COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.

Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.

Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.

Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.

Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.

Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.

Paskali
PASKALI;
Vyuo vyote Tanzania vimeshafunguliwa tangu J3 wiki hii.
 
Kwenye darasa moja ninalofundisha, huwa nawaambia wanafunzi wangu "perception matters". Bahati mbaya au nzuri maamuzi mengi hufanyika kwa kutumia (based on) perceptions. Kwenye takwimu za COVID 19 inaelekea tumejikanyaga mahali na matokeo yake iwe kweli au la tunakuwa perceived kuwa tunatumia data za kupika na itachukua muda mrefu hadi tuje kuaminika.
Unaweza ukasema na ni haki yako kusema "Kama mpaka sasa update ya Corona kwa Tanzania ilitolewa mara ya mwisho tarehe 29 April wakati huo idadi ya vifo ni 16, na mpaka leo hakuna update hivyo idadi ya waliokufa kwa Corona Tanzania bara ni huo 16 tuu, na huu ndio ukweli wenyewe........(Pascal hapo juu)". Je ni nani anakuamini? Nasikia hatufi tena kwa COVID19 bali kwa matatizo ya kupumua (yakijumlisha pneumonia, asthma, etc).
Wiki hii tuliyonayo wametoa updates tuna wagonjwa wanne. Updates nyingi tu zimeshatolewa baada ya April 29. Una vitu vingi ofisini
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.

Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.

Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.

Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.

Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.

Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.

Pascal
Pascal ummy amesema tanzania ina wagonjwa 4 wenye corona, kiutalamu katika magonjwa ya kuambukiza hao watu wanne wanaweza kuambukiza zaidi ya watu 20 ndani ya masaa 24 kama hatua za kujikinga nao hazitachukuliwa. Hivyo kusema ugonjwa upo, wamarekani hawajakosea labda Ummy angesema hakuna mgonjwa wa corona Tanzania halafu wakaja wamarekani wakasema kwamba wagonjwa wapo, hapo tungesema wanatusingizia kwa kusema uwongo. Kwa taarifa za serikali yetu ugonjwa upo.
 
Wazungu hawajawahi kuongopa mjomba

Wamarekani hawana sababu ya kuongopa!! Kweli hao wagonjwa wanne wa covid 19 ndio wagonjwa wa nchi nzima waliobaki au ni wagonjwa waliopo hospital za serikali Dar es salaam? Kwasababu ukienda Aga khan na Hindu Mandal tu kule kwenye ICU zao hapo Dar ndio utabaini kama balozi wa marekani anaongopa au anasema kweli!!!

Wananchi hawawapeleki wagonjwa wao hospitali kwani kule hakuna huduma wamebakia kuwatibu wagonjwa wao nyumbani kwa NYUNGU na wakiitwa mbele ya haki wanawazika kimya kimya kwa heshima na sio kutupwa kama wafanyavyo serikalini!!
 
Hospitali ya Temeke hakuna Daktari anayeingia wodi ya wagonjwa wa corona
 
Wiki hii tuliyonayo wametoa updates tuna wagonjwa wanne. Updates nyingi tu zimeshatolewa baada ya April 29. Una vitu vingi ofisini
Mkuu hujatembea na uzi wangu. Hapo juu nilimkwoti Pascal lakini pointi yangu ni kuhusu perception. Ukieleweka vibaya ni vigumu watu kukuamini. Kwa kutoa data kutumia vigezo vyetu na sio vys kimataifa ndio kumeleta tatizo hili.
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.

Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.

Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.

Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.

Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.

Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.

Paskali

Kwa ufahamu wangu maambukizi ya ugonjwa wa korona yamepungua sana au watu waliaombukizwa hawaendi moja kwa moja hospitalini. Sababu inayosababisha watu wasiende hospital labda ni ufahamu tulio nao wa tiba mbadala kama limao, tangawizi, vitunguu swaumu, nyungu na kadhalika.

Pia wagonjwa waliokuwa wamelazwa wamepona kabisa ushaidi ninao kwani niko katika fani ya uuguzi na pia ni mtoa huduma. Kuna kitu kisichoongelewa nacho ni dawa ya asili kutoka madagascar imeleta matokeo makubwa sana pia dawa ya utafiti ya NIMR. Wengi wanachojua ni kuwa dawa ya asili kutoka madagascar ilikuja sample kwa ajili utafiti kama alivyosema kabudi, si kweli mzigo ulikuja wa maana na ndio umeleta matokeo haya tunayoyasikia. Nchi haiwezi kusema watu wamepona kwa dawa hiyo kwani bado haijadhibitishwa na WHO.
 
Hii hoja ya kijinga kila mwenye tope kichwani anaileta
Wewe ukitangaziwa wamekufa 200 itakusaidia nini? Utaenda kuwafufua?
Serikali imeshasema ugonjwa upo tuchukue tahadhari full stop
COVID ipo lakini sio ugonjwa special sana hadi tuutukuze. Kuna magonjwa mengi kila dakika yanaua watu wengi tu na maisha yanaendelea.
Kwenye hii COVID namuunga mkono raisi Magufuli
 
Kila mtu anajua Corona ipo sana Tz, watu wanaugua kimya kimya na kuzikana kimya kimya pia. Serikali ilichokifanya ni kusitisha kutoa taarifa rasmi (ili kuhalalisha harakati za kimaisha ziendelee) lakini wakati huo huo taarifa za reja reja zikiendelea kuzagaa mitaani.

Hivyo ubalozi wa USA yuko sahihi kwa 100%, na hakuna ajabu yoyote kwa USA kutoa taarifa zenye lengo la kulinda raia wake waliopo hapa Tanzania. Ndio kazi iliyemleta Tanzania, na analipwa kwa kodi za wamerekani. Hatuwezi kumpangia cha kusema wala kufanya juu ya raia wa nchi yake.

Na sisi balozi wetu wa Tz aliyepo kule USA anapaswa kutoa taarifa za kulinda raia wa Tz waliopo huko USA au wanaotaka kwenda USA (ikiwezekana wasiende kabisa!) maana huko Corona ipo na kuna ghasia za maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi. Bahati mbaya balozi wetu huko USA yuko usingizini tu. Hajui anachotakiwa kufanya, sijui anasubiri kuambiwa na kina Bashiru au Pole Pole kitu cha kufanya

Uko sawa.
Kuna watu wanashindwa kuelewa kuwa Eneo la Ubalozi wa Merekani nchini Tanzania ni nchi kamili ya USA na Balozi ana Haki ya ku-report lilote au chochote anachokiona ndani ya Tanzania.
Covid-19 bado ipo Tanzania na ndiyo maana bado Serikali inasistiza watu kuvaa Barakoa, Majitiririka na Kufukiza!
Kuna Madreva wa Malori wanaovuka mipaka kwenda Kenya, Uganda,Rwanda, Zambia, DRC n.k wanapimwa na kuonekana Wana Maambukizi lakini Serikali haitoi any update!
Tunasikia Kuna raia wa Namibia kaondoka Tanzania juzi kwenda Namibia kufika kwao amepimwa kakutwa ana Virusi vya Covid-19!
Balozi wa Marekani yuko sahihi kabisa kama Serikali Wanataka kumnyamazisha Balozi waanze kutoa taarifa ya every after 24 hrs Kama wanavofanya Majirani zetu.....Kwani Kuna tatizo gani kutoa updates? Kama mnapima watu 100, 500 au1000 na wote hawana maambukizi nini mbaya? Kuficha data ni uwoga na utapeli wa kijinga!!!
 
Wewe ukitangaziwa wamekufa 200 itakusaidia nini? Utaenda kuwafufua?
Serikali imeshasema ugonjwa upo tuchukue tahadhari full stop
COVID ipo lakini sio ugonjwa special sana hadi tuutukuze. Kuna magonjwa mengi kila dakika yanaua watu wengi tu na maisha yanaendelea.
Kwenye hii COVID namuunga mkono raisi Magufuli

Hayo ni maswali ya kihuni.
Hivi huko wanakotangaza idadi ya Maambukizi, walokufa au kupona kunakuwa na Ufufuo wa wafu?
Hizo ni data zinaxosaidia ku-alert jamii na kusaidia kupanga strategies za kukabiliana na Covid-19 kwa kujua ukubwa au udogo wa tatizo....!
Kunyamaza au kuficha taarifa za ugonjwa ni udhaifu,uwoga na unafiki wa kiwango cha juu sana!!
 
Pascal utamponza Jiwe akurupuke ,maana baada ya kumwita balozi ndio wamewatwanga hizo taarifa mbili unaelewa maana yake?Ya Kwanza ya Mike Pompeo ya pili ya Jana ,kiteknolojia,kiuchumi,kimabavu yaani kijeshi bado watoto wadogo sana Saddam Hussein na Muammary Qaddafi na pesa zao na silaha zao ambazo sisi hatuna wamefyekwa ije kuwa Jiwe watakamata kama kuku.
 
Baada ya kumwita balozi wa Marekani majibu yalikuwa haya hapa.Haisadii Sasa wewe unafikiri Jiwe atapona wamarekani hawamwachi mwaka huu time will tell ,moods endelea kublock .
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.

Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.

Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.

Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.

Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.

Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.

Paskali
Pascal, ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya. Usemi huu ni mzito sana hasa ukiangalia mustakabali wetu na jumuia za kimataifa kwa siku za karibuni.
Iraq na Iran hapo awali zilikuwa na mahusiano mazuri sana na ya faida na Marekani. Lakini zilipoanza chokochoko za kuitana majina mabaya Waongo, wauaji, hawana haki za binadamu nk yaliyofuata yanajulikana na hasa kwa rafiki mkubwa Saadam kuishia kunyongwa.
Hali hiyo hata kwa Gaddafi wa Libya. Alipimana ubavu na US ikaishia kufia mtaroni na ni baada ya kuitwa majina mabaya.
Kwa uzalendo uliotukuka tuzungumzie viashiria vya kwetu kwa muktadha wa hoja yako. Kwa nini tumekuwa na mahusiano mabaya ghafla na hawa jamaa na wameanza kutufanya kama mbwa (kutuita majina mabaya) anayetaka kuuawa?
Walikuja na hoja za Makonda na kumpiga marufuku asikanyage kwao. Local media zetu zikatumika na muhusika kutoa kauli za dharau na serikali ikapuuzia tamko lao mabeberu. Mistake.
Huwezi kuambiwa mtu wako anazuia watu kuishi (anaua) halafu hata kuomba ushahidi uchunguze na kuchukua hatua hutaki maana yake ni mzushi, na wameweka kiporo wababe hao.
US katika kujibu tamko mwanzoni mwa mwaka huu la Rais aliyesema uchaguzi utakuwa huru na haki walisema wanategemea Rais atalinda kauli yake na kuruhusu tumehuru lakini dalili zote ni kuwa US wamepuuzwa kimya kimya. Huwezi kumpuuza kiwango hicho mtu anayekufadhili wagonjwa wako kupata dawa za bure ARV na huduma nyingine nyingi.
Yako mengi, na Pasco na wengine wanayajua. Back to mjadala ni kuwa jee huku kuanza kuitwa majina mabaya (kama mbwa anayetaka kuuliwa) ni sababu za kuelekea kutuchapa? Wanatuchapaje! Nadhani wana njia nyingi sana za kutuchapa hasa mwaka huu wa uchaguzi kwa kulichochea na kulianzisha tuu.
Jee tuko tayari kuwadhibiti kama taifa? Hapana hapana hapana. Sio katika hali hii tuliyonayo.
CCM imeleta utengano ulio zaa uadui wa kiitikadi, ni suala la kumwagiwa petrol kidogo tuu na tunalipuka kama Libya. Na hilo likitokea kwa ufadhili wa hao tuwaitao mabeberu nchi haitakuwa mikononi mwa CCM tena wala Chadema, ACT au CUF bali kwa vibaraka watakao wekwa na hao walio fadhili pambano.
CCM watumie huu muda mfupi kabla ya uchaguzi kuweka mambo sawa na kurudisha kuheshimiana. Mazingira ya uchaguzi yawe ya haki na huru huku wakifuta makesi yote ya kisiasa tuingie katika ushindani huku watu wanacheka sio wameficha visu mfukoni.
Mimi sio mwanaccm, lakini Nina watoto wanaccm na ndugu wanaccm. Jee naweza kufurahi ugomvi wa kisiasa? Kila mtu akijiuliza hilo ataona kuwa siasa ni jambo la kupita na maisha yapo tuu.
TUOGOPE SANA KUITWA MAJINA MABAYA. KUNA KITU WANAPANGA KUFANYA
 
Hayo ni maswali ya kihuni.
Hivi huko wanakotangaza idadi ya Maambukizi, walokufa au kupona kunakuwa na Ufufuo wa wafu?
Hizo ni data zinaxosaidia ku-alert jamii na kusaidia kupanga strategies za kukabiliana na Covid-19 kwa kujua ukubwa au udogo wa tatizo....!
Kunyamaza au kuficha taarifa za ugonjwa ni udhaifu,uwoga na unafiki wa kiwango cha juu sana!!
Kwa hiyo ukiambiwa kuna vifo 300 strategies zitabadilika?
Kuna tofauti ipi ya kuambiwa ugonjwa bado upo na kutangaziwa idadi ya vifo?
Hatutangazi sasa.
 
Back
Top Bottom