CoViD-19: Siku 30 zijazo ndo muhimu zaidi kujitahadhari, angalia hili jedwali hapa

CoViD-19: Siku 30 zijazo ndo muhimu zaidi kujitahadhari, angalia hili jedwali hapa

Virus ni content kutoka kwenye cell , fovoured ph yake ni around neutral, ikizidi survivability inapungua content yake inakuwa denatured because virus ni RNA ni kapart ka protein. Protein inakuwa affected na higher or low PH, PH ya mazingira yake ikizidi au kupungua neutral umbo la kirusi linakuwa distorted

NAONA HAPO WAMEBASE KWENYE HIYO POINT

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimekuelewa vizuri sana....
Naamini anaejua anachokiongea hawezi kukosea maelezo kiasi cha kutoa maana tofauti, In this case the wording was off. mi hutumia hii njia kujua whats fake and whats genuine. Hata ninaponunua kitu nikawa na wasi wasi kama ni fake mi hutafuta the fine details kama font, barcode, na vitu kama hivyo, more often than not hua kuna kasoro.
 
Sawa sawa

Hii nineikuta kwenye WhatsApp sehemuu

Hii ni kutufahamisha sisi kuwa pH ya virusi vya corona inatofautiana kutoka 5.5 hadi 8.5.

Wote tunahitaji kufanya, kupinga virusi vya corona, tunahitaji kuchukua zaidi ya vyakula vya alkali ambavyo viko juu ya kiwango cha juu cha pH cha Virusi.

Ambavyo ni:

* Limao- 9.9pH *
* Chenza- 8.2pH *
* Parachichi- 15.6pH *
* Vitunguu - 13.2pH *
* Maembe - 8.7pH *
* Tangerine - 8.5pH *
* Mananasi - 12.7pH *
* Dandelion - 22.7pH *
* chungwa - 9.2pH *

Unajuaje kuwa una coronavirus?
1. * Kuwashwa kwenye koo
2. * kukauka koo
3. * Kikohozi kikavu. *
4. Joto kubwa
5. kupumua kwa tabu

kwa hivyo unapoona vitu hivi haraka chukua maji ya moto kiasi weka limao kisha kunywa

Usibakie na habari hii peke yako. Sambaza kwa familia yako yote na marafiki. Mungu akubariki.
Hivi hii ni kweli au ndo kuna watu wanataka kutuuzia malimao na maparachichi.
 
Facts we are not safe at all [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24] [emoji24]
View attachment 1405768

Kwa mwezi mzima, USA ilikua na kesi 15 tu, walidhani wako salama na wameishinda corona!

Siku 22 za kwanza, Italy walikua na kesi tatu tu!!, walidhani wako salama!!!!
Siku 21 za kwanza, Egypt walikua na kesi 3 tu, walidhani hali iko sawa!!!
siku 26 za kwanza, Spain walikua na kesi 7 tu, walidhani hali iko shwari!!!
siku 34 za kwanza, France walikua na kesi 14 tu, walidhani madaktari wako ngangari kuzulia virusi!

Italy, USA, France, Germany, South korea zimekua zikipambana na corona kwa siku zaidi ya 52, Nchi za Africa kando na Egypt na SA, zimekua zikipambana na corona hata siku ishirini hazijapita alafu tunajifanya eti huku kwetu hali si mbaya kama ulaya, kumbe hao jamaa siku ishirini za kwanza hali yao ilikua shwari tu kama vile huku tunadhania.

Alafu, Ukiangalia nchi za USA, Italy, France... kuna mahali flani kwa jedwali utaona kesi zao za siku zilikua zinaongezeka mara mbili ya siku iliopita... Hii ni baada ya wao kuacha kufanyia testing kwa wale walio na dalili (symptoms) za corona pekee na badala yake kufanya mass testing ya watu wote walio safiri hata kama ni kutoka eneo moja la nchi kwenda eneo lengine.....

Kwa mfano, USA sahii ndo inaongoza kwa kesi za crona ikiwa ni kesi 188,000 zilizopatikana positive, lakini ukiangalia USA ilianza kufanya mass testing wiki iliopita, kabla hapo walikua hata hawajui hali kamili

hii tovuti inaonyesha nchi zinazoongoza kwa total tests zilizofanya na nchi by 20th march, wakati huu, USA ilikua haijaripoti kesi nyingi kwasababu walikua wameanya tests 103,000 pekee

View attachment 1405783

How many tests for COVID-19 are being performed around the world?

Sahii USA ndo inaongoza kwa kufanya tests kuliko nchi, hakuna nchi inaikaribia kwa test manake wanasema wamefanya 1 million tests, hii ndio maana kesi za USA zimekua zikiongezeka kila uchao hadi kupita kesi za china, Italy, France..etc.....

--------------------
The White House promised an ever-increasing number of coronavirus tests would be available by the end of the month, saying the number of available test kits could be as high as 27 million. But tracking analysts say only about 1 million total tests have been administered nationwide.
The White House promised 27 million coronavirus tests by end of March, but U.S. just hit 1 million
-------------------------

Kenya najua tumefanya tests kama 800 na contact tracing and quaranteen imeika watu 2,000.... Serekali ilitangaza akwamba wataanza kufanya mass testing sijui ni wiki hii au lini, lakini wakianza kufanya, usishtuke ukiona kesi zinaongezeka kwa ma mia kila siku....

current stats as of today, sorted by total cases

View attachment 1405789

sorted by total deaths

View attachment 1405801

-------------------------------------------------------

Kwahivyo tuwe makini, fwateni maaagizo ya serekali manake hao wengine walikua na kesi chache kwa wiki kadhaa hapo mwanzoni na wakafikiri wako salama, Kumbuka huku Africa tukijaza mahospitali kwasababu ya corona magonjwa mengine ambayo yanaua watu wengi yatawanchwa kutibiwa, watu walio na malaria, ukimwi, watakua hawajisumbui kwenda hospitali manake wanaogopa corona kwahivyo watabaki majumbani waugue kimya kimya... kwahivyo hata kama si watu wengi watauliwa na corona, kuna wengi zaidi watakufa sababu corona ilipewa kipaumbele kwa hospitali zote.

Take care, be safe!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hehehe mbona imekuuma hivi, hasira zako hizo hzitapooza Corona, ni kirusi ambacho kimeshatua Afrika na lazima tupambane sio kujiwekea hasira za kijinga.
Fahamu kwamba sisi tunapima watu 300 kwa siku ilhali nyie juzi waziri wenu niliona sehemu amesema mumefaulu kupima watu 300 tangu Corona iwashukie, sasa hapo labda kilaza stupid mwenye IQ ya zezeta hataweza kuelewa tofauti ya nchi inayopima watu 300 kwa siku na ambayo inapima 300 kwa wiki mbili.
Tatizo lenu mnategemea maabara moja tu, Tanzania visiwani mpaka bara, mikoani kanda ya ziwa, kusini na kaskazini nyote mnatuma samples zenu sehemu moja Dar, kule sampuli zimesongamana.
Sisi hapa tuna maabara kadhaa zimezagaa maeneo tofauti, hivyo tunao huo uwezo wa kupima watu wengi kwa kasi. Nyie mumekua mfano wa mtu kuwachekelea wenye UKIMWI kisa yeye hajapima, yupo yupo tu.
Fahamu hiki kirusi kinasambaa kama moto wa porini, hao wachache mliofaulu kuwagundua nacho utakua kila mmoja anaweza kuwa aliambukiza watano na hao watano kila mmoja huko mbele kaambukiza watano wake....mtandao mrefu sana na ndio kinachotendeka Ulaya.
Hiki kirusi kuna wengi wanaambukizwa na kuambukiza hata kabla hawajaona dalili, yaani ukiambukizwa, chochote utagusa au yeyote unamgusa anacho.
Huko kwenu tatizo wataalam wote wamekua waimba mapambio wa kumsifia rais badala ya kumshauri, ameishia kuwa na kauli tofauti na marais wote wa dunia, amewaambia mchukulie poa na kuendelea na maambo ya misongamano.
Maabara kadhaa ni ngapi hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ikiipiga Afrika kama ilivyoipiga ulaya na Amerika nina uhakika robo tatu ya bara la Afrika itaondoka!
 
Huwa unasafiri kwa daladala?
Kuna projection zimeonyesha mwezi huu hapa Kenya tutakua na waathirika 10,000 hivyo muhimu kujiandaa kisaikolojia, serikali iendelee kupima kwa kasi na kufukuzia marafiki wa marafiki wa marafiki wa waathirika wote, vituo vya kupima viwe kote nchini, halafu Wakenya tuhamasishane njia za kujizuia, binafsi kila siku nafanya ugomvi na makondakta wa daladala wanaofanya uzembe, tuwatajie bila kuchoka, na zaidi ya yote tuepuke kusafiri kwenda vijijini waliko wazee wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maabara kadhaa ni ngapi hizo

Sent using Jamii Forums mobile app

Ninazozifahamu hadi sasa
- National Influenza Center
- Kenya Medical Research Institute (Kemri)
- Moi Teaching and Referral Hospital (MTRH) kule Eldoret
- Tawi la Kemri Kisumu pia
- Na sasa Mombasa pia wamewezeshwa.

Kwa kifupi zimezagaa mikoa yote, hatutegemei sehemu moja.
 
Huwa unasafiri kwa daladala?

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwani ni ajabu kusafiri kwa daladala, fahamu za kwetu sio chafu zenye mibanano kama kwenu, huku kila mtu lazima aketi chini na kufunga mkanda, huwa ni nafuu sana hata kuliko magari binafsi, wengi hutumia magari binafsi kama unajua utakua na mizunguko ya mjini, lakini kama unakwenda sehemu moja na unajua utageuza moja kwa moja, huna haja ya kuhangaika na gari lako.
 
Yap, Replication is just a simple mechanism that can be done in Vitro,
infact Virus doesn't replicate in it's own, it codes your genetic code to replicate its own copies,
Yaani kwa Lugha rahisi ni kama Paka anampanda mbuzi halafu mbuzi anaanza kuzaa mapaka ya kutosha. This is what it does, tofauti na bacteria au fungi ambae akikuvamia anapata mahitaji kama chakula, hewa na pH inayomfanya azaliane kwa kujigawagawa (fission/lysis) na kufanya idadi yake iongezeke.
Na ndio maana hadi leo hakuna dawa ya Virus, yaani hata dawa ya Virus wa Mafua haipo, ni ngumu sababu virus ni just a particle with genetic material iliyovaa protein, anaweza kujibadilisha na kuendana na host tofautitofauti.
Mfano huyu virus wa Corona leo utashangaa kuona mwakani amebadilika sio Huyu tena, (mutation) means hata kama ni kutafiti dawa maana yake muanze upya ambapo huenda akabadilika tena. Only vaccine can work.
Kuna vitu basic mtu hatakiwi kubisha. "Virus sio living organism" yet it replicates it genetic code, interesting!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kipindi kama hiki? Acha fix bwana, huna Gari.
Kwani ni ajabu kusafiri kwa daladala, fahamu za kwetu sio chafu zenye mibanano kama kwenu, huku kila mtu lazima aketi chini na kufunga mkanda, huwa ni nafuu sana hata kuliko magari binafsi, wengi hutumia magari binafsi kama unajua utakua na mizunguko ya mjini, lakini kama unakwenda sehemu moja na unajua utageuza moja kwa moja, huna haja ya kuhangaika na gari lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzi mzuri sana unaweza kuwa pinned. Hoja fikirishi kulingana na uzi huu ni hizi
1. Testing wenye dalili
2. Mass testing
Kwa mujibu wa uzi testing wenye dalili ilionyesha kuongezeka waginjwa kwa uchache sana
Mass testing inaonyesha idadi kubwa ya watu wenye maambukizi

HOJA.:
Kwanini watu wenye maambukizi hawakuonyesha dalili baada ya kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu japo hawa kuwa tested?
Ili waongezeke kwa kipimo cha testing wenye dalili?

Kwanini Mass testing inaonesha waathirika na COVID 19 wengi?

Je iko shida kwenye mass testing?
Vipimo ni transimiters agents?
Hofu(Fear) inapunguza kinga za mwili na kuruhusu virus kupata nguvu ya kuonyesha dalili?

Niko huru kukosolewa. Hata kwa povu ruksa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko hivi mkuu, 80% ya watakaoambukizwa COVID19 watapona on their own na Majority Yao hawatanotice hata dalili, why bother testing them uwajaze fear?
Kwa nini wale wanaoona dalili wasiwahi kwenda vituo vya afya kama mamlaka zinavyohimiza na uzuri unapiga simu unafuatwa ulipo?
Mimi naona kutrack wale suspects ni Bora zaidi na pia kuhimiza kila anaehisi dalili awahi kituo cha afya, hatuwezi kupima nchi nzima kwanza hatuna resources na pia ni kutengeneza unnecessary panic.
Japo nahisi kuna nchi zinaona fahari kusoma namba kubwa ya wagonjwa si unajua kuna pesa mzee $ [emoji389]

Kwanza kipindi hiki ndio sitoki kabisa, kazi yangu inanipa uhuru wa kukaa ndani hata mwezi uishe, natoka tu wakati wa kukimbia.
Makondakta wa daladala nagombana nao nikipita stendi na kuona wachache wao vichwa ngumu wanapokea abiria bila sanitization.
 
Kama huwezi kufanya "tracing of contracts" ya watu wote watakao test positive ili waweze kuwa "isolated", mass testing inapoteza maana kabisa, ni upotezaji wa resources na kuongeza mzigo katika mfumo wa Afya, bora kuamua kufanya " lockdown" japo kwa mikoa yenye maambukizi mengi "hotspots".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa nyie ndo mnahatarisha maisha ya watu zaidi kwa kuokota okota na kusambaza habari za vijiweni.

Kirusi kina pH?!! ni sawa na kuniambia pH ya mbuzi ni 8.4!!

Chemistry 101....
pH scale unaijua?
Acid ni kati ya 0 hadi 6 na alkaline ni kati ya 8 hadi 14.
Sasa Limao inakuaje 9.9? Chungwa inakuaje 9.2?!
Funga kazi ni parachichi 15.6 na Dandelion ya 22.7!!! Hiyo ni pH scale ya sayari nyingine.
Hivi shule ulienda kufanya nini?!!
😀😀😀😀😀😀😀
 
Uzi mzuri sana unaweza kuwa pinned. Hoja fikirishi kulingana na uzi huu ni hizi
1. Testing wenye dalili
2. Mass testing
Kwa mujibu wa uzi testing wenye dalili ilionyesha kuongezeka waginjwa kwa uchache sana
Mass testing inaonyesha idadi kubwa ya watu wenye maambukizi

HOJA.:
Kwanini watu wenye maambukizi hawakuonyesha dalili baada ya kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu japo hawa kuwa tested?
Ili waongezeke kwa kipimo cha testing wenye dalili?

Kwanini Mass testing inaonesha waathirika na COVID 19 wengi?

Je iko shida kwenye mass testing?
Vipimo ni transimiters agents?
Hofu(Fear) inapunguza kinga za mwili na kuruhusu virus kupata nguvu ya kuonyesha dalili?

Niko huru kukosolewa. Hata kwa povu ruksa

Sent using Jamii Forums mobile app

Mass testing ni muhimu sana kupunguza maambukizi maana unawagundua mapema kabla hawajaambukiza, fahamu kwamba miili inavyopokea hiki kirusi inatfautiana binadamu kwa binadamu, kunao anapokea na kuambukiza bila ya yeye kuhisi dalili yoyote, kunaye anapokea na dalili kupandisha mzuka ndani ya wiki moja anafariki, hususan kirusi kikishambulia mapafu na bila ventilator unakwenda.
Watu wengi tumezoea tukiumwa mafua tunayanywea maji moto ya limau unakohoa siku mbili yanakuondoka, sasa huo uzembe kwa sasa haipaswi, ukiona unapata dry cough na una uhakika kwa namna moja au nyingine ulikua exposed sehemu, na kwa vile vituo vya testing vipo kadhaa, bora nenda ukakaguliwe kabla kuambukiza mkeo, watoto wako na majirani na wao wakaambukize huko mbele, ni muhimu kuchukua tahadhari.
Pia ni muhimu sana kuwa na hofu, yaani tutishike balaa belua ili tuchukue tahadhari, hiki kitu sio mchezo kinaua maelfu kwenye nchi ambazo zina uchumi na teknolojia za hal ya juu, kwa hivyo hofu itatusaidia, la sivyo kiburi na ujinga vitatuangamiza, unakuta kwenu huko Makonda bado anakusanya wananchi maskini kwenye mikutano nimeona picha yake.
 
How?
Mfano Nairobi ina watu karibu milioni 4, unafanyaje hiyo mass testing au mnapima jiji zima?

Hatuna uwezo wa kupima jiji nzima, unafukuzia kwanza wale wote ambao wamekua into contact na wachache waliopo kwenye karantini na kila unayemfikia unafukuzia yeyote aliyegusana naye yaani unajaribu kukusanya mtandao wote, ila pia unahamasisha kila mmoja anayehisi dalili zozote aje akaguliwe mapema, hiyo ndio ubora wa kuwa na maabara kadhaa, sampuli zinashughulikiwa fasta fasta.
Wenzetu Ulaya wanapima 100,000 moja kwa siku, sisi hapa tunapumulia kwenye 300 kwa siku, nyie hapo kwa wiki mbili ndio waziri alisema mumefaulu kupima 300.
 
Aah, hutoki kabisa kwa sababu kazi yako inakupa jeuri, meaning umeajiriwa.
Kumbe kelele zoote unasubiri mwisho wa mwezi kuchungulia bank account,[emoji3][emoji3]
BTW Hata mimi kazi yangu inaniruhusu hata kukaa ndani miezi sita bila kutoka kabisa, ila siwezi kujifungia ndani muda wote huo na nina miradi yangu mikoani, lazima nisafiri karibu kila wikiendi na niwe na likizo ya wiki nzima kila quarter ili niwe huru, sasa ukinifungia ndani unadhani ni nini kitatokea?
Ndio maana watu timamu kama Magufuli wanalifahamu hili sababu nao ndio wametoka huku na wanawajua watu wao, Kenyatta ni mtoto wa Kishua, Familia bora, hajui shida ndio maana hajui hata maisha ya wakenya ndio maana anakurupuka na anaamua mkae ndani ikiwa Maisha ya 90% wakenya ni mkono kinywani, Ni wazi viongozi wenu hawawajui, ndio maana Muhoho Kenyatta yule mtoto wa Uhuru ambae atakuwa Rais wenu baadae hajui hata kiswahili, anajihisi ni Mzungu..
Maisha hayawezi Simama sababu ya Mafua na ukizingatia Ajali za Barabarani huku kwetu zinaua mara kumi ya hiyo corona, Yaani kama Watz wangekuwa na hofu kiasi hicho basi wangeacha hata kusafiri, juzi hapa umekuja kufungua uzi unalalamikia Watz wamekuja kupiga mishe za pesa Kenya bila kujali Corona,

Muhimu Chukua Tahadhali kwako na wote uwapendao, Ukiona dalili piga simu bure au ripoti haraka kituo cha Afya, Ukiona mtu ana dalili piga simu haraka, Mgeni yoyote karibu Tz ila lazima ukae quarantine siku 14 kwa Gharama zako.

Back
Top Bottom