#COVID19 #COVID19 NIMR: Chanjo zitakazotolewa Nchini ziko salama kwa asilimia 99.9

#COVID19 #COVID19 NIMR: Chanjo zitakazotolewa Nchini ziko salama kwa asilimia 99.9

Baada ya ufafanuzi mzuri wa kisayansi uliotolewa na Mkurugenzi mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya kupitia Clouds tv sitashangaa kumuona Askofu Gwajima akibadili mawazo na kutimba Ikulu kupata chanjo hapo kesho.

Prof Yunus Mgaya amesema chanjo ya Johnson & Johson inaweza kuwaathiri watu 4 tu katika kila watu 1,000,000 hivyo usalama wake ni wa uhakika.

Prof Mgaya amesema anatamani angekuwa miongoni mwa watu watano wa kwanza watakaochanjwa kesho.

Chanzo: Clouds tv
CCM Chama Cha Mazezeta

EeeenHeee, Heeee!

Mkuu unanifanya nicheke sana!
Kwa taarifa kama hiyo iliyotolewa hapo tu, ndiyo iwe sababu ya wewe kutupa kila kitu pembeni?

Mbona taarifa yenyewe uliyoweka ni kama tangazo la biashara zaidi kuliko matokeo ya utafiti halisia; hilo halikupi shaka kidogo?

Ndiyo, najuwa ni akheri ya kumwamini Prof. Mgaya kuliko mipasho ya akina Askofu Gwajima wasiokuwa na kitu kichwani lakini ukisikia wanapayuka utadhani dunia wameiumba wao!

Prof. Mgaya, kama umemnukuu vyema, na hayo ndiyo maneno aliyotumia katika maelezo yake, basi kachanganya na siasa humo humo kuliko sayansi.
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.

Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.
Mkuu, hata samaki hupata chanjo, labda useme tu kwamba sisi hatuna mazoea hayo.

Inawezekana akawa amesomea "vaccination" ya samaki, kama yeye ni mtaalam katika mambo ya samaki? Haina tofauti sana na chanjo za binaadam. Chanjo ni chanjo tu!
 
Baada ya ufafanuzi mzuri wa kisayansi uliotolewa na Mkurugenzi mkuu wa NIMR Profesa Yunus Mgaya kupitia Clouds tv sitashangaa kumuona Askofu Gwajima akibadili mawazo na kutimba Ikulu kupata chanjo hapo kesho.

Prof Yunus Mgaya amesema chanjo ya Johnson & Johson inaweza kuwaathiri watu 4 tu katika kila watu 1,000,000 hivyo usalama wake ni wa uhakika.

Prof Mgaya amesema anatamani angekuwa miongoni mwa watu watano wa kwanza watakaochanjwa kesho.

Chanzo: Clouds tv
Bwashee, kwa kuwa uko karibu na hao wanaotoa huo "ufafanuzi mzuri wa kisayansi", unaweza kunisaidia kujua 'kisayansi' kama kuna taasisi yoyote ya kisayansi au kitabibu ambayo imefanya haya yafuatayo:
1. Imechukua angalau kachupa kamoja ka hizo chanjo na kuzisasambua ili kujua kwa uhakika kuwa kile tunachoambiwa kimo kwenye ingredients ndicho haswa kilichomo. Kama nakumbuka vizuri, Canada waliikataa chanjo ya J&J kwa kutokubaliana na utengenezwaji wake.
2. Kuchunguza kwa undani madhara yanayoweza kutokea mwilini miaka angalau 10 ijayo, ili tujiridhishe kwamba kweli chanjo (hizi za majaribio) hazina madhara kwa binadamu wa sasa na wa kizazi kijacho.
Kwa kuwa nyie mko huko karibu na wapiga debe nadhani mnaweza kutusaidia sisi makapuku tulioko huku vijijini.
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.

Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.
Huyu Baba Anatumiwa Na Mabeberu
Johnson And Johnson Mpaka Wa Covax
 
Sijamsikia na inawezekana akawa sahihi, ila huyu baba alisoma wapi vaccinology? Yeye yuko kwenye samaki na mambo ya bahari muda wote, authority anaitoa wapi ya kuongelea vaccinology? Tuwekee papers zake kwenye hii field.

Huyu ali advocate malimao na NIMRCAF enzi wa Mwendazake, leo analeta talalila za vaccine.
Hakuna wa kumuamini kabisa katika hili... Waliokuwa upande wa Magufuli waki-advocate natural remedies kwa nguvu zote na kupinga Western methods leo wamegeuka...

Tafsiri yake ni kuwa kesho akija raisi mwenye kuamini katika maombi watageuka tena na kuanza kuponda hizi njia wanazopigia chapuo Leo as per Samia's tune... So sad...

Wanasiasa wanafk na waongo waongo kwa maslahi yao ni wakuwapuuza na kuwaogopa kabisa... Mostly linapokuja suala la kucheza na afya zetu kwa maslahi yao ya gizani...

For now wapo bize na mabarokoa na chanjo... Nchi imesimama kabisaaaaaa.
 
Atuambie kwa nini Wamarekani wanaikimbia na huku wakiwasukumizia Watanzania dosses millioni?
 
Enzi za Marehemu alisema Watanzania tuvute subira kwenye ishu ya chanjo maana chanjo huchukua hadi miaka 10 kutafiti ubora wake, leo kageuka kasema siku hizi kuna tekinolojia mpya ya kuharakisha chanjo kwa hiyo eti chanjo kutengenzwa harakaharaka kama tulivyoona ni sawa!
Hawa ma-professor njaa
 
Hakuna wa kumuamini kabisa katika hili... Waliokuwa upande wa Magufuli waki-advocate natural remedies kwa nguvu zote na kupinga Western methods leo wamegeuka...

Tafsiri yake ni kuwa kesho akija raisi mwenye kuamini katika maombi watageuka tena na kuanza kuponda hizi njia wanazopigia chapuo Leo as per Samia's tune... So sad...

Wanasiasa wanafk na waongo waongo kwa maslahi yao ni wakuwapuuza na kuwaogopa kabisa... Mostly linapokuja suala la kucheza na afya zetu kwa maslahi yao ya gizani...

For now wapo bize na mabarokoa na chanjo... Nchi imesimama kabisaaaaaa.
Tena this blood shameless so-called professor came forward to despise western medicines by that time, during Magufuli's era. Today he is advocating the same thing he denounced!
 
TAASISI ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), imesema ipo kwenye mchakato wa kutengeneza chanjo dhidi ya ugonjwa wa Covid- 19.

Aidha, NIMR ilisema jana kuwa chanjo zitakazotolewa nchini dhidi ya ugonjwa huo ni salama kwa asilimia 99.99 na zimethibitishwa na na jopo la wanasayansi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).

Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk Yunus Mgaya alisema hayo jana wakati akijibu swali kama Tanzania ina mpango wa kutengeneza chanjo yake dhidi ya corona.

Dk Mgaya alikuwa akizungumza kwenye Kipindi cha Clouds 360 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha Clouds kinachomilikiwa na Kampuni ya Clouds Media Group.

“Ndio Tanzania tunao mpango wa kuja na chanjo yetu ya corona. Rais Samia Suluhu Hassan alishasema na Katibu Mkuu akazungumzia hilo pia na sisi NIMR tukapewa jukumu,” alisema Dk Mgaya.

Alisema kutokana na maagizo hayo, tayari NIMR iko kwenye mchakato utakaoifikisha kwenye utafiti wa chanjo yake.

“Nasema Inshallah Mungu akipenda, tunaweza tukawa na chanjo yetu Tanzania ya ugonjwa huu na magonjwa mengine,” alisema Dk Mgaya.

Alisema Covid 19 ilivyoingia na kusambaa dunia nzima wanasayansi waliona hakuna namna ya kuudhibiti ugonjwa huo kwa kuwa hauna dawa hivyo mkazo uliwekwa kwenye chanjo.

Dk Mgaya alisema na hadi jana kulikuwa na chanjo zaidi ya 200 duniani zilizokuwa kwenye majaribio, lakini zilizopitishwa na WHO zitumike chini ya mpango wa dharura ziko sita.

Alitaja chanjo hizo kuwa ni nne kutoka Marekani ambazo ni BioNTech, Pfizer, Johnson & Johnson na Moderna NIAID, Novavax ya Uingereza, AstraZeneca ya Sweden na China ziko mbili; Sinovac-CoronaVac na Sinopharm.

Aidha, alisema chanjo ya Urusi ya Sputnik V ambayo pamoja na kwamba imeshaanza kutumika kwenye nchi nyingi duniani, bado inafanyiwa tathmini na WHO huku Cuba ikitengeneza chanjo inayoitwa Abdala.

Alisema chanjo hupitishwa zitumike baada utafiti na mamlaka mbalimbali kujiridhisha ziko salama kwa matumizi.

“Mfano chanjo inatengenezwa Marekani ni lazima ipitiwe na udhibiti wa mamlaka za Marekani pia lazima WHO iidhinishe. WHO ina kamati zake za kitaalamu zinazokagua mpaka kujiridhisha kitaalamu na kubwa zaidi huangalia usalama na ufanisi,” alisema mtendaji huyo wa NIMR.

Alisema chanjo sita zilizopitishwa na WHO zimefaa, haziwezi kumdhuru mtu kwamba akinywa atakufa au kuugua na kwamba kiwango cha athari ni kidogo mno kinachofikia asilimia 0.00004.

Dk Mgaya alisema manufaa ya chanjo za corona ni pamoja na kupunguza vifo, kuzuia watu kulazwa hospitalini, kupunguza makali ya ugonjwa na maambukizi.

Habarileo
 
Inafikirisha kiasi. Hatahivyo, wasiwasi wangu ni kuona tabaka la watu wa “sampuli” hii, wanaojiita wataalamu, wakishadadia na kufafanua “kitaalamu” ufanisi wa aina anuai za chanjo za COVID-19.

Kama kweli wana ubobezi wa kitabibu, kwanini hawakuthubutu hata “kuungaunga” wapate mfano wa chanjo ya kwao wenyewe na badala yake wakaishia “kuhubiri” ubora na udhaifu wa chanjo zilizoundwa nanwanaume wenzao?

Hivi, mathalani, ni nani utamwamini akikuchambulia mifumo ya gari aina ya TOYOTA kwa ufanyaji kazi wake, ubora na udhaifu, kati ya fundi makenika mzoefu wa muda mrefu na muundaji (manufacturer) wa gari lenyewe?

Rai yangu: Turejee kauli ya Mhe. Rais wetu ya kuwa “chanjo ni hiyari ya mtu” na tuache propaganda za ama kuisifia au kuikosoa chanjo.

Nimeshangaa kuona “profesa” akiipigia debe chanjo ya J&J kuwa na “efficiency” ya 99.9% ilihali watengenezaji wenyewe wa chanjo hiyo wapo “openly uncertain” kuhusu hilo.

Tupunguze mapambio. COVID-19 ni maji yaliyozidi unga wa wataalam duniani kote, na ndio maana chanjo tofauti zinazidi kuvumbuliwa. Kwa kifupi tupo kwenye mapambano, sembuse yeye Profesa Mgaya!?

Tell him not to politicize serious agenda.

Asubuhi njema na kazi iendelee!
 
Kama hakuna ubabe na kujipendekeza huko NIMR, basi hakuna tatizo hata kama angekuwa amesoma Sayansi Kimu kwa sababu, yeye ni Mkurugenzi tu hapo NIMR, na kwahiyo tunatarajia awe anaongea kile kinachotoka kwa watalaamu wa hapo!!

Lakini kama kuna kujipendekeza, hapo ndo linaanza tatizo...

Ndo pale Kigwangala yule yule aliyekuwa anakejeli chanjo wakati wa Magu kwa sababu tu Magu alikuwa anakejeli chanjo; leo ndie Kigwangwala huyo huyo anayeshabikia chanjo kwa sababu tu SSH ni mfuasi wa chanjo!!!

Huyu professor ni mnafki tu
Watu Kama Hawa ni hatari Sana kwenye taifa
 
Yaani jana nilivyoanza kufuatilia kauli za Yunus Mgaya za wakati wa JPM na hizi anazotoa sasa, nikabaki hoi!!

Kabisa mkuu huyu professor anaonekana Ana unafki wa kiwango cha hali ya juu
Au ana njaa Kali , kusema kweli anashangaza sana
 
1. Nikichanjwa naacha kuvaa barakoa?

2. Nikichanjwa sitaambukizwa?

3. Nikichanjwa siwezi kuugua?

4. Nikichanjwa siwezi kufa?

5. Nikichanjwa ikija Corona ya design nyingine siwezi ambukizwa?
 
Nenda kachanje, mbona huwa mnachanjwa chale za kuzuia kulogwa na wachawi na bado mkisafiri kwenda mikoa mingine huwa mnalogwa tena.
 
Back
Top Bottom