr. Ye kuwachunguza wanasayansi nguli wawili wa Kimarekani pamoja na tafiti ambazo wanazifanya (FBI mpaka sasa haijataja majina ya wanasayani hao wawili).
FBI pia wakadukua jumbe za mawasiliano ya simu kwa mtandao wa WeChat ("whatsapp" ya China) ya Dr. Ye na walishitushwa kukuta kwamba yeye pamoja na wanasayansi wengine kadhaa kutoka NUDT walikuwa wanaandaa 'research paper' kuhusu 'risk assessment model' mahususi kwa ajili ya mradi wa kibaolojia wa kijeshi.
Huyu ni Dr. Ye, mwanasayansi wa pili ambaye alinaswa na nyavu za FBI.
Mwanasayansi wa tatu kunaswa ndiye yule Profesa Charles Lieber nguli wa kemia na nanoscience.
Uchunguzi wa FBI uligundua kwamba, Profesa Lieber alikuwa recruited kupitia programu ya Thousand Talents.
Baada ya kuingizwa kwenye programu hii, Prof. Lieber akawa anatumiwa na Wuhan University of Teknology (WUT) kama "strategist scientist".
FBI wakagundua kwamba, Taifa la China walikuwa wanamlipa Prof. Lieber kiasi cha Silingi milioni 120 kila mwezi (Dola elfu 50) kama "posho". Pia walikuwa wanampa nyongeza ya milioni 360 (doa 158,000) kwa mwaka, kama malipo ya "kujikimu". Juu ya hiyo, walikuwa wanamlipa shilingi bilioni 3.5 kila mwaka (dola 1.5 milioni) kwa ajili ya "tafiti".
Kwa taarifa ya FBI iliyotolewa mwezi uliopita, May wanasema kwamba bado kuna wanasayansi kadhaa wanawafuatilia nyendo zao.
Lakini mpaka sasa hawa niliowaeleza ndio wanasayansi muhimu zaidi waliokamatwa na FBI mwaka huu toka February mpaka sasa baada ya mlipuko wa Covid-19.
Sasa,
Jambo ambalo nataka ukumbuke ni kwamba uchunguzi na hatimaye ukamataji huu wa hawa wanasayansi chanzo chake ni ile cable ya kishushushu toka Ubalozi wa Marekani pale Beijing kwenda Washington wakitahadharisha serikali ya Marekani kwamba kuna uwezekano mkubwa wanasayansi wa Kituo cha Wuhan Institute of Virology wanafanya uhandisi vinasaba wa virusi ambavyo wamevitoa kwa popo mapangoni jimboni Yunnan.
Na muhimu zaidi ni kwamba walikuwa wanahisi kwa kasi na ufanisi ambao WIV walikuwa wanaenda nao, walikuwa wanapata msaada wa kitaalamu kwa siri toka kwa wanasayansi wengine walioko nje ya China.
Kwa hiyo kamata kamata hii ya wanasayansi, na ushahidi ambao FBI wameuweka hadharani, hivi viwili vina-confirm wasiwasi ambao Ubalozi wa Marekani walikuwa nao… kwamba kuna "kitu" kilikuwa kinaundwa pale WIV.
Kama ambavyo nilisema mwanzoni kabisa mwa makala hii… kwamba binafsi huwa sipendi ku-conclude jambo, napenda mijadala. Kwa hiyo lengo la mimi kuandika andishi hili sio kusema kwamba janga hili la Covid-19 kasababisha fulani, kwa sababu hakuna mtu ambaye ana uwezo wa kuthibitisha kwa asilimia mia moja kwamba fulani kasababisha janga hili, au janga hili limetokea kwa sababu hii au ile.
Tunachoweza kufanya ni kutazama mazingira ya namna ambavyo jambo limetokea, kisha tukakusanya ushaidi, vidhibiti na vielelezo. Vidhibiti hivi vitusaidie kunoa mbongo na kujenga hoja kuhusu yale ambayo hayasemwi kuhusi janga hili. Kisha wewe binafsi ufanye hitimisho, kwa kadiri ambavyo mjadala umekwenda.
Kuna maswali kadhaa yanahitaji majibu… mfano ile device iliyoonekana Kenya, Dubai na China ilikuwa ya nani na alikuwa anafanya nini kwenye nchi hizo?
Jawabu ni kwamba, devide ile ilikuwa inamilikiwa na mtu anayeitwa Linfa Wang, msomi wa PhD toka chuo Kikuu cha Duke-NUS nchini Singapore ambako pia kwenye hicho chuo yeye ni Mkurugenzi wa Programu/Idara "Emerging Infectious Diseases".
Kuna ushahidi mpaka wa tiketi za ndege na risiti za hoteli akiwa kwenye nchi hizo nilizozitaja na baadae mwezi wa kumi kuibukia pale China Wuhan Institute of Virology.
Swali la, alikuwa anafanya nini kwenye nchi hizo, naomba nijaribu kulijibu kwenye makala mahususi ya Deep State.
Swali lingine la msingi sana ambalo lazima kila mtu anajiuliza ni kwamba… kama kirusi cha Covid-19 kilitengenezwa pale WIV, je, kilivujishwa makusudi au kilivuja kwa bahati mbaya?
Na kama kilivujishwa kwa makusudi ni nani alikivujisha?
Na lengo la kukivujisha ni nini?
Majawabu ya maswali haya ndio sababu kwa nini mwanzoni mwa makala hii niliongea viti vingi sana… nikaeleza matukio huko Pakistan, Afghanistan, Marekani na kadhalika. Matukio yale yalikuwa yanajibu maswali haya.
Ila kama ambavyo tulikubaliana ni kwamba ni vyema wote tuvuke mto kwa mtumbwi mmoja, kila mtu tumbebe. Kwamba nieleze specifically nini kilitokea pale Wuhan Institute of Virology.
Na naamini hilo deni nimelilipa.!! Nimeeleza kwa undani kabisa nini kilitokea pale WIV. Nikiingia ndani zaidi ya hapo, kuna wapwa zangu watasema nawavuruga, hawanielewi.
Kwa hiyo..
Masuala mengine yote, na majawabu ya maswali niliyoyaweka hapo juu, tafadhali usikose kuisoma makala hiyo mahususi kuhusu Deep State.
Kwa hili suala la Covid-19 na kilichotokea pale Wuhan Institute of Virology, mpaka kufika hapa naomba nihitimishe.
Kesho twaanza makala mpya.
Pia kwa wale wafuatiliaji wa VIPEPEO WEUSI na SHAH TAZAMON tuna-resume kuanzia kesho maana nilizisimamisha tumalizane na hii Covid-19.
Niwatakie mchana mwema, tukutane kesho kwenye makala mpya.
Shukrani.
Habib B. Anga "The Bold"
To Infinity and Beyond