COVID19 Tanzania: Wagonjwa wapya 35 waongezeka; idadi yafikia 88 (Aprili 15, 2020)

Sio wakati wa kulaumiana kama taifa..yashamwagika,ndio kipindi cha kuwa pamoja kuhakikisha tunavuka salama japo kwa maumivu!
 
Partial lockdown ni muhimu sasa. Watu wasiingie wala kutoka kwenye mikoa yenye maambukizi.Magari ya mizigo ya chakula na bidhaa nyingine ndio yaruhusiwe kuingia hiyo mikoa.

Tulionya, huu ugonjwa unakua exponentially na hatua madhubuti zichukuliwe mapema.
Mikusanyiko yote pamoja na ile ya makanisani na misikitini ipigwe marufuku. Viongozi wa dini wasiachwe kuwa merchants of death.

Bar na night clubs zifungwe pia haraka. Tutakwisha jamani.
 
Kubwalao kakimbilia shamba, anasikilizia tu na kuwaongopea watu wachape kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hapa ndipo napomueleewa na kumpenda waziri wa Afya wa Uganda yule Mama ni smart sana na anamiliki hekima.
Kwenye hili janga hakuna wa kupongeza wala kulaumu..hali ni mbaya kote. Si ulaya, Marekani wala Afrika, hajulikani mwenye akili wala mpumbavu wote mamoja..hali ni chafu.

Ukija kwa Waganda, nimekaa nao, Tabia zao na huu ugonjwa ni bora hata watz.
Mungu asaidie tu.
 
Vituo vya mwendo kasi leo walikuwa wanapiga dawa

Wabongo wananawa mikono vyema tu tatizo masks yani bado ukivaa unaonekana kituko cha karne ya 30

Sent from my Infinix X559C using Tapatalk
Ndugu yangu wee nani alikudanganya kunawa mikono bila kuzuia mikusanyiko kunatatua tatizo? Hata wangenawa mikono na mafuta ya moto bila kuzuia mikusanyiko ambayo ndiyo njia kuu ya kueneza virus ni bure.

Sisemi kuwa wapige marufuku watu kutoka ila wanaweza ku-minimize mikusanyiko kama ya nyumba za starehe, mikutano, ibada, masoko, sherehe nk. Kufunga shule hakuna mantiki yoyote kama watoto hao hao waliokatazwa kukusanyika shule wanakusanyika nyumba za ibada au kwenye sherehe.
 
Ili ongezeko linatufundisha nini mimi na wewe ?

Kuna watu hawataki kutulia hata kama hawana shughuli maalumu za kufanya. Hawa ndio wasambaza wa hivi virus
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…