COVID-19: Tanzania yakataa chanjo ya kigeni, yalenga tiba ya kiasili

COVID-19: Tanzania yakataa chanjo ya kigeni, yalenga tiba ya kiasili

Heri kusubiri chanjo mpk mwaka 2022 mwishoni au kutumia wataalum wako..? Ni wapuuzi tu ndio watakaoitusi serikali,ifike mahali serikali isimamie watu wake tu kuliko kukarisha kalio kusubiri chanjo ya mwaka 2022!. Na hii iwe funzo kwa mataifa yote ya afrika ya Kuwa sisi tunahesabika Kama race ya mwisho so Kama hatuta beba nchi zetu wenyewe hakuna atatubebea.
 
Chanjo "daraja la kwanza" ya akina Pfizer na wenzake huko kwa binadamu "daraja la kwanza" wanaiogopa wakidai imetengenezea kwa kukurupuka mno, je hii yetu ya daraja la mwisho si ndio mkojo wa punda kabisa....
Jamani sisi tunahitaji chanjo ya malaria na ukimwi sio covid 19, tukatae huo upumbavu wa kufanya miili ya waafrika ni panya wa maabara!
Kwahiyo hizo ulizo taja mnatengeneza nyinyi?
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽 Tushukuru sana Mungu tulikuwa na viongozi waliokuwa na uelewa wa hali ya juu na pia waliona mbali siyo hawa ambao wanajifanya wanajua kila kitu kumbe hawajui lolote.
Hapa Tanzania miaka yote tumekuwa tukipokea na kuzitumia chanjo kutoka kwa mabeberu kama za Polio, Kifua Kikuu kwa watoto, Pepo Punda, Kifaduro, Surua, Kuharisha, Nimonia, Yellow fever, Hepatitis nk. pasipo shida zozote. Sasa leo tunaibuka na kuikataa chanjo ya Corona, eti tunatengeneza zetu za miti shamba!

Upuuzi mtupu wa Tz.
Sijui nani kawaroga?
 
Heri kusubiri chanjo mpk mwaka 2022 mwishoni au kutumia wataalum wako..? Ni wapuuzi tu ndio watakaoitusi serikali,ifike mahali serikali isimamie watu wake tu kuliko kukarisha kalio kusubiri chanjo ya mwaka 2022!. Na hii iwe funzo kwa mataifa yote ya afrika ya Kuwa sisi tunahesabika Kama race ya mwisho so Kama hatuta beba nchi zetu wenyewe hakuna atatubebea.
Malalamiko hayo sio mazuri msiwafanye wenzenu ela za kiutafiti maabara wanaokota eti upewe sawa na matajiri. Wew ukiwa kama mfanya biashara unauza m2 asie na uwezo wa kununua bidhaa flani unaweza mpa bure wakati bidhaa iko kwenye demand na wenye uwezo? Yaani waafrica tunazingua kujifeel imferior kila ki2 tupewe favour sisi kulko matajiri malalamiko muda wote.

Jikite kuipongeza serikali kufanya maamuzi ya ku2mia watafiti wa ndani sio kuwatukana wenzako utadhani wewe ni jukumu lao. Infact sidhani mtu mwenye uwezo bongo akiagiza kwa sahivi atakataliwa ila nyny wa bure subirini 2022.

Tena bora hata jamaa wanaonekana kuthamini tungekuwa sisi nd tuna uwezo nadhani wasingesaidiwa hivi. Maan hata madini tunalalamika sana kuibiwa wakati hizo ela zimefanya project kubwa zilizoifikisha dunia hapa tulipo. Nahisi tulitaiwa tuibiwe maan kucontribute kwa hiari tusingeweza.
 
Umekurupuka ndugu! Ujumbe wangu ni kuitaka afrika iamke na sijalaumu yoyote Yule hapo zaidi ya kuwalaumu wanaoiponda serikali juu ya uamuzi huo! Hiyo ni alert tu by the way ulivyo nielewa ndo ubongo wako ulivyo mpana ktk ufinyu wa upana wa uelewa.
 
Chanjo "daraja la kwanza" ya akina Pfizer na wenzake huko kwa binadamu "daraja la kwanza" wanaiogopa wakidai imetengenezea kwa kukurupuka mno, je hii yetu ya daraja la mwisho si ndio mkojo wa punda kabisa....
Jamani sisi tunahitaji chanjo ya malaria na ukimwi sio covid 19, tukatae huo upumbavu wa kufanya miili ya waafrika ni panya wa maabara!
Kwa nini unasema ''hatuhitaji''? Sema huhitaji wewe na familia yako. Wako wengi tu wanahitaji. Hata Ulaya kuna wengi tu wamesema hawataki kuchanjwa lakini bado hawajazuia wanaotaka. Ni haki ya mtu kuamua juu ya matibabu yake.
 
Umekurupuka ndugu! Ujumbe wangu ni kuitaka afrika iamke na sijalaumu yoyote Yule hapo zaidi ya kuwalaumu wanaoiponda serikali juu ya uamuzi huo! Hiyo ni alert tu by the way ulivyo nielewa ndo ubongo wako ulivyo mpana ktk ufinyu wa upana wa uelewa.
Ushaanza kujikana hapa hapa tena. Aliesema wazungu wanatuona wapumbuvu nani? au ulikuwa unamaanisha nini?
 
Kwa hili serikali big up. Kwanza hata hivyo korona kwetu hakuna. Japo najua watawanyima vibali watu wetu kusafiri huko kisa hawana chanjo.
 
Tanzania haitaagiza kinga ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, Wizara ya Afya imesema.

Badala yake, msemaji wa Wizara ya Afya Gerald Chami alisema, serikali inaendelea na shughuli ya kufanyia majaribio tiba za kiasili.

“Hakuna mipango ya kuagiza chanjo ya virusi vya corona kutoka ughaibuni. Wataalamu wetu wa afya na wanasayansi wanaendelea kutafiti na kufanyia majaribio matibabu ya kiasili,” akasema.
Tanzania nchi yangu imefika pabaya. Naamini tuna watalaamu wa kutosha wa kulitafakari jambo hili na kutoa maamuzi yakueleweka. Nionacho hapa ni mkanganyiko wa hali ya juu.
Tunaendeleza upuuzi ule ule wa dawa siu chanjo ya Madagascar ambayo hakuna anae izungumzia sasa.

Huko duniani COVID 19 inaua kweli (hapa kwetu ni siri ya watu wachache, wengi hatujui kinacho endelea). Dunia ikifunguka tutawalinda vipi watanzania watakao safiri na je wageni wakishuka na hiyo Covid 19 tutafanya nini?. Afadhali wangesema tutaangalia ni chanjo ipi inatufaa lakini naona wameamua tuendelee kunywa "matogwa" yetu?.
 
Ushaanza kujikana hapa hapa tena. Aliesema wazungu wanatuona wapumbuvu nani? au ulikuwa unamaanisha nini?
I mean kwamba tunaonekana kama race ya mwisho. Kwasababu hiyo ya 2022 kwenye uzi hapo wamesema zitapewa nchi tajiri kwanza sasa watu wamejikita kwa wenye nacho kwanza w useme wanakuona kama race y mwisho meaning wanakudharau wakati wanakusaidia still.
 
Ushaanza kujikana hapa hapa tena. Aliesema wazungu wanatuona wapumbuvu nani? au ulikuwa unamaanisha nini?
Hivi mkuu unajua kusoma kweli au nabishana na mtu jitu tu..😅
 
I mean kwamba tunaonekana kama race ya mwisho. Kwasababu hiyo ya 2022 kwenye uzi hapo wamesema zitapewa nchi tajiri kwanza sasa watu wamejikita kwa wenye nacho kwanza w useme wanakuona kama race y mwisho meaning wanakudharau wakati wanakusaidia still.
Historia ya muafrika kuonekana race ya mwisho haijaanza leo labda uwe huelewi mambo! Hivi mkuu itokee ugonjwa serious unaoua kwa spidi then uje uwaambie watu watapata dawa 2022 mwishoni unafikiri nini hapo we komba mboga..?? Unazungumzia utajiri kwenye uhai au unaandikaandika tu!
Hujui italy Hadi watu walikuwa wakitupa hela kisa hazikuwa zinawasaidia covid ilikuwa inaua watu na utajiri wanao! Mi naona Kuna mahali hapajakaa sawa ktk uelewa wako ujumbe wangu umeusoma kuhisia na sio kiuchambuzi.
 
Tutaagiza za kuleta maabara zetu za utafiti bongo na zingineza za kuchoma sample, tulieni
 
Wewe ndio hujaelewa mbona wenye uwezo baadhi ya magonjwa ambayo yanaua kwetu wanaenda kuponea nje.

Madaktari wanahitaji pesa kuendelea kufanya tafiti mzee. Halafu wewe hujasoma vizuri maelezo hiyo ya 2022 ni ya makampuni binafsi sio ya WHO maan yenyew imeshaanza kutolewa uganda na kenya.
 
Wewe nd hujaelewa mbona wenye uwezo baadhi ya magonjwa ambayo yanaua kwetu wanaenda kuponea nje. Madaktari wanahitaji pesa kuendelea kufanya tafiti mzee. Af wewe hujasoma vizuri maelezo hiyo ya 2022 ni ya makampuni binafsi sio ya WHO maan yenyew imeshaanza kutolewa uganda na kenya.
😅😅 Dah! Mkuu tufanye umeshinda ili yaishe ilimradi tunapumua inatosha..😅
 
Nchi hii yaweza kuwa hatari zaidi duniani. Siku moja hii jeuri itatokea watu fulani puani. Au nasema uongo ndugu zangu??
 
Wazungu wana hasira na waafrika walisema tutakufa kama kuku wamekuta hatufi sasa wamezira ohh dawa hatuwapi hadi 2022 wakidhani labda tutawalilia lilia hali jibu tumewapa hatutaki
 
Back
Top Bottom