COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

Kwa lugha nyingine, maabara zilizo kundi la BSL-4 wanatafiti na kuunda biological agents mpya (bacteri, virusi vipya) vinavyoweza kutumika kama silaha lakini kutokana na upya wake bacteria au virusi hivyo havina chanjo au tiba na huwezi kudhibiti.

Kaka naendelea kusoma vyema makala yako na huku nikiwa natafakari.

Inawezekana vipi katika hali halisi mtu utengeneze kitu kisha ushindwe kukimudu ? Hapa napataka gagaiko.

Pili, tunaambiwa Virus sio hai, lakini tunajiuliza kitu kinachoenea kupitia njia fulani vipi kisiwe hai huku kima athiri ?

Tatu, umesema ya kuwa Bacteria nao wanaundwa (Wanatengenezwa), ila kwao wao wanasayansi husema Bactria ni living organism au living things, kwa maana ni hai, uhai unapatikana wapi ? Yaani sawa sawa leo hii mtu atuambie amemtengeneza mbwa na kuwa hai.

Hili limekaaje, naomba msaada wa maelezo juu ya utengenezwaji wa viwili hivi, au kwao wao Wanasayansi wanamaanisha nini wanaposema "Wametengeneza" kitu fulani. Ila sharti la kitu kiwe kimetengenezwa, lazima kitanguliwe na kutokuwepo kwake kisha ndio kije kuwepo.

Naendelea kusoma makala yako.

Ahsante.
 
Mkuu naomba usinisahau kwenye taglist yako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi mwenyewe sielewi nasikia watu wanasema hali mbaya sana,lakini huku mitaani mambo mwake tu yanaendelea kama kawaida
 
SEHEMU YA PILI


DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani.!?




#2


Jana niligusia kuhusu maabara ya Wuhan Institute of Virology - WIV inayoongozwa na mwanamama msomi wa Kichina na mwanasiasa Dr. Wanga Yanyi, nikaeleza kuhusu kupanuliwa kwake na kisha kupandishwa hadhi toka BSL-2 mpaka BSL-4 ambayo ndiyo daraja la juu kabisa la kiusalama kwenye maabara zenye kuhusika na urutubishaji, uundaji na utumiaji wa biological agents.
Kisha nikaanza kueleza kuhusu tukio fulani lililotokea mwaka 2011 nchini Pakistan jimboni Lahore.

Sasa,


Wakati yule Mmarekani aliyekamatwa kwa tuhuma za kuua Wapakistani wawili akiwa anahojiwa na Polisi, kitengo kingine kilikuwa kinafuatilia mawasiliano yake katika simu ambayo walimkuta nayo. Simu ile ile ambayo ndani yake zilikutwa picha za maeneo ya siri ya kijeshi yaliyoko mpakani mwa Pakistan na India.
Katika kuchunguza mawasiliano ya simu ya Raymond Allen polisi wakagundua kwamba aliwasiliana na simu nyingine ambayo ilikuwa maeneo ya barabara maarudu hapo Lahore inayoitwa Jail Road.
Ubaya ni kwamba siku ile ambapo Raymond anapata mkasa kwenye makutano ya barabara Qurtaba eneo hilo lingine ambalo kuna mtu alimpigia simu, yaani Jail Road nako kulikuwa kuna mkasa mwingine wa ajabu sana ulikuwa unatokea.

Watu walioshuhudia tukio hilo lingine hapo Jail Road walidai kwamba ilitokea gari aina ya Toyota Land Cruiser ndani yake kukiwa na wanume wanne wenye asili ya kizungu ambayo ilikuwa inaendeshwa kwa kasi mno huku ikifanya 'overtake' za hatari kabisa. Bahati mbaya barabara hii Jail Road huwa kwa kawaida ina foleni kubwa.
Mashuhuda wanasema kwamba baada ya gari hiyo kukwamba kwenye foleni, dereva aliitoa gari kwenye upande anaopaswa kuwa na kuanza kuendesha kwa kasi ile ile upande mwingine dhidi ya magari yanayokuja mbele.
Mashuhuda wanadai kwamba ilikuwa ni kama wanaangalia filamu kwa namna ambavyo dereva alikuwa akiendesha kwa kasi huku akikwepa magari ambayo yalikuwa yanakuja mbele yao.

Ikatokea kwamba wakati gari hii Land Cruiser ikiendeshwa hivi kwa kasi kwenye 'saiti' ambayo sio yao, kulitokea pikipiki ambayo yenyewe ikawa inakuja kwa kasi sana mbele yao. Gari ikashindwa kukwepa pikipiki hii na wakagonga vibaya sana kiasi kwamba pikipiki na dereva wake wakatupwa nje kabisa ya barabara.
Ajabu ni kwamba gari hiyo haikusimama bali iliendelea na safari kwa mwendo ule ule wa kasi na upande ule ule wa barabara ambao hawakupaswa kuwa wanaendesha.


Sasa, awali polisi walisikia kuhusu mkasa huu lakini hakukuwa na hisia yoyoye kwamba labda pengine matukio haya yalikuwa yanahusiana.
Lakini baada ya ripoti ya wataalamu wao wa teknohama kugundua kwamba Raymond muda ule ule ambao alikuwa anapiga watu risasi aliwasiliana na mtu kwa simu ya mkononi simu ambayo ilikwenda kwenye namba ya simu ya mtumiaji ambaye alikuwa maeneo ya Jail Road hapo ambapo pia nako walisikia kuhusu tukio lile la gari kuendeshwa kana kwamba kwenye filamu wakaanza kuhisi pengine kulikuwa na uhusiamino kati ya matukio haya mawili.
Lakini sababu ya pili ni vile barabara hiyo ya Jail Road ukiifuata inakwenda kutokea moja kwa moja pale makutano ya barabara ya Qurtaba ambako kulitokea tukio la Raymond kupiga Wapakistani wawili risasi.
Lakini sababu ya tatu ambayo ilikuwa ya kushangaza zaidi ni kwamba kwa kutumia camera za usalama mtaani polisi walifanikiwa kupata namba za ile Land Cruiser ambapo ilionekana kwamba imesajiliwa kwa namba LZN-6970. Lakini walipofuatilia namba hizi wakang'amua kwamba zilikuwa za bandia sababu namba hizo zilikuwa zimesajiliwa jimboni Punjab kwa jina la mtu anayeitwa Sufi Munawwar Hussain.

Wasiwasi wa Polisi kituo kikuu hapo Lahore ukaongezeka zaidi juu ya huyu mtu ambaye majina yake kwenye kitambulisho yalionyesha anaitwa Raymond.


Kuna majina matatu ambayo ni muhimu sana kuyakumbuka kadiri ambavyo tunaendelea na andishi hili.
Wale Wapikistani wawili ambao Raymond aliwapiga risasi mmoja alikuwa anaitwa Faizan Haider, ambaye alikuwa na miaka 22 na yule mwenzake alikuwa anaitwa Faheem Shamshad (pia alikuwa anajulikana kwa majina ya Muhammad Faheem) ambaye huyu alikuwa ni kijana wa miaka 26.
Yule jamaa aloyegongwa na Lad Cruiser pale Jail Road jina lake alokuwa anaitwa Ebadur Rehman (pia jina hili kwa ligha ya Urdu linatafsiri kama Ibad-ur-Rehman).

Yakumbuke majina haya matatu.


Juzi niliwaeleza kwamba katika kitambulisho ambacho Raymond alikutwa nacho kilionyesha kwamba alikuwa ni muajiriwa wa kampuni inayoitwa Hyperion Protective Consultants ambayo nilieleza kuwa hii ilikuwa ni shell Company ya kampuni mama ya Blackwaters Worldwide ambao nikasema hawa ni moja ya 'contractors' wakuu wa CIA.
Kuna jambo la msingi sana kulielewa kuhusu hawa Blackwaters Worldwide kabla sijaendelea mbele sana.


Kama umekuwa mfuatiliaji wa vita ya Iraq basi sina shaka utakuwa umewahi kusikia kisanga cha Nisour Square Massacre.
Kisanga hiki cha Nisour Square Massacre pengine ndio moja ya skandali kubwa ya kwanza kufanya Marekani wakosolewe vikali na hatimaye wafanye mabadiliko makubwa katika oparesheni zao za pale Iraq.
Kisanga hiki kinahusu vifo vya Wairaq 17 huku wengine 20 wakijeruhiswa vibaya kwa kupigwa risasi mchana na hadharani kabisa na Wanajeshi wa Marekani ambao walikuwa wanasindikiza msafara wa Balozi wa Marekani pale Iraq. Tukio hili lilitokea mwaka 2007 mwezi Septemba tarehe 16…


Inaendelea


Habib - 0718 096 811 (WhatsApp Only)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma comrade... tuko pamoja
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali mujarabu kabisa haya chief... nitarejea na majawabu kwa kirefu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Katika engineering technology yyt mkuu kuna mda tunatengeneza technology ambazo inafikia muda tunashindwa kujua zinafanyeje kazi na ikifikia hio hatua ndipo inakua ngumu kumudu. Mfano mzuri na rahisi ni swala la Artificial intelligence. Wiki juzi nlitengeneza game la karata lkn ikafikia hatua BOT nloitengeneza mm inanifunga kwa tricks ambazo hata sikuifundisha nikaona huo ni ujinga, then nikaamua kuanza upya na kutumia njia tofauti ambayo itafanya BOT asiwe na uwezo mkubwa sana.

Hivyo hivyo ni kwenye field ya microbiology engineering, wanasayansi wanaweza kuinduce mutations kwenye genome fln ili wapate kiumbe tofauti. Sasa ikitokea mutations zikafanyika randomly kinaweza kutokea kiumbe cha ajabu ambacho hata wao wakashindwa kukicontrol. So inawezekana kabisa kutengeneza kitu ambacho ukashindwa ww kukimudu.

Pili umeongelea uhai wa virusi na usambazaji wake. Virusi vikiwa nje ya mwili wa binadamu vinakua sio viumbe hai bali ni chembe chembe tu. Sasa vikiwa nje inategemea structural characteristics zake. Kama ni particles kama za vumbi basi zitaweza sambaa kwa kupeperusha, kugusana etc.. Lakini kama zina nywelenywele(flagella) zinaweza kusambazwa kwa vimiminika etc..
Vikiishaingia kwenye mwili wa binadamu ndo vinatumia RNA kutoka kwa binadamu ili kudevelop(japo hii inategemea aina ya kirusi lkn mfano wa kirusi kinachotumia RNA ya binadamu ni HIV)

NOTE:virusi vingi vinakua na RNA(single stranded) tu lkn ili viwe viumbe hai inabidi viwe na DNA(double stranded) so vikiingia kwa binadamu ndo vinaenda kwenye cell na kutumia RNA ya kwenye cell ya binadamu na hii huifanya cell ibehave tofauti(ndipo ugonjwa unapoanzia hapa)

Tatu umeongelea uhai wa bacteria zinazotengenezwa. Ukweli nibkwamba wanasayansi hawatengenezi uhai bali wanatumia DNA kutoka kwa vijidudu vingine na kuzifanyia some engineering kubadilisha mpangilio wa bases(or wanaweza fanya mutation) kisha wanapata kiumbe tofauti na kiumbe cha mwanzo. Japo wanasema cell is the basic unit of life lkn ukienda deep zaidi ni kwamba DNA ndio basic unit of life
 
Nimejiongalia sipo labda nisubirie selection yapili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…