Ni vile hatupendi kuwasikiliza vyema wataalamu wa afya badala yake TUNAMPA MASIKIO ASKOFU GWAJIMA 🤣
Anyways ,hii chanjo ya J&J ina vidudu ndani yake...virusi viitwavyo ADENOVIRUS...hivi vikiingia mwilini mwa mtu huamsha kinga(seli nyeupe) kupambana navyo....
Ikumbukwe Vidudu hivyo(ADENOVIRUS) kimaumbile vinafanana na virusi vya CORONA ila tu vinakuwa vimepunguzwa nguvu ya kuleta madhara.....
Mwili uliochomwa chanjo hiyo huwa na uwezo wa kupambana na virusi vya CORONA pale vinaposhambulia....kwa kuwa MWILI unakuwa na kumbukumbu ya kupambana na vile virusi vya ADENOVIRUS katika ile chanjo ,basi hata Kama ukipata maambukizi mapya(mathalani hii Delta)basi hutoweza kufikia madhara ya kulazwa ama kutibiwa CHUMBA CHA DHARURA na gesi puani......
Kuhusu kifo huweza kufa yeyote tu hata bila ya kuumwa.....
#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#NchiKwanza
#KaziIendelee