COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

Ombi!Mkuu tusaidie kumonita post za mwendelezo 5,6,7 nk....Post zipo nyingi nashindwa kuzipata mkuu.
 
Nimevutiwa na huu uzi ila naomba kuelekezwa jinsi ya kufanya setting ya notification ili mdau akiweka uzi niweze pata taarifa[emoji1545]
kama una tumia App fanya ku subscribe tu huu uzi utakua unapokea tu notifications
 
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?





#16



Wanasayansi watatu wale walikamatwa pale Marekani wakihusishwa na programu ya "Thousands Talents" ya nchini China.

Profesa Zaosong Zheng Mtafiti na Muhadhiri wa chuo kikuu cha Harvard.
Wa pili ni Dr. Yanging Ye Muhadhiri na nguli wa Biomedical Engineering toka chuo kikuu cha Boston.
Na wa tatu ni huyo nguli ambaye nimemueleza pale juu, Profesa Charles Lieber Mkemia na Mtafiri toka chuo kikuu cha Harvard.


Kabla ya kukamatwa kwa wanasayansi hawa na kabla hata ya mlipuko wa maambukizi ya Covid-19, mwaka juzi, yaani 2018 Ubalozi wa Marekani jijini Beijing walituma cable kwa serikali yao kuwatahadarisha kuhusu masuala kadhaa ambayo yanaendelea ndani ya kituo cha Wuhan Institute of Virology.
Kipindi hicho ndio kituo WIV kilikuwa kina miezi michache tu toka kipandishwe hadhi kufikia ngazi ya BSL-4.
Kwa kuwa Marekani walikuwa wanatoa ufadhili kwa kituo hiki hivyo walikuwa pia wanawajibika kufahamu kwa undani kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Lengo la ufadhili wao kwa kituo hiki ilikuwa ni kuwapa uweshaji WIV ili waweze kutafiti aina mpya za virusi ambavyo vinaweza kutokea ili kama endapo itatokea mlipuko fulani huko mbeleni basi wanasayansi wawe na ufahamu na utaalamu wa kutosha kuweza kutengeneza tiba na chanjo dhidi ya kirusi hicho na hatimaye kukidhibiti.

Kwa hiyo Ubalozi wa Marekani pale China mwezi January mwaka 2018 walituma ujumbe maalumu wa wataalamu kwenda kutembelea kituo cha WIV.
Ujumbe huo uliongozwa na Bw. Jamison Fouss ambaye ni Cousul General wa Marekani pale Wuhan. Pamoja naye alikuwepo Bw. Rick Switzer, ambaye ni mwambata wa Ubalozi kwenye masuala ya mzingira, sayanasi, teknolojia na afya.

Ujumbe huu ulitembelea WIV mwezi January mwaka 2018 na hata ujio wao watu hao uliripotiwa kwenye tovuti ya kituo japo kwa sasa taarifa hiyo imefutwa kwenye tovuti japi bado iko 'archived' kwenye mtandao wa intaneti unaweza kuipata.

Baada ya ziara yao hii hao mabalozi wadogo na waambata wa masuala ya Sayansi na tiba ndipo Ubalozi wa Marekani Beijing wakatuma Cable yenye muhuri wa "Sensitive" ambayo kwenda Washington kueleza wasiwasi wao kuhusi kituo cha WIV.

Kwenye Cable hii Balozi alieleza kwamba ujumbe ambao ulitembelea kituo ch WIV wameona dalili kwamba si tu wanasayansi ndani ya kituo cha WIV wanatafiti virusi vipya vya corona toka kwenye jamii ya popo aina ya 'horseshoe' wanaopatikana mapangoni jimboni Yunnan, bali kuna uwezekano wanafanya uhandisi wa vinasaba (genetic engineering) ya virusi hivyo toka kwa hao popo waishio mapangoni.
Lakiki wasiwasi wao mkubwa zaidi ulikuwa ni kwamba wanasayansi wa kituo cha WIV wanapata msaada wa kitaalamu kwa siri toka nje ya China.
Kwa sababu kama wasiwasi wao huo ulikuwa sahihi (kwamba wanafanya uhandisi wa visababu wa Virusi vya Corona toka kwa popo aina ya 'horseshoe') ilikuwa ni ngumu kwa watafiti wa WIV wao pekee kuweza kufanya hizo synthesis na uhandisi wa vinasaba wa aina hiyo ya virusi sababu maabara yao haina wataalamu wa kutosha wenye uzoefu sababu ndio kwamba walikuwa wamepandishwa ngazi ya BSL-4.

Hivyo cable hii ndio ilikuwa chanzo cha vyombo vya usalama vya Marekani kuanza kuchunguza Wanasayansi ambao wanafadhiliwa chini Programu ya Thousands Talents.


Matunda ya Upelelezi huu ukaanza kupatikana mwaka jana 2019 mwezi July.
Pale Canada wana maabara moja tu yenye hadhi ya BSL-4.
Maabara hii inaitwa NML (National Microbiology Lab) iko kwenye mji mkuu wa jimbo la Manitoba mahala panaitwa Winnipeg.
 
Maabara hii inahifadhi na kufafiti baadhi ya virusi hatari zaidi duniani kama vile Ebola na Henipah (Nipah).

Mwaka jana mwezi huo July kulitokea Security breach hapo kwenye maabara NML nchini Canada.
Wiki chache baadae vyombo vya usalama walipata taarifa kwamba kuna maabara nchini China wamepokea shipment ya sampuli za virusi vya Ebola na Henipah.
Baada ya uchunguzi wakagundua kwamba sampuli hizo za virusi zilizotumwa China vimetokea hapo maabara ya NML nchini Canada.

Ikabidi ufanyika uchunguzi wa kina zaidi ambapo wakabaini kwamba wanandoa Bi. Qiu Xiangguo ambaye ni Virologist na mumewe Chen Keding ambaye ni biologist pamoja na mwanafunzi wao mmoja wa Phd kutoka nchini China walibainika kuhusika na tukio hilo la kuiba hizo sampuli na kuzituma nchini China (ambapo kwa namna yeyote sampuli hizo zilipelekwa Wuhan Institute of Virology sababu ndio mahala pekee wanapoweza kuhifadhi sampuli hatari ya namna hiyo kwakuwa WIV ndio maabara pekee nchini China yenye hadhi ya BSL-4).

Tukio hili lioishitua mno vyombo vya usalama sababu lilikuwa linarandana na tahadhari ambayo walikuwa wamepewa kwenye Cable kutoka ubalozi wa Marekani Beijing kwamba kuna uwezekano kituo cha WIV kinafanya uhandisi wa vinasaba vya virusi vya corona toka kwa aina ya popo 'horseshoe' waishio mapangoni jimboni Yunnan.

Tukio hili likiwa bado halijapoa linatokea tukio lingine la hatari zaidi.

Sijui kama bado wanaendelea mpaka sasa au la, lakini kuna kipindi pale Library chuoni Mzumbe walianzisha kitengo cha urejeshaji vitu ambavyo vimepotea.
Utamaduni huu wenzetu wa nchi za magharibi kwenye campus za vyuo vyao wanao miaka mingi… kwenye campus kunakuwa na kitengo kinachojulikana kwa jina maarufu la "Lost-and-found".
Mfano nimepoteza kitambulisho changu, ukikiokota unakiwasilisha hapo, na wao wanawasiliana nami.

Mwezi Septemba mwaka jana kwenye campus ya chuo kikuu cha Arkansas-Fayetteville nchini Marekani hapo mahala pa "Lost-and-Found" walipokea hard drive ya computer ambayo moja ya wanafunzi wao aliiokota.

Ili waweze kumfahamu mmiliki wa hard drive hiyo ilibidi waichomeke kwenye comoputer waone kilichomo ndani kama kinaweza kuwasaidia kufahamu nani mmiliki wake.
Walipoichomeka kwenye computer, kile ambacho walikikuta ndani yake kiliwafanya sio wawasiliane na mmiliki wake bali watoe taarifa kwenye vyombo vya usalama.
 
Dr. Qiu Xiangguo ndani ya maabara ya NML
Screenshot_20200623-131959_Gallery.jpeg
 
Back
Top Bottom