COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

COVID-19: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atangaza ongezeko la Wagonjwa Wapya 196. Visa vyafikia 480

Vifo bado ni 10?
Mpaka tarifa hizi zinakuja hapa, ilikuwa umesubiriwa wewe Tu ili kuwepo sasa wa kuongezeka Kati ya waliokufa, Bahati mzuri kumbe uko vizuri, hakuna SASA wa kuongezeka! MUNGU akupe siku nyingi zaidi mkuu, na usiendelee kuombea vifo kuongezeka
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Vifo vingine 6 vya wagonjwa COVID-19 vimeongezeka na kufanya jumla ya vifo kufikia 16 Tanzania, wagonjwa waliopona wamefikia 167. “uzushi wa kwamba kila kifo ni cha corona sio sahihi kuna magonjwa mengine yanayoua”

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''

Kwa nini kuna siri nyingi kuhusu Korona wakati inatakiwa kujulikana hata wale wenye nayo ili tujilinde na kujikinga nao? Serikali haiaminiki hata kidogo kwa janga hili, walitupotosha na kusema ni mafua tu, hawajafunga mipaka kwa abiria, hawakuzuia ndege toka nchi zenye Korona, wakatuambia barakoa ni kwa ajili ya watu wenye korona, sasa wanatangatanga baada ya kuweka pesa mbele kabla ya Afya.
 
Hahaha eti vifo 6 tu nyoooooko. Waliotajwa tu siku chache zilizopita kufa kwa tatizo la kupumua wanazidi 6, makaburi mapya yaliyozikwa watu usiku yanazidi kumi, huyu jamaa anahisi watanzania wote matahira. Hiki ni kituko bora nichukue stats za china sio hizi hahahaha ovyo kabisa
 
Mpaka tarifa hizi zinakuja hapa, ilikuwa umesubiriwa wewe Tu ili kuwepo sasa wa kuongezeka Kati ya waliokufa, Bahati mzuri kumbe uko vizuri, hakuna SASA wa kuongezeka! MUNGU akupe siku nyingi zaidi mkuu, na usiendelee kuombea vifo kuongezeka
"....UTAKUFA HAKIKA" hayo ni maagano ya yule mlieamriwa mumuombe kwa siku tatu.
Tangazeni vifo itasaidia kuweka sawa akili za wabishi kutekeleza maelekezo ya wataalam.
 
jamani msimsumbue Majaliwa ameeleweka wagonjwa ni 480

idadi ya vifo ni 16 tu...na ameongezea kusema 'vifo vingine ni magonjwa mengineyo'

mtajua wenyewe

Labda atoe na
*idadi ya vifo vya magonjwa mengineyo imefikia ngapi.?
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ametangaza Ongezeko la Wagonjwa Wapya wa Corona Nchini 196. Tanzania Bara Wagonjwa 174 na Zanzibar 22. Amesema kuwa visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Tanzania vimeongezeka na kufikia 480.

Vifo vingine 6 vya wagonjwa COVID-19 vimeongezeka na kufanya jumla ya vifo kufikia 16 Tanzania, wagonjwa waliopona wamefikia 167. “uzushi wa kwamba kila kifo ni cha corona sio sahihi kuna magonjwa mengine yanayoua”

Waziri Mkuu akinukuliwa, amesema...

''Kuanzia Aprili 23 - Aprili 28,2020 tumepata wagonjwa wapya wa Corona 196 ambapo kati ya hawa Bara wapo 174 na Zanzibar 22 ambao Waziri wa Afya Zanzibar ameshawatangaza, hii inafanya jumla ya visa vya Corona Tanzania kufikia 480 kutoka 284 ambavyo vilitangazwa Aprili 22''

Kuna mzee wangu amefariki tangu juzi,lakini hadi hivi leo tunasubiria majibu ya corona,sasa katika mazingara ya aina hiyo unatwgemea Nini?Serikali hii ina uwezo wa kukamatwa,kutesa na kuua wanaoikosoa na kufuja Mali ya umma tu
 
Back
Top Bottom